MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 10,223
- 22,299
"Bora mtu baki kuliko ndugu"
Hii ni kauli maarufu sana nyakati hizi kwasbabu ya upendo wa wanafamilia wengi kupungua baina yao. Wanafamilia wamekuwa hawapendani na kupelekea umaskini kuzidi kushamiri. Kwanza tujue kuwa bila familia imara hakuwezi kuwa na taifa imara. Mafanikio ya taifa yanaanza na familia. Familia ndo zinatoa wataalamu, wanasiasa, wanamichezo, wasanii hata viongozi wa dini. Lakini kwa upande mwingine familia ndo zinatoa mafisadi, majambazi na wahalifu wa kila aina. Kwahiyo familia sio kitu cha mchezo mchezo.
Tukija kwenye hoja kuhusu uhusiano wa umaskini na familia ndo tunajikuta tunajiuliza swali kuu "tunauondoa vipi umaskini kwenye familia?". Kimsingi kazi hii sio ndogo.. ni shughuli pevu kwelikweli yenye mchakato mrefu. Hakuna kanuni sahihi jinsi gani umaskini utatokomezwa lakini kuna mambo ya kuzingatia bila kujali mbinu gani inayotumika na wanafamilia kupambana na umaskini. Kuna familia nyingi zilizojiondoa kwenye umaskini kwa kupitia elimu. Mbinu ya elimu ni ya uhakika sana. Lakini kuna zingine kupitia vipaji vya wanafamilia wakajikuta pia wamefanikiwa. Kina Filbert Bayi, Diamond Platinumz, Christiano Ronaldo, Harmonize, Shilole, Kajala, Steve Nyerere na wengine ni mifano ya watu walioweza kuushinda umaskini kupitia vipaji vyao.
Lakini ili umaskini kutokomezwa lazima familia nzima iwe kitu kimoja na wapendane. Yaani asitokee mtu kujiona bora kuliko wenzake au kuleta ubinafsi na wivu. Mara nyingi huwa anatokea mwanafamilia mmoja ambaye nadhani Mungu humtumia kuondoa umaskini wa familia. Kwa mfano anaweza kutokea mtoto mmoja mwenye akili za ajabu akaja kupata kazi ya mshahara mnono na marupurupu akawainua wenzake. Au mwingine akaanza biashara na kufanikiwa kisha kuibeba familia yake.
Diamond Platinumz ni mfano hai mrahisi wa mwanafamilia mmoja kufanikiwa na kuiinua familia yake nzima. Lakini hiyo huwa inawezekana endapo wanafamilia wanaheshimiana na kupendana. Tukiangalia Diamond ni mdogo kwao lakini iko wazi familia yake inamheshimu na kumpenda hivyo wakajikuta na wao wananufaika. Lakini pia Diamond angeweza kuwa mbinafsi na kufakamia hela zake peke yake na vidosho ila kutokana na upendo ndo tunaona pia ndugu zake wanaofahamika na wao wako vizuri.
Je, huu umoja na upendo inawezekanaje? Jibu ni kupitia wazazi. Baba na mama lazima wawajibike kuwajengea watoto roho za kupendana na kusaidiana kuanzia utotoni. Mimi baba yangu toka utotoni lazima awepo kwenye chakula cha usiku na familia nzima. Hata baada ya kula lazima awapigie stori mbalimbali na kujikuta familia nzima mnafurahi. Wale kina baba wanaotumia muda wa jioni kuwa bar na kurudi watoto wamelala mnafanya upumbavu. Hata kina mama pia lazima wawe wakali sana kwa watoto wenye tabia za ubinafsi ili asije akawa na tabia hiyo. Wazazi wanapoachana huwa ni huzuni duniani mpaka mbinguni, lakini hata ikifikia point lazima muachane basi hakikisheni mnapambania watoto wenu wakue vizuri.
Single mama pia hakuna jinsi, lazima mpambanie watoto wenu wakue vizuri wakiwa na maadili mazuri. Mama Diamond ni mfano mzuri wa mama aliyehakikisha mwanae anafanikiwa na kuwa na maadili. Yule kijana ana nidhamu. Lakini ile nidhamu yake ni kazi ya Bi Sandra.