Naishangaa Serikali, sidhani kama ina nia ya dhati kukabiliana na umaskini

The Next MP

Member
Nov 15, 2023
37
43
Kupitia NSSF, na PSSSF serikali imekuwa ikiwanyima wananchi wake mafao hasa upande wa NSSF mfuko ambao ni wa watumishi wa sekta binafsi.

Fedha hizi ni za wananchama walioko kwenye ajira makampuni na taasisi mbalimbali. Tabia moja ya ajira za sekta binafsi sio kama serikalini. Sekta binafsi Kuna baadhi hutoa mkataba wa mwaka mmoja mmoja. Mtu akifanya kaz miaka miwili minne au mitano boss anaweza kumtimua au kampuni inaweza kushuka kiuwezo na hatimaye mtu anapoteza kazi.

Shida inakuja pale mtu kapoteza ajira hana mwelekeo akiangalia mafao yake Kuna milioni Tano sita au kumi na kitu huko. Anaona kuliko kukaa Bure kuranda randa mtaani bila kazi ni bora achukue pesa yake afanye uzalishaji.

Akienda NSSF Sasa aanakutana na vigingi anakula chuma Cha hatari mwenyewe anaamua kukata tamaa anaacha hata kufuatilia.

Sasa kwanini serikali isiruhusu watu wa sekta binafsi kuwa wanapewa pesa zao ili kusaidia kupunguza umaskini? Kuwazuilia watu pesa zao ni kutengeneza na kuongeza umaskini zaidi, waachieni watu wachukue pesa zao waendeshe familia zao, wafanye miradi yao, wafanye biashara zao.

Kwanini muwakatalie wakati ni pesa zao? Hivi serikali ipo serious kupambana na umaskini?
 
Haipo serious... sababu ingekua serious ingepambana na umeme (biashara nyingi ukuaji wake unategemea umeme) then internet sababu taarifa zote muhimu unazipata online na kuna ujuzi mwingi tu wa kujifunzia online bado kuna namna nyingi wafanyabiashara wananufaika kupitia mitandao, ila namba 1 mpaka wasaidizi wake ni genge la watu wasio na akili wala maono
 
Back
Top Bottom