Upembuzi wa kitabu cha mtu tajiri zaidi babylon

Aug 25, 2019
79
80
UPEMBUZI YAKINIFU WA KITABU CHA MTU TAJIRI ZAIDI BABYLON

"THE RICHEST MAN IN BABYLON"

Na LEONARD JULIUS SHIGANGA WA MWANAMATINGATINGA.
KWAMBA,

THE RICHEST MAN IN BABYLON ni kitabu kilichoandikwa na GEORGE S CLASON, kinachoongelea siri ya utajiri iliyokuwa ikitumika na ustaarabu wa kale kabisa katika mji wa babeli ambapo siri hizo mpaka sasa zinafanya kazi licha ya mabadiliko makubwa ya sayansi ya teknolojia yaliyotokea hadi sasa tupo kwenye ulimwengu wa haraka yaani "Very fast paced world" AU ulimwengu wa habari "Information world".

Kwa undani zaidi, KITABU hiki kinaongelea maeneo tofauti ya usimamizi wa fedha kuanzia jinsi ya kuweka MIPANGO ya kifedha kwa maisha yako ya sasa na baadaye, jinsi ya kusimamia UTAJIRI wako kwa kuujenga, kuutunza na kuukuza zaidi na mwisho namna gani haya yote yanavyoweza kuathiri maisha yako ya sasa na ya baadae.

Nakukaribisha sana twende pamoja kwenye uchambuzi wa kitabu hiki ili uweze kuondokana na changamoto za kifedha kama zinakukabili kama kuondokana na madeni mabaya, kuweza kuweka akiba, kuweza kuiwekeza akiba ya fedha zako kwenye maeneo sahihi yanayokuwa na thamani kubwa kadri siku zinavyoenda ili uweze kuwa huru kifedha.

Mtu aliyetamani kumiliki dhahabu "The Man Who Desired Gold"

Miaka kadhaa iliyopita katika mji wa BABELI "BABYLON" kulikuwa kuna mtu anayeitwa Kobbi na Bansir. Katika mazungumzo baina ya watu hawa wawili Bansir alikuwa akilalamika kuwa katika maisha yake amefanya kazi sana lakini akijiangalia hakuna mali alizokusanya na kuonyesha kwa watu tofauti na juhudi alizoweka.

Katika kipindi kile fedha iliyokuwa ikitumika ni DHAHABU, hivyo walikuwa wakiongelea kiasi cha DHAHABU walichoingiza kwa miaka yote waliofanya kazi, wakijiangalia hawana hata DHAHABU ya kuonyesha kwa kipindi chote walichofanya kazi, DHAHABU zote walizokuwa wakipata wamezitumia na kubaki hawana chochote.

Katika mazungunzmo yao ya msingi walikuwa wanajadili vipi wataweza kutengeneza utajiri maana kwa njia walizokuwa wanatumia licha ya juhudi kubwa katika kazi hawakuweza kutengeneza utajiri, katika mazungumzo yao walikuwa bado hawajakata tamaa, walikuwa wanaamini kuna namna wanaweza kufanya au kuna mwongozo wanaweza kutumia na hatimaye kupata utajiri. Kadri walivyokuwa wanazungumza wakakumbuka kuna rafiki yao tangu enzi za utoto wao ambaye ana mafanikio makubwa na utajiri aliyeitwa ARKAD ambaye alikuwa akiitwa (MTU TAJIRI ZAIDI BABELON).

Kimusingi kila mtu ana muda wa kutosha kutengeneza utajiri lakini wengi wetu tunauacha upotee bure bila kufanya vitu vya maana.

MTU TAJIRI ZAIDI BABELON "THE RICHEST MAN IN BABYLON"

Watu hawa yaani, Kobbi na Bansir walihakikisha wanakutana na Arkad ili awape siri alizotumia na anazoendelea kutumia kupata na kuendelea kuwa tajiri zaidi.

Baada ya kukutana na Arkad, arkad aliwaambia Kobbi na Bansir sababu zinazowafanya washindwe kukusanya utajiri huenda wameshindwa kufahamu sheria ambazo ndiyo zinazosimamia UTAJIRI, sheria au mwongozo unaoongoza jinsi ya kutengeneza UTAJIRI, kuusimamia na kuukuza zaidi.

ARKAD aliendelea kuwaambia sheria ya kwanza aliyoanza kuitumia na anaendelea kuitumia mpaka sasa ni kwamba anahakikisha asilimia 10 ya kipato chochote anachoingiza anajilipa yeye kwanza na kuweka akiba.

ARKAD aliendelea kuwaeleza, bila kujali kiasi gani unaingiza kiwe kidogo au kikubwa, lazima ufuate sheria hii ya kujilipa asilimia 10 ya kipato hicho ulichoingiza, hapa siyo swala la umeingiza kiasi gani swala ni umejilipa kiasi gani.

Mara zote jilipe wewe kwanza. Kila fedha unayoingiza unaweza kuigeuza kama mtumwa wa kukufanyia kazi.

Bila kujali kiasi gani unaingiza kiwe kidogo au kikubwa cha msingi mara zote jilipe wewe kwanza. Kimsingi katika mazungumzo haya walipata mwanga wa jinsi ya kuanza ili waweze kutengeneza na wao utajiri. Pia kuna mambo mengine aliyowashirikisha kwani na yeye alijifunza kutoka kwa mtu wa kwanza TAJIRI katika babeli aliyeitwa Algamish. Kimsingi alijifunza mambo 4 yafuatayo.

JAMBO LA KWANZA: Ishi chini ya kipato chako.
JAMBO LA PILI: Tafuta ushauri mzuri wa sehemu ya kuwekeza fedha zako kutoka kwenye watu wenye weledi na uzoefu mkubwa kwenye eneo hilo.
JAMBO LA TATU: Usikubali kushauriwa na mtu ambaye hayupo au hafanyi iwe ni uwekezaji au biashara husika.
JAMBO LA NNE NA MWISHO: Jifunze jinsi ya kuifanya fedha ikufanyie kazi.

Sheria 7 kwa ajili ya kuwaponya Watu wa babeli waliokuwa wanaangamia kwenye lindi la umasikini.

Katika nchi hiyo, Mfalme wa babeli aliyeitwa Sargon alikuwa na hofu juu ya mji na watu wake kwani kadri siku zinavyoenda watu walikuwa wanazidi kuwa masikini. Kimsingi umasikini ulikuwa ukiongezeka kadri muda ulivyokuwa unaenda. Hivyo mfalme alimtafuta mtu tajiri babeli Arkad ili aweze kumshauri namna ya kufanya ili aweze kuwasaidia watu wake. Alipokutana na ARKAD alimueleza mfalme hadithi yake jinsi alivyoweza kujenga utajiri wake kuanzia chini kabisa kwa kutumia siri 7, hivyo alimfundisha mfalme siri 7 kama watu wake watazitumia wataweza kuondokana na umasikini na babeli ikaweza kushamiri zaidi. Siri hizo 7 ambazo ARKAD alimfundisha mfalme ni kama zifuatazo.

SIRI YA KWANZA: Kipato chako ndicho chanzo cha kwanza cha kutengeneza utajiri, weka akiba angalau asilimia 10% ya kipato chako unapokipokea.

Kwa kila senti 10 unazopokea, tumia senti 9 na baki na senti 1. Hatimaye, kwa kufanya hivyo utaweza kutunisha mfuko wako. Fedha nyingi zitatiririka kwako kama hautatumia fedha zako zote.

SIRI YA PILI: Dhibiti matumizi yako.

Weka mpango wa bajeti kwa matumizi yako. Matumizi yako muhimu yatakuwa yanakuwa na kuongezeka mara zote kama hautokuwa na mpango madhubuti wa matumizi yako. Usichanganye matumizi na tamaa. Tuna tamaa zaidi ya uwezo wa vipato vyetu. Hivyo tunatakiwa kudhibiti matumizi yetu ya msingi. Weka asilimia 10 kwa ajili yako. Matamanio yoyote yaliyo nje ya bajeti yako achana nayo. Endelea kuiboresha bajeti yako. Kwa kuwa na mpango bora wa bajeti ya matumizi yako utaweza kutunisha mfuko wako na hatimaye kujenga utajiri. Kumbuka daima kuwa " siku zote MANUNUZI hujitahidi kutanuka na kuongezeka ili yakutane na MAPATO kila yanapoongezeka"

SIRI YA TATU: Zifanye DHAHABU zako ziweze kuongezeka Zaidi na Zaidi.

Zifanye DHAHABU zako zikufanyie kazi na kuzalisha DHAHABU nyingi zaidi. Tengeneza kipato ambacho uwe unafanya kazi au umesafiri chenyewe kinaingia bila uwepo wako. Kipato hiki ndiyo UTAJIRI halisi ulivyo. Zifanye FEDHA zako zikufanyie kazi wewe kwani ndiyo maana ya UTAJIRI.

SIRI YA NNE: Linda Hazina yako Isipotee.

Jifunze kulinda FEDHA zako kidogo ulizonazo kabla haujapata FEDHA nyingi za kuzisimamia. Jifunze kwa umakini kabla haujafanya uwekezaji. Usikopeshe fedha kwa watu ambao hawawezi kukulipa. Usiruhusu tamaa zako zikufanye ufanye maamuzi ya kijinga ya matumizi ya FEDHA zako au uwekezaji. Pata ushauri kwa mtu mwenye hekima ambaye amewekeza kabla yako sehemu hiyo na yupo tayari kukupa ushauri wa bure. Wekeza sehemu salama na rahisi kuchukua fedha zako.
SIRI YA TANO: Miliki Nyumba ya kuishi.

Kila mtu ni vyema kumiliki nyumba ya kuishi, kwani atapunguza gharama za maisha na hivyo kubaki na FEDHA nyingi za kutunza na kufanya uwekezaji.

SIRI YA SITA: Tengeneza mazingira ya kuwa na kipato cha uhakika katika uzee wako.

Fanya maandalizi sasa ya kuwa na kipato cha uhakika miaka ijayo, utakapokuwa mzee na hauna uwezo wa kuingiza kipato. Kwani kwa kuwa na maandalizi sasa utaweza kuishi maisha bora wewe na familia yako yasiyo na msongo mkubwa wa mawazo.

SIRI YA SABA NA YA MWISHO: Ongeza uwezo wako ili kupata kipato kikubwa zaidi.

Matamanio ya kuongeza kipato chako ni muhimu na yenye mashiko. Kimsingi ni kitu unachotakiwa kuwa nacho muda wote kwani kitakusaidia uweze kujifunza zaidi jinsi ya kukusanya mali. Kimsingi matamanio yanatakiwa kuwa rahisi na yanayoeleweka. Kulifahamu kusudi lako mapema kutaongeza zaidi uwezo wako na hivyo kukuza kipato chako. Utaweza kupata zaidi kwa kufanya shughuli zako kwa msimamo na huku ukiwa unaongeza ujuzi zaidi. Jifunze zaidi unachofanya ili kuwa mbobezi na hatimaye utaweza kulipwa zaidi. Kadri unavyojifunza zaidi, ndivyo unavyoweza kuongeza kipato chako zaidi.

JINSI YA KUTENGENEZA BAHATI YAKO.

Mbali na siri alizotaka mfalme kwa mtu tajiri babeli amshirikishe ili ziweze kuwasaidia watu wake, PIA alimuomba amuelezee kama inawezekana mtu kupata bahati itakayokufanya uwe na utajiri. ARKAD hakutaka kuongea mambo mengi, alimueleza mfalme kuwa bahati nzuri ni fursa unazokutana nazo unapokuwa umefanya maandalizi ya kutosha. Mara nyingi bahati huwa zinawatokea watu ila watu wanashindwa kuzichangamkia. Lazima uchukue hatua pale bahati inapojitokeza. Lazima uachane na uvivu, uzembe na hali ya kutokuchukua hatua na kuhairisha maamuzi unayopaswa kuchukua. Kuvutia bahati nzuri, ni lazima sana uchangamkie fursa zinazojitokeza. Bahati nzuri inaweza kutokea kwa kuzipokea na kuzifanyia kazi fursa zinazojitokeza. Hatua lazima zichukuliwe ndiyo bahati nzuri ya mafanikio inaweza kutokea.

Namna bora na sahihi ya kukutana na bahati nzuri ni kuwa tayari muda wowote kukutana nayo, na namna sahihi ni kuwa katika mchakato sahihi, mchakato sahihi wenyewe ni kufanya kazi kwa utofauti, kujilipa kwanza kabla ya matumizi ya kipato chako, kuwekeza akiba yako baada ya kupata ushauri kwa watu wenye hekima na uzoefu wa uwekezaji huo.

SHERIA 5 ZA DHAHABU " THE 5 LAWS OF GOLD"

Hali kazalika, Kalabab aliwauliza watu wake, kama watapewa begi kubwa la DHAHABU au mwongozo wenye maaarifaa yatakayo wasaidia kuwa na hekima watachagua nini. Watu wote walisema watachagua begi kubwa la DHAHABU, Kalabab aliwaambia hivi ndivyo mbwa mwitu angefanya kwa kuhakikisha anakula leo kila kitu bila kukumbuka kesho yake itakuaje. Aliendelea kuwahadithia kuhusu Nomasir, mtoto wa kiume wa ARKAD. Nomasir alipewa DHAHABU na mwongozo wenye maarifa yenye hekima na baba yake, ili aweze kuziongeza dhahabu zaidi. Miaka 10 baadaye alitakiwa amuonyeshe baba yake jinsi alivyotumia mali ile kutengeneza mali zaidi, lakini alikuwa hana cha kuonyesha, kwa sababu hakufuata mwongozo ule aliopewa na baba yake, alipoanza kuufuata mwongozo ule aliweza kutengeneza UTAJIRI mkubwa.

Hivyo nomasir alimweleza kalabab SHERIA 5 ZA DHAHABU alizofundishwa na baba yake.

SHERIA YA KWANZA: Dhahabu zinakuja na kuongezeka kwa mtu ambaye ataweka asilimia 10 kwa ajili ya siku zijazo na familia yake,

SHERIA YA PILI: Dhahabu zinamfanyia kazi mmiliki wake kama atazitumia vizuri na pia zitaongezeka mara dufu.

SHERIA YA TATU: Dhahabu zinakaa kwa mwekezaji mwenye hekima.

SHERIA YA NNE: Dhahabu zinamkimbia mtu ambaye anawekeza maeneo ambayo hayajui, hana ujuzi nayo, pia hajapata ushauri kutoka kwa mtu ambaye ana utaalamu na maeneo hayo anayotaka kuwekeza.

SHERIA YA TANO: Dhahabu zinamkimbia mtu anayelazimisha kupata zaidi au kufuata ushauri kwa watu wanaotaka kujinufaisha binafsi au kuwekeza kwenye maeneo ambayo hana uzoefu nayo bali kwa tamaa ya kupata zaidi.

MWISHO: Alimalizia kwa kusema, utajiri unakuja na kuondoka haraka kwa wale ambao hawaelewi vizuri sheria za DHAHABU. Utajiri wa kweli na halisi unatengenezwa taratibu kwa muda mrefu.

Ushauri kutoka kwa mtu anayefanya biashara ya kukopesha.

Rodan mtengenezaji wa vipuri alijikuta ana kiasi cha vipande 50 vya dhahabu. Hivyo aliamua kutafuta ushauri kutoka kwa Mathoni ambaye anafanya biashara ya kukopesha, kwani alikuwa hajui avifanyie nini vipande vile vya dhahabu. Mkopeshaji alimwabia Rodan aina ya mikopo anayoweza kuwapa watu, kuwa kwa kila mkopo anaotaka kumpa mtu lazima ahakikishe kuna dhamana ya mkopo huo kama jengo, fedha, marafiki au familia ya mkopeshwaji.

Alimwambia asimkopeshe rafiki yake, kama ana tamani kumsaidia sawa kwani hii itamuondolea mzigo mkubwa kwenye akili yake na kuharibu mahusiano. Mkopo mzuri anaoweza kuutoa na kuwa na uhakika wa kupata FEDHA yake ni ule unaowekewa dhamana ya mali yenye thamani kubwa kuliko thamani ya mkopo uliotolewa. Mkopesha mzuri huzingatia na kuwa makini na dhamana kwanza ya mkopo anaotoa kuliko kuwa na tamaa ya faida atakayopata baada ya kukopesha.

Kimsingi hayo ndiyo aliyomueleza mkopeshaji yule Rodan kwani kama hatofanya hivyo, anaweza kupoteza akiba yake ya vipande 50 vya DHAHABU alivyovitunza.

UKUTA WA BABELI.

Banzar mlinzi wa geti kuu la kuingilia mji wa babeli, alikuwa mtu wa kwanza kutoa taarifa kuhusu wavamizi waliozunguka mji wa babeli. Banzar aliendelea kulinda usiku na mchana na kuwaangalia maadui wasivamie na kuingia ndani ya mji. Baada ya wiki 3 walinzi wa mji waliweza kuwathibiti maadui na kuwashinda na kuthibitisha jinsi walivyo imara. Mji wa babeli ulikuwa imara kuwathibiti maadui wowote waliotaka kuvamia na kutawala mji huo.

Wafanyabiashara wa ngamia katika mji wa babeli.

Tarkad alichukua fedha kwa watu huku akiwa hajapata chakula kwa siku mbili. Alikutana na rafiki yake ambaye ni mfanyabishara wa ngamia aliyeitwa Dabasir. Dabasir alimuulizia kuhusu fedha alizokuwa nazo. Huku akimuelezea kipindi alichokuwa mtumwa Syria. Alikuwa na madeni mengi na kumwambia hakuna mtu ambaye anadaiwa anaweza kujiheshimu na kuheshimika, lazima ataendelea kuwa mtumwa maisha yake yote.

Aliendelea kumueleza makosa makubwa ya FEDHA aliyoyafanya katika mji wa babeli na kumpelekea kuwa na mzigo mkubwa wa madeni na kuchukuliwa kama mtumwa syria. Mke wa bwana wake alimuonea huruma na kumpa fursa ya kutoroka.

Alichukua ngamia na kuondoka Syria kwenda jangwani, alipokuwa ugenini alikuwa anatambua makosa yake. Mfano madeni yake yalikuwa ni adui yake mkubwa, alikuwa na rafiki yake mwaminifu babeli anataka kulipa madeni yake. Alirudi babeli na kukutana na watu wote waliokuwa wanamdai na kuwaambia wawe wavumilivu kwani kwa sasa nafanya kazi, hivyo atakuwa anawalipa kidogo kidogo mpaka atakapo maliza madeni yake.

Mkopesha wa babeli Mathon alimsaidia kupata kazi ya kuwatunza ngamia, alifanya kazi kwa bidii na kulipa madeni yake yote. Aliongea haya yote kwa Tarkad ili aweze kufuata mfano wake kwa kufanya kazi kwa bidii hata kama una madeni makubwa kiasi gani utaweza kuyalipa yote na kubaki ukiwa huru. Pia unaweza hata kuondokana na utumwa kama utafanya kazi kwa bidii na kuwa na nidhamu na kipato unachoingiza.

Mtu mwenye bahati Babeli.

Sharru Nada, anasafiri na mjukuu wa rafiki yake, Hadan Galu. Sharru anamwambia Hadan mwanzoni alikuwa mtumwa, hivyo lakini alipo uzwa kwa bwana aliyekuwa anafanya kazi za kuoka mikate alipata bahati kwa sababu alikuwa na shauku ya kujifunza kwa bidii kazi ile na biashara ile. Baada ya kuifanya kazi ile na biashara kwa ustadi mzuri aliweza kununua uhuru wake. Pia hata babu yake Hadan alimweleza alikuwa mtumwa kama yeye ila alinunua uhuru wake mapema kabla yangu. Wakati Mimi na Babu yako tulipokutana tena babu yako alikuwa tayari kashaachiwa huru na mimi niliuzwa tena kwa bwana mwingine. Babu yako alinunua uhuru wangu, kwa kweli hadithi hii ilimstua sana Hadan. Kuanzia hapo aliondoka na mtazamo na msimamo kuwa kazi ndiyo njia sahihi kuitumia kupata mafanikio.

MWISHO

Kupitia kitabu cha mtu tajiri zaidi kwenye mji wa babeli, kuna mambo yafuatayo unayoweza kujifunza zaidi.

JAMBO LA KWANZA: Anza kutunisha mfuko wako kwa kujilipa kwanza asilimia 10 ya kila FEDHA au kipato unachoingiza bila kuacha hata mara moja.

JAMBO LA PILI: Dhibiti matumizi yako, sababu ya kushindwa kudhibiti matumizi yako ni matumizi mengi yasiyo ya lazima uliyoyapa kipaumbele na kutawaliwa na tamaa. Hivyo kuwa na bajeti ya matumizi yako ili ubaki na fedha ya kuweka akiba.

JAMBO LA TATU: Akiba yako hakikisha unaiwekeza kwenye maeneo yanayoweza kuifanya iongezeke zaidi.

Linda hazina yako isipotee, hakikisha unawekeza sehemu ambayo unauzoefu nayo au kupata ushauri kwa watu wenye uzoefu na usikubali kutawalia na tamaa ya kupata zaidi kwa kuwekeza sehemu ambazo siyo sahihi. Utajiri ni mchakato siyo tukio la mara moja. Wekeza sehemu sahihi kwa msimamo wa muda mrefu.
JAMBO LA NNE: Miliki nyumba ya kuishi, ili uepuke gharama za kulipa kodi. Unapoepuka gharama za kodi unaongeza uwezo wako wa kuweka akiba na kuwekeza zaidi.

JAMBO LA TANO: Tengeneza mazingira ya kuwa na uhakika wa kipato chako kwa siku zijazo. Kila mtu lazima afikiri kuhusu hatima ya maisha yake ya baadae atakapokuwa mzee hana uwezo wa kufanya kazi na kuzalisha kipato. Kama muda haukukusaidia kujifunza, njia bora ni kuwa kuijali familia yako ni kwa kufanya maandalizi yako sasa utaishi vipi utakapo staafu.

Mtu tajiri anasema, weka akiba na wekeza akiba hiyo kwani itakusaidia katika uzee na ulinzi wa familia yako pia.

JAMBO LA SITA: Ongeza uwezo wako wa kuingiza kipato, unaongeza uwezo wako huo kwa kujifunza na kuwa na hekima na kuwa na ujuzi zaidi. Hivyo ni deni kwa kila mtu kujenga uwezo utakaomsaidia kufikia malengo yake.

KWA LEO NIMEISHIA HAPO THANK YOU VERY MUCH FOR READING THIS GOOD NEWS!

Think AND TAKE STEPS
shiganga2010@gmail.com
 
Asante sana ndugu yangu Napoleon the second nimesoma yote zaidi sana nimejifunza na kujifunza na kujifunza tena.
Hiki kitatu nakutana nacho sana kwenye mitandao lakini lugha ndio changamoto ! Sikuwahi kujua kama kina elimu kubwa kiasi hiki.
Ahsante pia na wewe ndugu yangu@Pendaelli kwa kujifunza maarifa haya kwa undani zaidi ni kweli kitabu kimetumia lugha ngumu but nimeona nikieleze kwa lugha nyepesi ili tunaotafuta maaarifa tujifunze vyema na twende pamoja 2024 hakuna kumuacha mtu nyuma.
 
Ahsante sana mkuu
 
Back
Top Bottom