Waraka wa Wazi kwa Rais kuhusiana na Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Usalama wa Taifa ya Mwaka 2023

John Wickzer Mulholland

JF-Expert Member
Apr 13, 2023
2,329
5,062
1. Kwanza kabisa napenda kusema kwamba Mimi binafsi huwa sipendi na wala sina utamaduni wa kupenda kutoa maoni yoyote humu mitandaoni wala kwenye Jamii kuhusiana na masuala ya siasa na hata ya masuala mengine yoyote ya kijamii. Kwa kifupi Mimi siyo mtu wa kupenda mijadala kabisa hususani mijadala isiyokuwa na tija kwa watu. Hata matumizi yangu ya kawaida ya simu ktk kufanya mawasiliano ya kawaida huwa ni hafifu, lakini kutokana na unyeti mkubwa na hatari kubwa ninayoiona itakayoletwa na suala hili la Mabadiliko ya Sheria ya TISS nimejikuta nalazimika kuacha shughuli zangu zote na kutumia muda wangu ili nitoe maoni yangu juu ya suala hili. Maoni yangu yatagusa kwa ujumla dhima na muktadha wa muswada huu wa Mabadiko ya Sheria TISS, sitaeleza kila kifungu cha Sheria hiyo Bali nitatoa mawazo yangu kwa ujumla tu. Natoa maoni haya kutokana na hatari ninayoiona endapo kama Sheria hii itapitishwa pamoja uzoefu wangu binafsi kuhusiana na Jambo hili.

2. Pili napenda kusema kwamba Mabadiliko haya ya Sheria ya TISS kama yalivyo, siyo 'Mabadiliko au Marekebisho ya Sheria' kama wanavyodai wenyewe waleta hoja Bali hili ni "TANGAZO KAMILI LA VITA YA MAUAJI YA MAKUSUDI DHIDI YA RAIA WA WATANZANIA" pamoja na raia wengine wote wa kigeni waishio hapa nchini. Hii ni hatari sana kupindukia. Kwa hali halisi iliyopo nchini Tanzania kuhusiana na matendo pamoja na Mienendo ya Utendaji wa Watu wa TISS pamoja na Askari wa Jeshi la Polisi(hususani kwa baadhi ya wale ambao pia ni Mawakala wa TISS) sikutarajia kabisa kwamba yupo mtu au Mtanzania ambaye angekuwa na mawazo au fikra za kutaka kuwawekea Kinga ya kutokushitakiwa kwa watu hao wanaofanya kazi TISS (ikiwamo na mawakala wao waliopo ndani ya Jeshi la Polisi, na ktk taasisi zingine zote, haki ya Mungu naapa sikutarajia kabisa kwamba kuna mtu au watu wenye mawazo hatari kama haya ya kutaka kuwawekea kinga ili wasishitakiwe Mahakamani.

3. Nitoe RAI kwa Rais yeye mwenyewe binafsi, Tume ya Kurekebisha Sheria, Wizara ya Sheria na Katiba pamoja na Wadau wengine wote wanaohusika na Jambo hili kuchukua hatua zote za tahadhari, niwatake watafakari upya kwa kina sana juu ya suala hili. Ni vyema WAKAACHANA KABISA NA MPANGO HUU. Wakumbuke ya kwamba mpaka sasa tayari kuna watu wengi sana ambao ni WAHANGA, MAJERUHI, MANUSURA au ambao tayari Wameathirika Pakubwa sana dhidi ya Vitendo vya kihalifu ambavyo wamefanyiwa na Watu wa TISS au Jeshi la Polisi kupitia Operesheni zao za Siri (Clandestine Covert Ops) ambazo wamekuwa wakizifanya dhidi ya raia. Chonde chonde Mheshimiwa Rais, usiruhusu Jambo hili kufanyika hapa nchini, kataa hayo Mabadiiko ya kutaka kuwawekea Kinga wafanyakazi na mawakala TISS wasishitakiwe Mahakamani, kataa kabisa jambo hili tafadhali sana. Aidha, tukumbuke ya kwamba 'DHULMA' huvutia 'VISASI', na kulipa kisasi ni HAKI kwa yule mtu ambaye Amedhulumiwa Haki zake.
Vile vile, kulipa kisasi inasaidia kupunguza Maumivu na kuleta Ahueni kwa yule mtu aliyedhulumiwa haki zake.

4. Mhe. Rais, narudia tena kusema na kusisitiza kwamba kataa Jambo hili kwa sababu Wahanga watokanao na vitendo viovu vya TISS na Polisi ni wengi sana, na watu hao mioyoni mwao tayari wamebeba MIZIGO MIZITO & MIKUBWA YA CHUKI, VINYONGO NA VISASI VIBAYA dhidi ya watu hao unaotaka kuwapa Kinga ili wasishitakiwe. Watu wengi tayari wamedhurika kutokana na vitendo vyao isipokuwa wapo kimya hawasemi kwa sababu aidha hawana pa kusemea, au kutokana na sababu Fulani fulani wameamua kukaa kimya lakini siyo kwamba wameridhika na uovu au dhulma walizofanyiwa au hawana uwezo wa kuwafanya, la hasha, bali wameamua kuvumilia tu. Pia, ikumbukwe ya kwamba hawa maafisa wa TISS na mawakala wao ambao wamekuwa wakiwafanyia watu udhalimu na uovu mbaya sana (uovu wa shetani) wananchi wanawafahamu kwa sababu wanaishi nao huko mitaani, wasifikiri kwamba hawafahamiki, la hasha. Hatari kubwa ninayoiona Mimi ni kwamba, endapo kama watumishi wa TISS watawekewa Kinga ili wasishitakiwe Mahakamani kwa uovu ambao wamekuwa wanaufanya, hali hii itawalazimisha wananchi kutafuta njia nyingine mbadala za Kujihami dhidi waovu hao. Naamini kwa dhati kabisa kwamba njia hizo mbadala hazitakuwa katika mfumo rasmi wa kisheria Bali ni kulipa visasi, na hatimaye itasababisha kuibuka kwa makundi ya watu-wanaharakati wa kulipa visasi na mwisho wake kuukaribisha rasmi UGAIDI WA NDANI YA NCHI. Ndiyo, Makundi ya kigaidi ya kulipa visasi lazima yataibuka na yatapata uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa umma wa Watanzania na wapenda Haki duniani kote.

Mhe.Rais usisaini Muswada huu, achana nao. Ni dhahiri kwamba wanaopendekeza muswada huu Wana nia ovu dhidi ya raia, Muswada huu ukiupitisha lazima maadui zako wataongezeka kwa kasi ya ajabu, mfano mzuri kwa Jambo hili utazame 'status' ya mtangulizi wako kwa umma kutokana vitendo vya utekaji na mauaji vilivyofanywa na "watu wasiojulikana", ambao kwa mujibu wa mapendekezo ya muswada huu wanatakiwa "kuwekewa Kinga" ili wasishitakiwe Mahakamani kutokana na uovu huo waliofanya. Inasikitisha na inaogopesha sana kupita kiasi, it's a real hell.

5. Aidha, tukumbuke kwamba mahali ambapo hakuna Haki hapawezi kuwa na Amani, kamwe haiwezekani kabisa kutokea. Endapo kama Maafisa wa TISS na Mawakala wao watawekewa Kinga ili wasishitakiwe kabisa Mahakamani kwa uovu wao maana yake ni kwamba wako juu ya Sheria au wameruhusiwa kuzivunja Sheria makusudi na utii wa Sheria wao hauwahusu. Kwao kutenda uovu wameruhusiwa, kwa mfano kuua raia, kuwateka mateka, kuwadhuru kwa namna mbalimbali kama vile kuwekea sumu, kumwagia tindikali, kuwaweka mateka, kujeruhi, kufanyia watu mashambulizi ya kuwahujumu (Sabotage attacks), ugaidi, n.k., n.k., Katika hali kama hii unatarajia wananchi wafanye nini ili kujilinda au kujihami dhidi ya uovu wa watu hawa???Jibu la swali hili ni kwamba "wananchi wanatakiwa kujilinda au kujihami kwa namna yoyote ile watakayoona inafaa ili wawe salama, ikiwamo na kulipa visasi, kwenda nao jino kwa jino, jicho kwa jicho, jeraha kwa jeraha, n.k., n.k. kwa sababu duniani kote inafahamika wazi kwamba "Penye SHERIA pana HAKI, penye Haki pana AMANI, na penye Amani pana MAENDELEO".Kwa kifupi ni kwamba raia watalazimika kuchukua tahadhari zote za kujilinda na kujihami muda wote na kujiwekea mikakati na mipango binafsi madhubuti ya kujilinda ama kujihami, hususani kuanzisha mbinu za siri za kujihami yaani underground resistance movements (Guerrilla wars), na naamini kwamba madhara ya mbinu za kujihami kama hizi yanajulikana wazi kabisa na kila mtu (mifano mizuri ni matukio yaliyotokea kule Mkuranga, Kibiti na Rufiji)

6. Nitoe WITO kwa washauri wa karibu kwa Rais, Bunge, Mahakama, vyombo vyote vya Dola pamoja na Rais mwenyewe(kama atasoma ujumbe wangu huu) kwamba Rais kwa sasa ajikite kwenye kutafuta "Maridhiano ya Kitaifa na Wananchi Wote", siyo kufikiria kutunga Sheria mbaya, kandamizi na za hovyo zitakazoongeza zaidi ufa wa Chuki, Gadhabu, Hasira na Visasi kwa Wananchi dhidi ya Serikali, hii ni hatari sana kwa mustakabali mwema wa nchi yetu. Namuomba Rais aunde Tume ya Kimahakama ya Maridhiano ya Kitaifa (yaani Tume Haki, Ukweli na Maridhiano ya Kitaifa) ili wale watu wote (hususani wale watu ambao wanajulikana sana kwa jina la 'WATU WASIOJULIKANA', ambao naamini kwa dhati kabisa kuwa wengi wao ni 'watu wa TISS na Polisi') ambao waliohusika ktk Kuwafanyia watu Uovu wa Shetani na madhila mbalimbali kufika katika Tume hiyo ya Maridhiano na Kisha "Watubu Dhambi Zao" ili kusudi Wasamehewe Dhambi , na kwa wale wenye "Dhambi Kubwa Zisizosameheka" basi waweze kuwajibishwa kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na taratibu za nchi yetu.

Jambo hili likifanyika litasaidia kupunguza FUKUTO kwa Wahanga la kutaka Kulipiza Visasi kwa madhila, hasara, Masaibu, uovu mbalimbali waliofanyiwa na 'Watu Wasiojulikana'. Jamani nyie watu msiofahamu ukubwa wa tatizo hili, tambueni ya kwamba "Wahanga" ni wengi sana katika nchi hii, Mimi mwenyewe binafsi ninayeandika ujumbe huu pia nikiwamo, isipokuwa tunavumilia tu na tumenyamaza kimya masukudi, lakini uvumilivu pia una mwisho wake. Sitaki kuelezea kwa undani zaidi kuhusu suala hili, kwa kifupi ni kwamba sisi ambao tayari ni Wahanga wa Jambo hili tayari tuna maumivu makali sana na "tumeshajeruhika" vibaya sana kupita kiasi kutokana na suala hili, halafu tena tunaona kuna mtu mwingine anataka kuwawekea Kinga kisheria watu wale wale (watesi wa raia) ili wasishitakiwe, hii ni hatari sana na kamwe haikubaliki na haitakuja kutokea ikubalike. Itoshe tu kusema kwamba Marekebisho haya ya Sheria ya TISS hayavumiliki na wala hayakubaliki kamwe. Kwa namna yoyote ile marekebisho haya yanafaa kutupiliwa mbali, Muswada huu wa Sheria yafaa utupiliwe mbali. Hata kama wabunge wote wataupitisha bungeni, Rais ASISAINI ili uwe Sheria kamili kwa sababu Sheria hii inaenda kuwa Janga la Kitaifa. Mimi binafsi ambaye tayari nina uzoefu na jambo hili nachukulia kuwa dhamira ya kutaka kurekebisha Sheria hii ya TISS ni TANGAZO KAMILI LA VITA DHIDI YA BINADAMU. Sheria hii ikipitishwa Watanzania watarajie kukumbwa na Maafa makubwa, vifo vingi vya raia ambao watakuwa targeted na uhalifu wa kupangwa (targeted grave crimes). It will cause the Grave Human Rights violation, hivyo raia Wana wajibu wa kuchukua tahadhari zote kabisa za kupinga jambo hili, ikiwezekana kupigana vita hii kwa gharama yoyote ile mpaka wapate ushindi.

Lakini pia ninajiuliza ni nini hasa lengo la muswada huu??? Lengo ni lipi hasa la kutaka kuwawekea Kinga watu wa TISS ili wasishitakiwe kwa makosa yao wanayofanya?? Je, Mahakama zetu hazina uwezo au mamlaka au hazina nguvu ya kuwaadhibu wavunja Sheria za nchi hii mpaka sasa Serikali ione kwamba kuna haja ya kuwapa TISS mamlaka hayo ya "kuwaadhibu raia wavunja Sheria za nchi??? Je, hao waadhibiwa watarajiwa haki yao ya kusikilizwa au haki ya kujitetea kabla ya kuhukumiwa iko wapi?? Raia watuhumiwa wa TISS, je, watakuwa na haki gani ya kujitetea mbele ya TISS kabla hawajahukumiwa?? Sheria hii Mhe. Rais itazame kwa makini sana, kamwe usiisaini kwa sababu madhara ya Sheria hii ni makubwa sana na tena mabaya sana ambayo hayataweza kurekebishika.

7. Mwisho, napenda niwakumbushe kwamba matukio mabaya yanayoendelea kutokea hapa nchini kama vile kuvamiwa kwa Vituo vya Polisi(e.g. Sitaki Shari Dsm), Tukio la Hamza Mohammed pale karibu na Ubalozi wa Ufaransa/Selander Bridge Dsm, matukio yaliyotokea Mkuranga, Kibiti na Rufiji (ambayo ukiyachunguza kwa umakini mkubwa utabaini kwamba matukio yale ilikuwa kama ni Operesheni ziitwazo "Underground Resistance Movements' au kwa jina lingine yanajulikana kama "Guerrilla War") pamoja na matukio mengine mengi ambayo yametokea ktk nchi hii, hayakutokea kwa bahati mbaya Bali ni matokeo ya Kukosekana kwa HAKI, na kuwepo kwa vitendo vya DHULMA, UONEVU na MANYANYASO ya watawala au wenye wenye mamlaka dhidi ya raia (watawaliwa). Hivyo, matukio haya tuyachukulie kama FUNZO KWETU, ni muongozo mzuri kwetu juu ya namna ambavyo tunapaswa kuenenda na kurekebisha yale ambayo yanaonekana wazi kuwa ni machukizo kwa umma/raia wa kawaida.

Naaga kwa kuwakumbusha kwamba: "IF INJUSTICE BECOMES LAW, RESISTANCE BECOMES DUTY"

Ombi kwa Wana JF:
Naomba mnisaidie kuwa-tag, e.g. Tume ya Kurekebisha Sheria, TLS, ZLS, LHRC, Wizara ya Sheria na Katiba, Polisi Tanzania, n.k., n.k
 
1. Kwanza kabisa napenda kusema kwamba Mimi binafsi huwa sipendi na wala sina utamaduni wa kupenda kutoa maoni yoyote humu mitandaoni wala kwenye Jamii kuhusiana na masuala ya siasa na hata ya masuala mengine yoyote ya kijamii. Kwa kifupi Mimi siyo mtu wa kupenda mijadala kabisa hususani mijadala isiyokuwa na tija kwa watu. Hata matumizi yangu ya kawaida ya simu ktk kufanya mawasiliano ya kawaida huwa ni hafifu, lakini kutokana na unyeti mkubwa na hatari kubwa ninayoiona itakayoletwa na suala hili la Mabadiliko ya Sheria ya TISS nimejikuta nalazimika kuacha shughuli zangu zote na kutumia muda wangu ili nitoe maoni yangu juu ya suala hili. Maoni yangu yatagusa kwa ujumla dhima na muktadha wa muswada huu wa Mabadiko ya Sheria TISS, sitaeleza kila kifungu cha Sheria hiyo Bali nitatoa mawazo yangu kwa ujumla tu. Natoa maoni haya kutokana na hatari ninayoiona endaoi kama Sheria hii itapitishwa pamoja uzoefu wangu binafsi kuhusiana na Jambo hili.
2. Pili napenda kusema kwamba Mabadiliko haya ya Sheria ya TISS kama yalivyo, siyo 'Mabadiliko au Marekebisho ya Sheria' kama wanavyodai wenyewe waleta hoja Bali hili ni "TANGAZO KAMILI LA VITA YA MAUAJI YA MAKUSUDI DHIDI YA RAIA WA WATANZANIA" pamoja na raia wengine wote wa kigeni waishio hapa nchini. Hii ni hatari sana kupindukia. Kwa hali halisi iliyopo nchini Tanzania kuhusiana na matendo pamoja na Mienendo ya Utendaji wa Watu wa TISS pamoja na Askari wa Jeshi la Polisi(hususani kwa baadhi ya wale ambao pia ni Mawakala wa TISS) sikutarajia kabisa kwamba yupo mtu au Mtanzania ambaye angekuwa na mawazo au fikra za kutaka kuwawekea Kinga ya kutokushitakiwa kwa watu hao wanaofanya kazi TISS (ikiwamo na mawakala wao waliopo ndani ya Jeshi la Polisi, na ktk taasisi zingine zote, haki ya Mungu naapa sikutarajia kabisa kwamba kuna mtu au watu wenye mawazo hatari kama haya ya kutaka kuwawekea kinga ili wasishitakiwe Mahakamani.
3.Nitoe RAI kwa Rais yeye mwenyewe binafsi, Tume ya Kurekebisha Sheria, Wizara ya Sheria na Katiba pamoja na Wadau wengine wote wanaohusika na Jambo hili kuchukua hatua zote za tahadhari, niwatake watafakari upya kwa kina sana juu ya suala hili. Ni vyema WAKAACHANA KABISA NA MPANGO HUU. Wakumbuke ya kwamba mpaka sasa tayari kuna watu wengi sana ambao ni WAHANGA, MAJERUHI, MANUSURA au ambao tayari Wameathirika Pakubwa sana dhidi ya Vitendo vya kihalifu ambavyo wamefanyiwa na Watu wa TISS au Jeshi la Polisi kupitia Operesheni zao za Siri (Clandestine Covert Ops) ambazo wamekuwa wakizifanya dhidi ya raia. Chonde chonde Mheshimiwa Rais, usiruhusu Jambo hili kufanyika hapa nchini, kataa hayo Mabadiiko ya kutaka kuwawekea Kinga wafanyakazi na mawakala TISS wasishitakiwe Mahakamani, kataa kabisa jambo hili tafadhali sana.

4.Mhe. Rais, narudia tena kusema na kusisitiza kwamba kataa Jambo hili kwa sababu Wahanga watokanao na vitendo viovu vya TISS na Polisi ni wengi sana, na watu hao mioyoni mwao tayari wamebeba MIZIGO MIKUBWA YA CHUKI, VINYONGO NA VISASI VIBAYA dhidi ya watu hao unaotaka kuwapa Kinga ili wasishitakiwe. Watu wengi tayari wamedhurika kutokana na vitendo vyao isipokuwa wapo kimya hawasemi kwa sababu aidha hawana pa kusemea, au kutokana na sababu Fulani fulani wameamua kukaa kimya lakini siyo kwamba wameridhika na uovu au dhulma walizofanyiwa au hawana uwezo wa kuwafanya, la hasha, bali wameamua kuvumilia tu. Pia, ikumbukwe ya kwamba hawa maafisa wa TISS na mawakala wao ambao wamekuwa wakiwafanyia watu udhalimu na uovu mbaya sana (uovu wa shetani) wananchi wanawafahamu kwa sababu wanaishi nao huko mitaani, wasifikiri kwamba hawafahamiki, la hasha. Hatari kubwa ninayoiona Mimi ni kwamba, endapo kama watumishi wa TISS watawekewa Kinga ili wasishitakiwe Mahakamani kwa uovu ambao wamekuwa wanaufanya, hali hii itawalazimisha wananchi kutafuta njia nyingine mbadala za Kujihami dhidi waovu hao. Naamini kwa dhati kabisa kwamba njia hizo mbadala hazitakuwa katika mfumo rasmi wa kisheria Bali ni kulipa visasi, na hatimaye itasababisha kuibuka kwa makundi ya watu-wanaharakati wa kulipa visasi na mwisho wake kuukaribisha rasmi UGAIDI WA NDANI YA NCHI. Ndiyo, Makundi ya kigaidi ya kulipa visasi lazima yataibuka na yatapata uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa umma wa Watanzania na wapenda Haki duniani kote.
Mhe.Rais usisaini Muswada huu, achana nao. Ni dhahiri kwamba wanaopendekeza muswada huu Wana nia ovu dhidi ya raia, Muswada huu ukiupitisha lazima maadui zako wataongezeka kwa kasi ya ajabu, mfano mzuri kwa Jambo hili utazame 'status' ya mtangulizi wako kwa umma kutokana vitendo vya utekaji na mauaji vilivyofanywa na "watu wasiojulikana", ambao kwa mujibu wa mapendekezo ya muswada huu wanatakiwa "kuwekewa Kinga" ili wasishitakiwe Mahakamani kutokana na uovu huo waliofanya. Inasikitisha na inaogopesha sana kupita kiasi, it's a real hell.
5. Aidha, tukumbuke kwamba mahali ambapo hakuna Haki hapawezi kuwa na Amani, kamwe haiwezekani kabisa kutokea. Endapo kama Maafisa wa TISS na Mawakala wao watawekewa Kinga ili wasishitakiwe kabisa Mahakamani kwa uovu wao maana yake ni kwamba wako juu ya Sheria au wameruhusiwa kuzivunja Sheria makusudi na utii wa Sheria wao hauwahusu. Kwao kutenda uovu wameruhusiwa, kwa mfano kuua raia, kuwateka mateka, kuwadhuru kwa namna mbalimbali kama vile kuwekea sumu, kumwagia tindikali, kuwaweka mateka, kujeruhi, kufanyia watu mashambulizi ya kuwahujumu (Sabotage attacks), ugaidi, n.k., n.k., Katika hali kama hii unatarajia wananchi wafanye nini ili kujilinda au kujihami dhidi ya uovu wa watu hawa???Jibu la swali hili ni kwamba "wananchi wanatakiwa kujilinda au kujihami kwa namna yoyote ile watakayoona inafaa ili wawe salama, ikiwamo na kulipa visasi, kwenda nao jino kwa jino, jicho kwa jicho, jeraha kwa jeraha, n.k., n.k. kwa sababu duniani kote inafahamika wazi kwamba "Penye SHERIA pana HAKI, penye Haki pana AMANI, na penye Amani pana MAENDELEO"
6.Nitoe WITO kwa washauri wa karibu kwa Rais, Bunge, Mahakama, vyombo vyote vya Dola pamoja na Rais mwenyewe(kama atasoma ujumbe wangu huu) kwamba Rais kwa sasa ajikite kwenye kutafuta "Maridhiano ya Kitaifa na Wananchi Wote", siyo kufikiria kutunga Sheria mbaya, kandamizi na za hovyo zitakazoongeza zaidi ufa wa Chuki, Gadhabu, Hasira na Visasi kwa Wananchi dhidi ya Serikali, hii ni hatari sana kwa mustakabali mwema wa nchi yetu. Namuomba Rais aunde Tume ya Kimahakama ya Maridhiano ya Kitaifa (yaani Tume Haki, Ukweli na Maridhiano ya Kitaifa) ili wale watu wote (hususani wale watu ambao wanajulikana sana kwa jina la 'WATU WASIOJULIKANA', ambao naamini kwa dhati kabisa kuwa wengi wao ni 'watu wa TISS na Polisi') ambao waliohusika ktk Kuwafanyia watu Uovu wa Shetani na madhila mbalimbali kufika katika Tume hiyo ya Maridhiano na Kisha "Watubu Dhambi Zao" ili kusudi Wasamehewe Dhambi , na kwa wale wenye "Dhambi Kubwa Zisizosameheka" basi waweze kuwajibishwa kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na taratibu za nchi yetu.
Jambo hili likifanyika litasaidia kupunguza FUKUTO kwa Wahanga la kutaka Kulipiza Visasi kwa madhila, hasara, Masaibu, uovu mbalimbali waliofanyiwa na 'Watu Wasiojulikana'. Jamani nyie watu msiofahamu ukubwa wa tatizo hili, tambueni ya kwamba "Wahanga" ni wengi sana katika nchi hii, Mimi mwenyewe binafsi ninayeandika ujumbe huu pia nikiwamo, isipokuwa tunavumilia tu na tumenyamaza kimya masukudi, lakini uvumilivu pia una mwisho wake. Sitaki kuelezea kwa undani zaidi kuhusu suala hili, kwa kifupi ni kwamba sisi ambao tayari ni Wahanga wa Jambo hili tayari tuna maumivu makali sana na "tumeshajeruhika" vibaya sana kupita kiasi kutokana na suala hili, halafu tena tunaona kuna mtu mwingine anataka kuwawekea Kinga kisheria watu wale wale (watesi wa raia) ili wasishitakiwe, hii ni hatari sana na kamwe haikubaliki na haitakuja kutokea ikubalike. Itoshe tu kusema kwamba Marekebisho haya ya Sheria ya TISS hayavumiliki na wala hayakubaliki kamwe. Kwa namna yoyote ile marekebisho haya yanafaa kutupiliwa mbali, Muswada huu wa Sheria yafaa utupiliwe mbali. Hata kama wabunge wote wataupitisha bungeni, Rais ASISAINI ili uwe Sheria kamili kwa sababu Sheria hii inaenda kuwa Janga la Kitaifa. Mimi binafsi ambaye tayari nina uzoefu na jambo hili nachukulia kuwa dhamira ya kutaka kurekebisha Sheria hii ya TISS ni TANGAZO KAMILI LA VITA DHIDI YA BINADAMU. Sheria hii ikipitishwa Watanzania watarajie kukumbwa na Maafa makubwa, vifo vingi vya raia ambao watakuwa targeted na uhalifu wa kupangwa (targeted grave crimes). It will cause the Grave Human Rights violation, hivyo raia Wana wajibu wa kuchukua tahadhari zote kabisa za kupinga jambo hili, ikiwezekana kupigana vita hii kwa gharama yoyote ile mpaka wapate ushindi.
Lakini pia ninajiuliza ni nini hasa lengo la muswada huu??? Lengo ni lipi hasa la kutaka kuwawekea Kinga watu wa TISS ili wasishitakiwe kwa makosa yao wanayofanya?? Je, Mahakama zetu hazina uwezo au mamlaka au hazina nguvu ya kuwaadhibu wavunja Sheria za nchi hii mpaka sasa Serikali ione kwamba kuna haja ya kuwapa TISS mamlaka hayo ya "kuwaadhibu raia wavunja Sheria za nchi??? Je, hao waadhibiwa watarajiwa haki yao ya kusikilizwa au haki ya kujitetea kabla ya kuhukumiwa iko wapi?? Raia watuhumiwa wa TISS, je, watakuwa na haki gani ya kujitetea mbele ya TISS kabla hawajahukumiwa?? Sheria hii Mhe. Rais itazame kwa makini sana, kamwe usiisaini kwa sababu madhara ya Sheria hii ni makubwa sana na tena mabaya sana ambayo hayataweza kurekebishika.
7. Mwisho, napenda niwakumbushe kwamba matukio mabaya yanayoendelea kutokea hapa nchini kama vile kuvamiwa kwa Vituo vya Polisi(e.g. Sitaki Shari Dsm), Tukio la Hamza Mohammed pale karibu na Ubalozi wa Ufaransa/Selander Bridge Dsm, matukio yaliyotokea Mkuranga, Kibiti na Rufiji (ambayo ukiyachunguza kwa umakini mkubwa utabaini kwamba matukio yale ilikuwa kama ni Operesheni ziitwazo "Underground Resistance Movements' au kwa jina lingine yanajulikana kama "Guerrilla War") pamoja na matukio mengine mengi ambayo yametokea ktk nchi hii, hayakutokea kwa bahati mbaya Bali ni matokeo ya Kukosekana kwa HAKI, na kuwepo kwa vitendo vya DHULMA, UONEVU na MANYANYASO ya watawala au wenye wenye mamlaka dhidi ya raia (watawaliwa). Hivyo, matukio haya tuyachukulie kama FUNZO KWETU, ni muongozo mzuri kwetu juu ya namna ambavyo tunapaswa kuenenda na kurekebisha yale ambayo yanaonekana wazi kuwa ni machukizo kwa umma/raia wa kawaida.
Naaga kwa kuwakumbusha kwamba: "IF INJUSTICE BECOMES LAW, RESISTANCE BECOMES DUTY"

