Nkerejiwa
Senior Member
- Feb 25, 2014
- 146
- 214
Kuna mambo yanafikirisha sana, unaweza kutumia siku nzima kuwaza lakini kamwe usipate jibu hata. Fikiria, mtumishi wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 25, anatoka hadharani kutangaza kodi mpya kwa bodaboda na bajaji, kodi ambazo kwenye bajeti ya serikali ya Wizara ya Fedha 2023/24 haipo kwenye kurasa zote 277 za bajeti iliyosomwa na Mh Mwigulu Nchemba mwezi Juni 2023.
Ikiwa mtumishi mwenye uzoefu mkubwa kama huyo anafanya uzembe wa kiwango hicho, tutumie maneno gani sahahi kuonesha kwamba hii sio hujuma? Haya tuulizane ndugu zangu, ni lini jambo kama hili liliwahi kutokea hapo awali? Yani mtu atoke tu huko alipotoka, aite waandishi wa habari na kutanganza kodi mpya tena kwa kundi tata kwelikweli jamii, bodaboda na bajaji.
Kwanini hata kama ulitangaza kodi hizo isiwe kwenye madini, sigara, vinywaji au bidhaa za kilimo, bali bodaboda na bajaji? Bila shaka mtu huyu anajua fika kwamba alichokifanya kingeleta taharuki kubwa sana kwenye jamii kulingana na kundi alilolienga, na hii ingemchafua Mh Waziri, Mwigulu Nchemba, mtu aliyepewa dhamana ya kusimamia mapato na fedha za nchi hii.
Iko wazi, kwamba katika Wizara ambayo haina makandokando hata chembe, ni Wizara ya Fedha, Mama mwenyewe analijua hilo na alishawahi kutamka kwenye moja ya hotuba zake Ikulu. Hii haiwezi kuwa habari njema sana kwa watu wasiompenda Madelu, kama utakumbuka, juzi tu limetoka la uchache wa dola nchini, likadhibitiwa vikali sana kwa nguvu zote, leo mtu anatangaza kodi mpya ambayo haipo kwenye bajeti, yaani makosa yaleyale kwenye wizara ileile. Hapana, sio bure.
TRA imefanya vizuri sana kukanusha taarifa hii kwa umma. Na yule mtu lazima awekwe chini na aeleze ni kitu gani kilimsukuma kufanya kitendo cha kizembe kama kile? Kitengo kile matokeo yake ni sawa na wanachofanya watu wanaochochea machafuko kupitia maandamo nchi kwa maana, kama umetangaza kodi mpya kwa kudi la bodaboda na bajaji ambao zaidi ya 90% ni vijana na katika wakati ambao gharama za maisha zimepanda kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta, unategemea kitu gani?
Naipongeza sana TRA, maana tangazo lile la kizembe kama lingelala basi pengine tungeamka vibaya kesho.
Pia soma: