Sheria ya kupandisha na kushusha bendera ya Taifa izingatiwe na iwe Amri kwa watu wote

Loading failed

JF-Expert Member
Sep 14, 2023
1,946
5,852
Kumekua na mazoea sana katika shule, vyuo, nyumba za ibada, taasisi , mashirika na ofisi za kiserikali na binafsi kwa wale wanaotumia bendera ya Taifa kupandisha na kushusha bendera ya Taifa kimazoea nje au ndani ya muda sahihi.

Pia kumekosekana uzalendo kwa wananchi kusimama wima pale wawapo au wapitapo maeneo yaliyopo karibu na bendera ya Taifa pindi inapo pandishwa au kushushwa jambo hili likiachwa litaondoa uzalendo ndani ya nchi yetu na kuonekana sisi ni wananchi wa ajabu.

Naiomba serikali yangu tukufu kupitia amiri jeshi wetu mkuu kwa kushirikisha vyombo vya ulinzi viwe vya serikali au sekta binafsi kusimamia kwa kina Amri, sheria na kanuni za kupandisha na kushusha bendera katika maeneo yote yanayotumia bendera ya Taifa. Pia mashuleni na vyuoni kuwekwe sheria kali , amri na kanuni za uwajibishwaji wa wanafunzi pale wanapo kiuka amri ya filimbi ya kumtaka asimame pindi bendera inapopandishwa au kushushwa .

Na katika barabara zetu zinazokatisha katika maendeo yote zilizopo bendera ya taifa kuwe na sign board za amri itakayo mtaka mtu au chombo cha moto kusimama pale zoezi la kupandisha na kushusha bendera linapofanyika huku wakishirikishwa vyombo vya ulinzi na usalama kukamata na kuwawajibisha watu wote watakao kiuka Kusimama .

Mwisho kabisa naiomba serikali ipige marufuku nguo au vitambaa vyovyote / mavazi yeyote yasiyo rasmi yanayotengenezwa kwa mfano wa bendera yetu ya Taifa na kuzagaa nchini .
 
Kwa serikali ipi mkuu watu watii?.
Tuanzie hapa kwanza twende taratibu...
 
Back
Top Bottom