Ombi kwa Wana JF:
Naomba mnisaidie kuwa-tag, e.g. Tume ya Kurekebisha Sheria, TLS, ZLS, LHRC, Wizara ya Sheria na Katiba, Polisi Tanzania, n.k., n.k
Kumbe wamewekewa Kinga ya kutoshtakiwa?

Kwa hoyo List imeongezeka kutoka Rais, makamu, waziri Mkuu, Spika na Jaji?

Mmh this is sicking the Nation
 
5. Aidha, tukumbuke kwamba mahali ambapo hakuna Haki hapawezi kuwa na Amani, kamwe haiwezekani kabisa kutokea. Endapo kama Maafisa wa TISS na Mawakala wao watawekewa Kinga ili wasishitakiwe kabisa Mahakamani kwa uovu wao maana yake ni kwamba wako juu ya Sheria au wameruhusiwa kuzivunja Sheria makusudi na utii wa Sheria wao hauwahusu. Kwao kutenda uovu wameruhusiwa, kwa mfano kuua raia, kuwateka mateka, kuwadhuru kwa namna mbalimbali kama vile kuwekea sumu, kumwagia tindikali, kuwaweka mateka, kujeruhi, kufanyia watu mashambulizi ya kuwahujumu (Sabotage attacks), ugaidi, n.k., n.k., Katika hali kama hii unatarajia wananchi wafanye nini ili kujilinda au kujihami dhidi ya uovu wa watu hawa???Jibu la swali hili ni kwamba "wananchi wanatakiwa kujilinda au kujihami kwa namna yoyote ile watakayoona inafaa ili wawe salama, ikiwamo na kulipa visasi, kwenda nao jino kwa jino, jicho kwa jicho, jeraha kwa jeraha, n.k., n.k. kwa sababu duniani kote inafahamika wazi kwamba "Penye SHERIA pana HAKI, penye Haki pana AMANI, na penye Amani pana MAENDELEO"
This is Scary
 
Huwa sipendi kusoma mada zenye mirengo ya kisiasa..ila hii nimeisoma mpaka nukta..nakuunga mkono asilimia 100 kama ni kweli wanataka kupitisha huo muswada...watu watateswa na kunyanyaswa mnoo...hao TISS wataua mno raia...
Pole sana kwa madhila hayo yaliyokukuta na bado una moyo wa kuwaonea huruma raia wenzako wasipatwe na yaliyokupata..hakika Mungu atakulipia.
 
Huu uzi ni wa moto. Umegusa mambo muhimu sana.
 
Wa wekewe kinga tu ila kinga ya kifo hawana maamuzi ya Leo matokeo tutakuja kuona miaka 20 mbele na itakuwa tumechelewa San. Mungu ibariki Tanganyika, Mungu ibariki Tanganyika Mungu ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom