=*=*=....BIG UP Faiza Foxy....=*=*=

=*=*=....BIG UP Faiza Foxy....=*=*=

Hongera FF.

Ila jamani, FF ni mgumu kiasi cha hata kushukuru? Manake simuoni ati, au sijapitia posts zote?

Oooh Dina, nashkuru sana jamani, sema nilikuwa bz kidogo, nimepata wageni wa ghafla (wanangu) hawaniwachi kila mmoja anataka kudeka kivyake, uzuri ni kwamba wana marafiki wanawaalika, basi kila wanapokuwa hawapo mie ndio napata nafasi ya kuingia JF.
 
ah ah ah ah ah ah ah ah ah ah ah ah !!! Eh eh eh eh eh eh eh eh eh !! Kwi kwi kwi kwi kwi kwi !! Mbavu zangu mie kumbe umeshiba uvinza kiasi hicho

Hongera sana sana FAIZA..

For the record jina ''FOXY'' ndio nalizimia kinoma humu ndani,lanipa raha tehe! tehe! tehe!

kwa leo naishia hapa siongezi neno
 
Faiza, nakupa hongera za dhati kabisa, nimejaribu sana kukupigia simu sijakupata, kwa bahati nzuri "Gozi" lako likanipigia alfajiri ya leo na kunieleza kuwa kakunyang'anya simu yako na kaizima. I wonder why.

Nikikupa pongezi peke yako itakuwa simtendei haki "shemeji" yangu, Gozi lako, nampa pongezi sana kwa kuidumisha ndoa hii kwa miaka hii yote. Najua kakustahamilia sana, au niseme mmestahamiliana? Nawapa pongezi za dhati.

Jamani wana JF, wakati FF ananiita mimi "Anko" huwa anakosea, mimi si "Anko" wake bali ni "cousin" wake kwa mama, yaani ni mtoto wa mama mkubwa na mdogo, ingawa nimemzidi kidogo tu kwa umri (tumecheza pamoja utotoni) lakini amezoea kuniita anko baada ya kuwa tu watu wazima na nephews wamekuwa wengi kiasi cha kusahaulika jina langu na kuwa ni ama "anko" au mjomba kwa wengi wanaonifahamu, inanshangaza kuwa hata "bi mdogo" (mke wangu wa pili) huniita anko.

Nimeongea hayo, kwa kutaka tu kuwafahamisha kuwa FF namjuwa, sana sana tena sana.

FF, kwa anaemjuwa, ni easy going, fun loving, with a big smile always. Anaependa sana ndugu zake na marafiki zake, yupo tayari kuwatetea awajuao hata kama wana makosa, she will never betray you! Ni mwanamke straight forward hatafuni maneno na siku zote husema, "nichukie kwa ukweli wangu, usinipende kwa uongo wangu".

Katika kukua kwetu jijini Dar. FaizaFoxy, mitaa ya kariakoo (ya late 60's na early 70's) ni maarufu sana kiasi anatisha kufatana nae. Umaarufu wake una kuja mara mbili, kwanza kazaliwa, kasoma na kukulia hapo Kariakoo, pili kaolewa na mtu maarufu sana pale Kariakoo na Dar au Tanzania kwa ujumla, kutokana na shughuli zake, ni mtoto wa Kariakoo tuliye kuwa nae pia.

Kwa miaka mingi tulipoteana na FF baada ya yeye kuolewa na kwenda kuishi nje ya Tanzania kwa muda mrefu sana, ukimuuliza mwenyewe kwanini mliamua kukaa nje miaka yote hiyo? mwenyewe hujibu "tulimkimbia" Nyerere na siasa zake za kukandamizana. Lakini najua ni stihizai zake tu, kama kuna mtu alikuwa akimpenda Nyerere tulivyokuwa tunakua basi sijamuona zaidi ya FF. Sijui kwa nini baada ya kurudi Tanzania akawa hapatani na Nyerere.

FF ni mkimya sana na huwa haongei mengi, mimi nashangaa hapa JF kawa ni mmoja wa "wapayukaji" na saa zingine huwa ananikera, lakini naweza kukisia ni kwa nini. Ntamuachia mwenyewe.

Nna mengi ya kuongelea kuhusu FF lakini itakuwa si vyema nikamsemea, pengine mwenyewe hatopenda kusemewa yake.

Hongera Faiza, Hongera G.

Psss. Hiyo nick ya Foxy, alipewa na kakaetu mkubwa (mungu amrehem), toka utotoni na imeshika mpaka leo, ingawa sana ilikuwa kwa kifamilia tu tunayoijua, nashangaa kukuta anaitumia humu JF, muulizeni mwenyewe ina maanisha nini.

Anko Zoooooomba!

You are the best! Usiseme mengi, please.

