Bendera Ya Taifa

Mlenge

Mlenge

Verified Member
Joined
Oct 31, 2006
Messages
594
Points
500
Mlenge

Mlenge

Verified Member
Joined Oct 31, 2006
594 500
Nianze na swali: Hivi unaweza kupeperusha bendera ya taifa mahali uishipo hata ikiwa wewe si kiongozi mtaani?

Nakumbuka wimbo ufuatao tuliimba chekechea, ile iliyoko pale karibu na 'Holofea' kama tulivyozoea kupatamka:

Bendera ya Tanzania,
Ndio ya kujivunia,
Ilianza kupepea,
Mwaka sitini na moja.

Hapo tunashuhudia,
Tunavyojitegemea,
Hapa kwetu Tanzania,
Uhuru umechanua,
Mola wetu Rabuka,
Ijaze yako fanaka!

Mwezi wa kumi na mbili
Saa sita kamili.
Siku ya tarehe tisa
Yalikuwa mambosasa!

Kilele Kilimanjaro
Bendera yatwitwitika
Hapa kwetu Tanzania
Uhuru umechanua
Mola wetu Rabuka
Ijaze yako fanaka!


Ilikuwa ni furaha tele kuimba wimbo huu.

Hivi naweza kuweka pazia lenye rangi za bendera?
Soksi?
Penseli?
Dekio?
Nguo za ndani?
Kilemba?

Naweza kuweka bendera ya taifa kabisa ya ukweli sebuleni? Jikoni? Bafuni? Sitaonekana nadhalilisha bendera?

Watanzania wengi hatujihisi kuwa huru kuitumia bendera ya taifa tupendavyo. Ukiangalia bidhaa zenye bendera za nje, mfano, bendera ya Marekani, utazikuta ni aina nyingi hapa Tanzania kuliko bendera ya Tanzania. Ukikatiza mitaani utakuta 'masela' wanapeperusha bendera ya Marekani kwenye kijiwe chao. Usiombe ukutwe unapeperusha bendera ya taifa, ilhali huna madaraka yoyote ya kiserikali, ni dhana ambayo pengine ni potofu. Hivyo, bendera ya taifa ukiiona inapeperushwa, ujue hiyo ni ofisi ya serikali. Baadhi ya wananchi wanaweza kudhani bendera ya taifa ni kwa ajili ya serikali tu. Wananchi wanaruhusiwa siku mojamoja kujidai nayo, hasa Taifa Stars ikiwa inacheza.

Ili kupunguza sintofahamu, ni vema:

1. Serikali iwe na bendera yake (kama haina bado) tofauti na bendera ya taifa. Ofisi za serikali zipepee bendera ya serikali.
2. Bendera ya taifa isiwe inashushwa saa 12 jioni.
 

Forum statistics

Threads 1,307,088
Members 502,332
Posts 31,601,272
Top