Bila UMAFIA hujawa tajiri bado. Umafia ndio dira ya utajiri

Mtu anataka pesa hiyo hiyo akalewe halafu anataka utajiri, anataka pesa hiyo hiyo akahonge vimada (michepuko) halafu anataka utajiri!

Utajiri wa bahati mbaya au bahati nzuri, siyo utajiri huo. Tuwache kujazana ujinga.
 
Kwanini mazingira ya bongo sio rafiki?

Mbona wageni wengi wanakuja kufanikiwa hapa...

Kuna mzungu anasema ukiwa U.k hakuna fursa ambayo haijafanywa kiusahihi..hata ukienda na billions kutoboa sio rahisi..

Ila Tanzania/Africa kuna 1000 opportunities.
Raia wa kigeni wakianzisha biashara bongo wanapewa msamaha wa kodi kwa miaka mi5 ya kwanza

Lakni ww mwenyeji ukifungua biashara yako leo, tegemea kesho kufatwa na TRA, FIRE, H/MASHAURI, TBS, TFDA, 0SHA, NEMC and the likes!!

Kwa namna hyo unafikiri utatoboa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ngoja niwape tafsiri halisi ya UTAJIRI

Iko hivi .....
Utajiri Umegawanyika katika Pande kuu mbili (2).

1)Utajiri wa Kiroho (Spiritual world)

2)Utajiri wa Kimwili (physical world)

Utajiri wowote ule utaouona unamilikiwa duniani basi Ulianzia ndani ya roho.

Kisha ukaja kudhihirika kwa macho ya Nyama (Physical world).


Foundation sahihi ya Kiroho ndio ita determine wewe ni tajiri wa aina gani. Sasa hapo kwenye Foundation ya Kiroho hapo ndipo Siri yenyewe ilipo !




Hivyo utakuta utajiri wa material things Huwa una principle ya "Accumulate More & More".

Tukumbuke Kuna utofauti Kati ya Accumulate na Abundance !
Roho ndo kitu gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tajiri kuingia peponi ni kipengele maana wengi wanafanya kazi nyingi na shetani kuliko Mungu. Wanaua just to get shit straight
Mie sioni tatizo hapo maana mbinguni kwenyewe hatuendi na mwili ila roho tu sasa kwa nini uteseke duniani?
Ukipata mchongo wa utajiri hata kama ni uchawi we piga ili ule raha duniani halafu ukifa itakayoenda motoni ni roho tu na hakutakuwa na wa kukucheka huko.
Mie nikipata mganga wa kuaminika wa utajiri niko tayari hata kutoa kafara wanaccm hata wanne au zaidi.!
 
Mambo haya ya "umafia" yapo barani Afrika tu,

Kwa vile ni mifumo ya hovyo iliyopo tangu enzi na enzi.

Waafrika wengi walio fanikiwa legally ni wachache sana kuliko wale walio fanikiwa illegally.

Kuna nchi zina mifumo mizuri, Kiasi kwamba ukijituma tu na ukatia bidii hata kuwa tajiri ni rahisi sana.

Afrika kumejaa mifumo ya rushwa, uhujumu, upigaji, umimi, ubinafsi na uhovyo wa kila aina kiasi kwamba ni ngumu mtu kutoboa kwa legal ways.
Mzee Hata hao ma billionaire was mbele nao baadhi ni 🔥🔥, ni wakwepa Kodi na ma lobyist
 
Mpaka ufikie level ya kuwa tajiri, ni lazima uwe umefanyiwa umafia hadi na wewe unakuwa mafia mkubwa.

Utajiri ni himaya, kila jicho linaiangalia himaya kwa husda. Kuna uchawi, ujambazi, figisu na michezo yote michafu.

Ukiwa tajiri utajilinda wewe na uzao wako kiroho, kimwili na kitàaluma ili usipitwe na teknolojia.

Bila kuwekeza kwenye teknolojia utajiri wako utakuwa ni wa muda mfupi tu.
Bado natafuta mwalimu wa kufundisha courses za computer kama vile word excel PowerPoint publisher adobe acrobat chatgpt windows operating system ,Linux operating system etc.kama una hiyo skillset usisite kunicheki.
 
Amancio Ortega ni bonge la drugs dealer.

Mbona hujawataja akina Bill Gates, Abrahamovich au sababu ushajua walipataje pataje utajiri wao?

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
Abrahamovich nafaham umafia wake na Rafiki yake Putin. Bill Gates sifahamu chochote mi nilidhani amepitia njia za kawaida tu bila makandokando yoyote, kwani ana tuhuma gani?
 
Kuvaa nguo za gharama, na kula vyakula vya bei mbaya migahawani ni kiashiria cha umasikini.

Unaponunua nguo za gharama kila wakati na kula vyakula kwenye migàhawa ya kifahari, jua kwamba wewe ni mrija wa utajiri wa mtu fulani. Unampelekea pesa, je wewe anakupa nini?

Ukipunguza matumizi yasiyo ya lazima, ukaanzisha kabiashara kako kadogo, utatamani kukakuza na kukaongeza kabiashara kako hako.


Pia chakula cha kula nyumbani kiko healthy na fresh
Inafikirisha sana aisee
 
Back
Top Bottom