Ushauri: Rangi za Bendera ya Taifa zifutwe katika sakafu za ndani ya Bunge

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,115
22,566
Salaam,Shalom.

Mimi ni Mtanzania mzalendo wa Nchi yangu nzuri Tanzania, naijua thamani ya Bendera ya Taifa LANGU.

Bendera yetu ya Taifa Ina RANGI kuu nne, Bluu, Njano, Kijani na Nyeusi. RANGI hizo za Bendera ya Taifa naziona katika sakafu za ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Sitaki kuhoji Uzalendo wa mtoa wazo la kupaka RANGI za Bendera ya Taifa katika sakafu za ndani ya Bunge la JMT, inawezekana, mtoa wazo Hilo alisukumwa na Uzalendo uliopitiliza.

Kwa maoni yangu kama Mtanzania, bendera au RANGI za Bendera Inatakiwa iwekwe juu, ukutani, au katika nguzo, Si katika sakafu.

Ninashauri yafanyike marekebisho, RANGI hizo ziondolewe chini, ikae red carpet pekee.

MUNGU ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Karibuni🙏
 
Bendera ya Tanzania ina rangi nne - kijani, njano, nyeusi, na bluu.

Rangi za kijani, njano, nyeusi, na blue sio bendera ya Tanzania. Bendera ni zaidi ya rangi. That's the context.
Wewe unakubaliana na designer wa kupanga RANGI za Bendera yetu katika sakafu ya bunge la JMT?
 
Wewe unakubaliana na designer wa kupanga RANGI za Bendera yetu katika sakafu ya bunge la JMT?
Hakuna sheria yoyote inayokataza kutumia rangi za bendera kwa mpangilio wowote utakaokupendeza.
 
Hakuna sheria yoyote inayokataza kutumia rangi za bendera kwa mpangilio wowote utakaokupendeza.
Unaweza kunitajia designer aliyetoa wazi la kupaka RANGI za Bendera ya Taifa letu katika sakafu ya bunge la JMT?
 
Bendera yaani flag ina definition yake rasmi inayotambulika. Sio kila chenye rangi ya bendera ni bendera.
Mtoa mada ana hoja. Na ni wazi anaumia anapoona Bendera ya Nchi yake haipewi Heshima hasa na Watunga Sheria.

Mfano kuna baadhi ya Shule utaona watoto wamevalia sweta zenye rangi ya Bendera yetu. Endapo Mgeni atakuuliza zile rangi kwenye sweta zinaakisi Bendera ya Nchi yako au ni urembo tu?? Wewe ungejibu nn??
 
Huy anayeon Kam ni rang tu bas azipak kweny nyumba yake kama anaon hazin maan zikiw Kam rangi tuone kama atamaliza wiki
Ni sawa na mtu achukue uamuzi wa kwenda kiwandani,aprint zuria lenye picha ya mama yake mzazi na Kisha kulitandika katika mlango wa kuingilia nyumbani kwake,

Tukimuuliza sababu za kufanya hivyo,atujubu, anampenda sana mamake,

Ataeleweka mbele ya JAMII?
 
Back
Top Bottom