TRA: Pikipiki (Bodaboda) kuanza kulipa Kodi ya Tsh. 65,000/- kwa mwaka

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,106
49,807
Bodaboda mmesikia hii? Sasa rasmi mtaanza kulipa Kodi. Hapa Serikali mmechemka na mnawaonea Bodaboda, maana kupata 20,000 kwa siku ni kazi kubwa ila Nchi itajengwa na Watanzania wote.

----
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema kuwa katika mabadiliko ya Sheria za kodi mwaka 2023, serikali imeweka kodi ya mapato kwa wasafirishaji wa abiria kwa kutumia pikipiki zenye magurudumu mawili (Bodaboda) ambapo watatakiwa kulipa kiasi cha Sh. 65,000 kwa Mwaka.

Hayo yamesemwa jana na Afisa mkuu wa usimamizi wa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Hamad Mterry, wakati akiwasilisha mada ya mabadiliko ya sheria mbalimbali za kodi kwa wafanyabiashara wa Mkoa wa Simiyu.

Mterry amesema kuwa hiyo ni moja ya sheria ya kodi ambayo ni mpya na imewagusa Bodaboda, ambapo watatakiwa kuichagia serikali kiasi cha Sh. 65,000 kwa mwaka, kuanzia mwaka huu wa fedha ambao tayari umeanza tangu Julai Mosi, 2023.

Afisa Mawasiliano na elimu kwa umma kutoka (TRA) Mkoa wa Simiyu, Benjamin John amesema kuwa Bodaboda anaweza kulipa kodi hiyo kwa awamu nne ndani ya mwaka, ambapo kila awamu atatakiwa kulipa Sh. 16,250.

Hata hivyo wafanyabiashara za kusafirisha abiria kwa kutumia pikipiki (Bodaboda) wanaona kodi hiyo inakwenda kuongeza ugumu wa maisha kwao, kutokana na kipato chao cha kila siku kuwa kidogo sana.

“ Ukizingatia kwa sasa kupata Sh. 10,000 kwa siku ni ngumu sana, lakini mafuta yamepanda bei, tunalipa LATRA, tunalipa Bima, bado familia inakutegemea, leo tumeletewa TRA, ukweli kodi hii inakwenda kutuumiza sana,” amesema Ntoni Deus.

My Take
Naunga mkono,Pia pombe na Sigara ziongezewe Kodi.
20230811_175701.jpg
 
Hiyo kodi ya 65000 Kwa mwaka ni sawa na shilingi 200 Kwa siku. Ni kiwango kidogo mno lakini naamini wapotoshaji watakikuza sana na kuonesha uonevu. Uzalendo ni kuhamasisha watu kulipa Kodi Kwa maendeleo yao.
Hiyo hela ni kubwa sana hasa kwa bodaboda!
Kuna watu wanafunga mwaka hawana hata akiba ya 10000 na wamefanya kazi mwaka mzima.
Kuna sehemu tuliambiwa tulipe 3000 kwa mwezi huku uswahilini na bado watu hawapati hiyo hela, ambapo ni wastani wa shilingi 100 kwa siku.
Kuitoa 3000 kwa pamoja bila sababu zinazoeleweka ni ngumu sana kwa watu wa uchumi fulani.
 
Bodaboda boda mumesikia hii? Sasa rasmi mtaanza kulipa Kodi.Hapa Serikali mumechemka na munawaonea Bodaboda maana kupata 20,000 Kwa siku ni kazi kubwa.

----
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema kuwa katika mabadiliko ya Sheria za kodi mwaka 2023, serikali imeweka kodi ya mapato kwa wasafirishaji wa abiria kwa kutumia pikipiki zenye magurudumu mawili (Bodaboda) ambapo watatakiwa kulipa kiasi cha Sh. 65,000 kwa Mwaka.

Hayo yamesemwa jana na Afisa mkuu wa usimamizi wa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Hamad Mterry, wakati akiwasilisha mada ya mabadiliko ya sheria mbalimbali za kodi kwa wafanyabiashara wa Mkoa wa Simiyu.

Mterry amesema kuwa hiyo ni moja ya sheria ya kodi ambayo ni mpya na imewagusa Bodaboda, ambapo watatakiwa kuichagia serikali kiasi cha Sh. 65,000 kwa mwaka, kuanzia mwaka huu wa fedha ambao tayari umeanza tangu Julai Mosi, 2023.

Afisa Mawasiliano na elimu kwa umma kutoka (TRA) Mkoa wa Simiyu, Benjamin John amesema kuwa Bodaboda anaweza kulipa kodi hiyo kwa awamu nne ndani ya mwaka, ambapo kila awamu atatakiwa kulipa Sh. 16,250.

Hata hivyo wafanyabiashara za kusafirisha abiria kwa kutumia pikipiki (Bodaboda) wanaona kodi hiyo inakwenda kuongeza ugumu wa maisha kwao, kutokana na kipato chao cha kila siku kuwa kidogo sana.

“ Ukizingatia kwa sasa kupata Sh. 10,000 kwa siku ni ngumu sana, lakini mafuta yamepanda bei, tunalipa LATRA, tunalipa Bima, bado familia inakutegemea, leo tumeletewa TRA, ukweli kodi hii inakwenda kutuumiza sana,” amesema Ntoni Deus.

My Take
Siungi mkono,Kwa nini pombe na Sigara zisiongezewe Kodi? Rais Samia umegombanishwa na Watu huku.
Hii ni kodi ya kitu gani???
 
Back
Top Bottom