Thanks for the gift, its beautiful. Aunt Z alikuja kumuona wajina wake, duhh mapapai matamu sijapata kuona, ntawaleta wote hawa on Sunday. be there for them please. Will call you.

Pssss,. Hiyo kwenye red, unakumbuka siku uliyoiba gari ya Mzee ukatupeleka Afrikana halafu tukakwama kwenye matope? Duhh, siku za mwizi arubaini, kila nikiwahadithia kina Z wanacheeeka!
 
Zomba... What an insight on FF.... Thank you.... I feel i know her mo'

And sasa i understand our last VM disagreement imetoka wapi....

Pamoja Saaana.
ADI


ADI, Zomba na mie damdam, he is my cousin na tumekuwa pamoja, we call him Anko because everybody calls him so. He is my favorite person.

Hilo ndio "nunda" la Kariakoo orijino, anajidai akitoka namimi kila mtu ananijua K'Koo, huyo na Gozi ndio sikubali kabisa kupita nao Kariakoo, maana kila kona watataka wasimame waongee, wanywe kahawa halafu mara wanakwambia "wee tangulia tu", wananikera kama nini, halafu hapa kanchomekea mimi.
 
Nikisikiaga jina Foxy basi namkumbuka Pam Grier.

And thats exactly how I got my nick! amazing, you are from my times, Foxy Brown, Remember? and then Black Mama White Mama.
Pam-Grier.jpg


If you've seen her, you've seen me! Then.
 
wifi nilikuambia natamani lile jukwaa la FF aliloliota! yaani siku hizi ukiongelea 2nd anniversary watu wanakuona like ana alien! it is a sad one, nadhani analysis ya tatizo inabidi ianzie kwenye kuzaliwa hadi sasa. kakangu eiyer alisema asubuhi labda vile wamama wanaenda kwenye siasa na kazini so watoto wanakosa malezi ya mama hadi wanashindwa jinsi ya kuishi na wenza wao? (i am looking for causal-effect relationships,lol!)

Tutalipata lile jukwaa, tartib, vitu vizuri havitaki haraka.

Halafu hii ya kulea watoto ukashindwa kufanya kazi, to me it was the opposite, wanangu walipokuwa wanakuwa mie nikifanya kazi ya kuajiriwa full time. Walipoanza kujitegemea mie ndio nimechoka kazi! inashangaza.
 
Hongera sana FF kwa kufikisha miaka 30 ya ndoa lakini nitakuwa simtendei haki Mumewe FF kwa ustahimilivu mkubwa.Kuishi na Mamaa wa mipasho miaka 30 si mchezo hata kidogo.Mwanzoni nilidhani FF ana miaka kati ya 18 - 20s baada ya kusoma hii bandiko nimebaini nilikuwa simtendei haki FF kuanzia leo FF nitamwita Dada FF.Tunapishana na Dada FF kwenye baadhi ya mada lakini kuna baadhi ya mambo Dada FF ananikosha sana [1] Hakimbiii mada aliyoianzisha Nape anastahili kujifunza hili.[2] Ni mjuzi wa kutetea hoja hatukani ingawa mipasho si haba.[3] Anaipenda dini yake Islam ikiguswa anakuwa mkali kama pilipili kichaa.




Ahsante sana. No comment.
 
Kwa kweli ana stahili hongera FF, du ina maana FF anagonga kama 50 years hivi kama aliolewa na 20 years! sasa nikifikiria na ukada wake wa CCM, na misimamo yake kweli inaingia akilini, nilikuwa nashindwa kuelewa , kumbe umri umekwenda!

Time never stands still!
 
mkuu inawezekana JF ndiyo mahali pake pa kupigia story na kumwaga utumbo na hasira zote, akiwa mtaani, rafiki yake ni mumewe tu. inawezekana pia ni mke mzuri sana huyo FF-anaweza hata akakuogesha huyo.

Mwenye siri ni mumewe!

Nimecheeeeka, yaani wewe mke mzuri ni wakukuogesha tu? Hayo mbona ni kawaida, muhim ni nini unachoogeshewa si kuogeshwa!

Ahsante sana.
 

Nampongeza FF kwa miaka 30 ya ndoa. Mimi nimesherehekea ya kwangu ya miaka 33 Jan 1, 2011

Kama ametulia kiasi hicho asijidhalilishe kutetea SIASA UCHWARA (by Rostam). Nina imani hakuna chuo kikubwa kuliko ndoa. Ushirikiano na familia yake ni msingi tosha na ushahidi wa kuvumilia hoja mbadala hata za kisiasa.


Ahsante sana, naona mimi na wewe we are almost in the same boat ingawa mwenzangu umenizidi kwa miaka 3, nadhani una mengi zaidi ya kuwajuza vijana wa leo. Nakupongeza sana.
 
Back
Top Bottom