CCM ni kikundi cha watu wasiozidi 100

joseph2

Senior Member
May 31, 2015
126
251
Ndugu Watanzania mwezangu naomba niwasalimie kwanza, heshima zote nawapa. Baada ya salam, naomba nijitambulishe kwa ufupi tu mimi ni nani, mimi ni Mtanzania tu wa kawaida mwenye umuri wakati, sio kijana sana wala sio mzee sana. Ila kama ujana au uzee ungepimwa kwa kiwango cha mapenzi kwa nchi, basi mimi nigekuwa kwenye kiwango cha juu kwa kuipenda nchi yangu Tanzania.

Baada ya kusema hayo naomba ni andike kinachoniumiza moyoni kutakana na utawala wa nchi yetu ulipofika sasa. Kwanza bila kupepesa macho, Chama kinacho kilishafeli kutawala muda mlefu.

Sasa hivi kinajiita Chama tawala lakini ukweli ni kwamba Tanzania sasa hivi hakuna Chama tawala, isipokuwa kuna kikundi cha watu wasio zidi 100 ambao ndio Chama tawala chini ya mwavuri wa CCM na hao watu sitawataja kwa leo ila siku zijazo nitawaweka wazi. Kwa leo acha kwanza niongee kuhusu namna hao watu wanaojiita CCM wanavyotudharau sisi Watanzania wote, wakiwemo wanachama wa CCM.

Watu 100 ndani ya CCM wakishafanya deal zao za kiufisadi na kuuza rasirimali za nchi kwa wageni huwa wanaenda kujificha CCM na kusema kuwa walichokifanya ni maamuzi ya CCM. Na kwasababu wanachoma wengi wa CCM uelewa wao ni mdogo au hata wenye uelewa hawana mamlaka yoyote wala jukwa la kusemea, basi wanajikuta na wao wameingizwa kwenye kapu la kuitwa CCM.

Maelezo ni mengi sana kuhusu hili genge la watu mia wanaolazimisha watu wote kuwa wajinga ndani ya CCM. Ila kilichonifanya niandike huu waraka ni huu mkataba wakugawa bandari kwa DP World.

Ukweli tangu mkataba huo uvujishwe mimi sipati usingizi, na nafikiri kuna Watanzania wengi kama mimi ambao hawalali kwa sababu ya huu mkataba. Huu mkataba ni zaidi ya kugawa bandari, tunakwenda kurudisha biashara ya utumwa na warabu nia yao kubwa sio bandari bali ni vyazo vya maji Safi. Tunakoelekea maji yatakuwa mali kuliko mafuta, na wezetu wanaangalia miaka mia mbili mbele.

Wakati hilo kundi la watu 100 wanaojiita CCM wakiangalia tu kiasi cha pesa zinazohitajika kufanikisha ushindi wa uchaguzi ujao. Kwa maelezo hayo naomba Watanzania wote wenye nia njema na nchi hii na wote wenye akili ya kuona mbele miaka kumi tu ijayo tuungane tuukatae huu Mkataba kwa gharama yoyote ile.

Na njie pekee ya kuukataa mkataba huu ni mbili tu; moja ni kuhakisha CCM inatoka madarakani kwa shari au kwa amani na nyingine ni kuingia ndani ya CCM na kuwaondowa hao watu mia ndani ya CCM.

Ila hiyo ya kuwaondowa hao watu 100 ndani ya CCM ni ngumu zaidi, kwasababu hao watu wamejimilikisha Mali za Umma, hivyo wana hela nyingi kupita kiasi na hawaoni shida kuua yoyote anayeonekana kuwa kikwazo kwao.

Kwa leo niishie hapa, maana machozi yameanza kunitoka kwa uchungu wa nchi yangu kujitubukiza utumwani kiurahisi namna hii, kwa vihela tu utu wa WaTanzania unauzwa.
 
Watu 100 ndani ya CCM wakishafanya deal zao za kiufisadi na kuuza rasirimali za nchi kwa wageni huwa wanaenda kujificha CCM na kusema kuwa walichokifanya ni maamuzi ya CCM. Na kwasababu wanachoma wengi wa CCM uelewa wao ni mdogo au hata wenye uelewa hawana mamlaka yoyote wala jukwa la kusemea, basi wanajikuta na wao wameingizwa kwenye kapu la kuitwa CCM.
Samuel Sitta alisema wapo 10, sasa sijui wamezaliana kipindi gani maana haizidi miaka 10 tangu afariki
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom