Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,064
- 22,757
Baada ya CCM kuitangazia dunia...
Kama chama tawala CCM kinakiri na kuitangazia dunia kwamba Tanzania hakuna mwenye uwezo, sifa wala busara, je tutegemee nini?
Sifa zote wanazozitaja kupelekea kuuzwa kwa bandari ndio sifa hizo hizo viongozi wao wengi ndani ya chama na ndani ya serikali wanazo.
Sasa shangaa walivyo mataahira. Baada ya kuitangazia dunia hivyo bado wana uhalali gani wa kuendelea kung'ang'ania madaraka?
Na Watanzania kwa ukondoo wao badala ya kuwawajibisha, wanawachekea tu na kupiga vigelegele huku wanaibiwa mchana kweupe.
Kwa nini kwa mfano tusiwatafute watu nje ya CCM wenye hizo sifa wanazokiri hawana watuongoze? Ya nini CCM kung'ang'ania madaraka?
Tumeanza na bandari na zipo tetesi kwamba yapo mengi yako jikoni yanapikwa na CCM, je tunarudi utumwani? Sasa tulidai uhuru wa nini?
Hivi kati ya Watanzania 60,000,000 wanaCCM ni wangapi? Sijui jamii za Kimataifa zinaiangaliaje hiyo CV mpya tuliyobebeshwa na CCM!
- Kwamba Watanzania hatuna mwenye uwezo wa kusimamia uendeshaji wa chombo kama Bandari kwa uadilifu!
- Kwamba Watanzania kwa ujumla wetu ni watu wasio na uaminifu katika utendaji wa kazi popote pale tulipo,
- Kwamba Watanzania kwa tabia sisi ni wadokozi, wala rushwa na wasiowajibika kwa matendo yetu.
- Kwamba Watazania kwa desturi zetu si binadamu walio na busara wala hekima katika kulinda kilicho chetu.
- Kwamba Watanzania hatuna ari ya kujiletea maendelo peke yetu bila kusimamiwa na wageni kutoka nje.
- Kwamba sisi Watanzania ni wavivu wa kufikiri tusio na ubunifu unaoendana na kasi ya mabadiliko duniani,
- Kwamba peke yetu, sisi Watanzania ni viumbe tofauti kabisa tuliojikuta labda hapa duniani kwa bahati mbaya tu.
- Kwamba pamoja na kujaaliwa neema lukuki ya mali asili sisi peke yetu hatuna fikra ya kujikwamua kutoka lindi la umasikini.