Bima ya Afya kwa watu wote kwa Nchi yetu bado sana, Tuanze na Wajawazito

RNA

JF-Expert Member
Mar 27, 2013
1,584
2,683
Habari wanaJF, Kwanza kabisa tukubaliane kwa Nchi yetu imekuwa shida sana kupata Takwimu za afya ,ni ngumu kujua watu wangapi wanazaliwa kwa siku , wanaofariki kwa siku , ni wastani wa watu wangapi wanapata ujauzito kwa Siku .

Hivyo kwa Uzoefu wangu nitakuja na Takwimu ambazo zitareflect kidogo hali halisi ya Afya katika nchi yetu .

Tanzania kwa sasa inakadiliwa kuwa na watu Milioni 60 ,wengi wao wakiwa wanawake hivyo tuchukue ni Milioni 32 .Ambapo kati ya hawa wanawake ambao wako katika umri wa Kuzaa yaani miaka 15-49 ni asilimia 20-25, hivyo tutachua ni milioni 8 .

Tunapozungumzia suala la BIMA kwa watu wote tunamaanisha kila mtanzania awe na uwezo wa kupata matibabu sahihi na wakati sahihi bila kuwa pesa taslimu mfukoni -malipo baada ya Matumizi .

Hali ilivyo sasa ni kwamba watanzania kama asilimia 15 tu wana bima za afya ,lakini kwa wagonjwa wanaofika hospitali nyingi asilimia 85 ni watumiaji wa Bima mbali mbali ,Asimilia 15 ni wanaolipa .

Hivyo kuna watu wengi huishia maduka ya Madawa na tiba asilia .

Kwa wastani Mtu mmoja hutumia shilingi Elfu 40-45 akienda kupata matibabu hospitali yenye hadhi ya Mkoa kwa Mara moja Gharama kati ya asilimia 20-25 ni pesa ya kumuona daktari nyingine ni dawa ,vipimo na gharama za upasuaji, hivyo kama kila mwezi watakwenda watanzania hospitalini kutibiwa na wengiwe wakafanyiwa upasuaji watu milioni 15 kati ya hizo 60 ni kwamba tutalazima kuwa na 15M x 40000 ambazo kwa haraka ni sawa na Bilioni 600 pesa ambazo ni Nyingi Sana .

Lakini hata kama tutatoa pesa za kuwaona Madaktari zikitolewa kwa wastani mgonjwa mmoja atagharamia elfu 30 mpaka 40 ambayo bado itakuwa ni zaidi ya bilioni 450 kwa mwezi kama watu milioni 15 watatibiwa .
Hivyo basi hili suala la Bima ya Afya kwa watu wote sio la kukurupukia inabidi kujipanga sana .

Kwa Utangulizi Huo napendekeza tuanze wamama Wajawazito wote ,yaani toka Mama akitambulika kuwa Mjamzito tu mpaka huduma za Kujifungua ziwe Bure .

Kwa kifupi uwekwe utaaratibu kliniki kina mama wanapewa kadi ambayo itaruhusu yeye kutibiwa popote pale mpaka ajifungue .

Tuanze na kundi hili sababu :-

1. Linamgusa moja kwa moja mama mwenyewe ,Baba na mtoto wote kwa Ujumla,hivyo kwa kumsaidia unasaidia unasaidia Jamii kwa Ujumla .

2. Ni wahanga wakubwa wa matatizo yatokanayo na Uzazi ukiachana na Mwanaume na mtoto

3.Kwa Idadi sio kubwa hivyo itakuwa rahisi kupata hizo pesa .

Tutapataje Pesa hizo ,Hapa tuachane Misaada ya watu wa Marekani hivyo kuna vyanzo viwili vikuu .

1. Ni mapato ya serikali kupitia Bajeti
2. Ni mapato ya serikali kupitia Tozo itakayo shughulika na Matibabu ya kina mama wajawazito Tu

Mfano :-Tuna laini za simu za mkononi zaidi ya millioni 50 ,Voda na Airtel wana jumla ya milioni 29 huku Tigo na Zantel 20 milioni na mitandao iliyobaki mitatu ina kamilisha .

Watanzania ni waelewa sana tukipata katika laini hizo 25 milioni tu zikawa active na wakaweza lipia 1000-1500 kwa Mwezi tutatengeneza bilioni 25 mpaka 37.5 bilioni ambazo kwa kina mama wajawazito tu zitawatosha kuokoa maisha yao .

Karibu wana JF tujadili suala nyeti la Afya kwa Wote .
 
Tutaanza na wamama wajawazito na watoto wenye Umri wa miaka 5 hadi 0.

Pia wanafunzi wa miaka 21 kushuka chini, wazee na wagonjwa wenye magonjwa Sugu.
 
  • Thanks
Reactions: RNA
Swala hili lingeanza na makundi haya maalum/ya msamaha wa matibabu yaani wajawazito,watoto chini ya miaka 5na wazee wasiojiweza kiuchumi hawa wangepewa namba/kadi maalum ambazo zitawawezesha kupata huduma za afya kituo chochote na kupitia kadi hizo vituo vifanye claiming ili kufidia gharama zilizotumika na kufanya huduma kuwa endelevu.Hii itaondoa manyanyaso hasa kwa wazee kwa kuwa vituo vitapata return zao tofauti na ilivyo sass.
 
Soma kwanza sera ya taifa ya Afya ndio ulete haya mapendekezo yako. Pili, zungumza na watu walioko kwenye hii sekta hasa wa chini kabisa, kwa UHURU kabisa wakupe hali HALISI.

Kwanza, Unapaswa kujua:

- Watoto wadogo chini ya Miaka 5 matibabu yao Ni BURE.

- Wazee, zaidi ya Miaka 60 matibabu yao ni bure.

- Wajawazito ( Wenye kadi za Kliniki ) matibabu yao Ni BURE.

Note: Nikisema BURE namaanisha BILA MALIPO.
 
Bure maana yake utalipia wewe, kodi zikipanda usilalamike. Mi najiuliza mtu ujana wote umeutumia ujajikatia bima unasubiri bure uzeeni na kutesa wananchi. Matibabu bure ni ngumu sana kwa nnchi changa lasiivo tukubali kodi kupanda kila siku
 
Soma kwanza sera ya taifa ya Afya ndio ulete haya mapendekezo yako. Pili, zungumza na watu walioko kwenye hii sekta hasa wa chini kabisa, kwa UHURU kabisa wakupe hali HALISI...
Hiyo bure wanakula wanachochangia wengine wanaopata huduma vituoni,,hili kundi la bure/msamaha ni kubwa so muda mwingine hawapati huduma wanadanganywa dawa hakuna
 
  • Thanks
Reactions: RNA
Soma kwanza sera ya taifa ya Afya ndio ulete haya mapendekezo yako. Pili, zungumza na watu walioko kwenye hii sekta hasa wa chini kabisa, kwa UHURU kabisa wakupe hali HALISI.

Kwanza, Unapaswa kujua:

- Watoto wadogo chini ya Miaka 5 matibabu yao Ni BURE.

- Wazee, zaidi ya Miaka 60 matibabu yao ni bure.

- Wajawazito ( Wenye kadi za Kliniki ) matibabu yao Ni BURE.

Note: Nikisema BURE namaanisha BILA MALIPO.
Bure wapi huko ? Jitahidi kufuatilia mambo
 
Soma kwanza sera ya taifa ya Afya ndio ulete haya mapendekezo yako. Pili, zungumza na watu walioko kwenye hii sekta hasa wa chini kabisa, kwa UHURU kabisa wakupe hali HALISI.

Kwanza, Unapaswa kujua:

- Watoto wadogo chini ya Miaka 5 matibabu yao Ni BURE.

- Wazee, zaidi ya Miaka 60 matibabu yao ni bure.

- Wajawazito ( Wenye kadi za Kliniki ) matibabu yao Ni BURE.

Note: Nikisema BURE namaanisha BILA MALIPO.
Huo ubure we unadhani watu wangejaa hospital za private ?
 
Soma kwanza sera ya taifa ya Afya ndio ulete haya mapendekezo yako. Pili, zungumza na watu walioko kwenye hii sekta hasa wa chini kabisa, kwa UHURU kabisa wakupe hali HALISI.

Kwanza, Unapaswa kujua:

- Watoto wadogo chini ya Miaka 5 matibabu yao Ni BURE.

- Wazee, zaidi ya Miaka 60 matibabu yao ni bure.

- Wajawazito ( Wenye kadi za Kliniki ) matibabu yao Ni BURE.

Note: Nikisema BURE namaanisha BILA MALIPO.
Huo utaratibu kwa sasa haupo.jaribu kufuatilia utaona.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ungeweka wajawazito na watoto chini ya Mwaka mmoja kwa kuanzia ingependeza .kiukweli matibabu ni gharama sana na raia wetu vichwa vigumu sana ukiwaambia wachange 100k kwa mwaka ni kama kuwatukana .
 
  • Thanks
Reactions: RNA
Ungeweka wajawazito na watoto chini ya Mwaka mmoja kwa kuanzia ingependeza .kiukweli matibabu ni gharama sana na raia wetu vichwa vigumu sana ukiwaambia wachange 100k kwa mwaka ni kama kuwatukana .
Lakini pia ni mtaji wa kisiasa Mama akifanikisha wajawazito kutibiwa bure atakosa mpinzani 2025
 
Back
Top Bottom