Ben Saanane na wenzake wapata ajali mbaya

Ben Saanane na wenzake wapata ajali mbaya

This is real sad and touching to lose young brains of this country
But as the holy book states ''God giveth life and God taketh life away'.
 
KWELI NIMEAMINI SIASA HUAMBATANA NA UCHAWI NA USHIRIKINA WA HALI YA KUTUKUKA.:sick:
 
Mingoi ni men.to fresh kama mame.nto wengine hana jipya.

Naaam, Mingoi hajaweka jipya hilo aliloweka ni la zamani sana na malipo yake ndiyo unayasikia sasa hivi. Haya mama, wewe tupe jipya.

Kufa kufaana.
 
Last edited by a moderator:
Na Ben Saanane
Ardhi ni katili,Nimepoteza zawadi...Nimepoteza lulu ya thamani Allan Meshili na Faith. Ni muda mchache uliopita nilikua nanyi,tukicheka,Kutaniana na kupeana moyo katika ndoto zetu Allan Patrick Meshili ,Umetangulia.Umeniacha rafiki yako uliyeniahidi utakua nami hadi tone la Mwisho. Umeniachia msiba mkubwa Moyoni.Sijawahi kuwa na Rafiki wa Kweli kushinda kipimo chako Allan.Umetimiza Ahadi yako hadi Pumzi yako ya Mwisho Faith Makundi,Nilihama siti ya mbele nikahamia kiti cha nyuma ili nisome kitabu ulichoniletea kama zawadi "Banker to the Poor"-Profesa Muhammad Yunus .

Kumbe ilikua ni zaidi ya kubadilishana siti!
Uliniahidi kutumia likizo yako kuhakikisha kipindi hiki tunapanga na kutekeleza yote tuliyokubaliana hasa proposal yangu ya kutumia VICOBA phasewise na kuanza mchakato wa kutengeneza network kwa ajili ya kuanzisha Benki ya Maendeleo ya Watu wa Rombo.Ulinishawishi nichukue likizo pia kipindi hiki kama wewe na Allan kabla hujarudi Afrika Kusini ili tuweke akili,taaluma na uzoefu wetu pamoja tufanye kazi kwa ajili ya jamii .Tulienda Rombo kwa ajili ya kampeni lakini pia kupata practical experience ya hali ya Rombo. Sasa mmetangulia,bado huko mliko mnataka nichukue Likizo? kwa ajili ya nini sasa?

Sikuamini kama mwisho wetu ungekua hivi,mbele ya Scania ya Mafuta.Aliyetugonga na kukimbia,hajakimbia hukumu bado...!Ni picha za kutisha na kuhuzunisha!

Washirika wangu,watu muhimu katika safari yangu nimewapoteza kwa mkupuo mbele ya Macho yangu. Sitamkufuru Mwenyezi Mungu,Ana mipango yake.
Ni machozi ya uchungu,Sina wa Kumlilia zaidi yako wewe Mwenyezi Mungu uwalaze pema peponi Allan na Faith Familia zinahuzunika na kuwalilia.Ni msiba mkubwa kwetu sote.

Nahisi Moyo wangu unazimia kwa huzuni.Ni uchungu mkali Moyoni.

Asanteni Makamanda mlioahirisha safari zenu na kuungana nami hadi Muhimbili.Mlinitambua kwa Tshirt ya M4C mkaungana nasi hadi muda huu tunapotoka Muhimbili.Wapo marafiki zangu wa kwenye mitandao ‪#‎Gabriel‬ na Mkewe ‪#‎Joyce‬ Mungure.Asanteni sana Namshukuru Mungu kwa kuniponya katika ajali hii....!Ni wewe pekee Unayejua kwanini umeniponyakatika ajali hii ya tatu katika maisha yangu .Sitakuhoji.! Kwa leo sina mengi ya kusema.

Mungu awabariki wote mlioungana nasi Muhimbili na marafiki wote mlioko Mbali.

Jina la Bwana lihimidiwe !

jina la bwana nani
?lihimidiwe. je wale uliowawaisha nao jina la bwana lihimidiwe .sumu ya kumuua zitto nayo jina la bwana lihimidiwe?
 
Naaam, Mingoi hajaweka jipya hilo aliloweka ni la zamani sana na malipo yake ndiyo unayasikia sasa hivi. Haya mama, wewe tupe jipya.

Kufa kufaana.

Bring back our girls mom faiz
 
Last edited by a moderator:
Kifo hakijui siasa mama. Hili ni pigo kubwa kwa Ben Saanane kama binaadam na tunampa pole yeye kwa kuumia na kwa kufiwa na makamanda wenzake na uchungu alionao leo hii utamfanya afikiri wale aliotaka kuwaua kwa sumu wenza wao wa karibu wangekuwa katika hali ipi? laiti mipango yake ya kuuwa kwa sumu ingefanikiwa (kama haijafanikiwa)!

na wale alio legeza nati za gari zao wafe kwa ajari kule bagamoyo
 
Mkuu FF inanikumbusha kipindi kile baada.ya.jamaa kushindwa kumuwekea sumu prezidaa Zitto na Habib Mchange walipokuwa hotelini Moro kuelekea Iringa jamaa walilegeza stud za tairi la gari wakijaribu kummaliza kwa njia ya ajali.

kumbe tunajuwa wengi hii ishu tehteh ben hata dk. slaa anakuogopa kukaa na wewe pembeni ni zaid ya shetani

kwanza ulijuaje ukahama siti kutoka ile ya mbele kwenda ile ya nyuma
ukipona njoo na majibu
 
Pole sana kwa ajali Ben na kupoteza rafiki. Wapate pumziko la milele.
 
kumbe tunajuwa wengi hii ishu tehteh ben hata dk. slaa anakuogopa kukaa na wewe pembeni ni zaid ya shetani

kwanza ulijuaje ukahama siti kutoka ile ya mbele kwenda ile ya nyuma
ukipona njoo na majibu
Duh Kwa aina hii ya kuandika Ni dhihirisho la Uelewa wako kuwa mdogo.
 
Yaani kuna watu humu wanatamani wangekuwa Mungu wabadilishe maamuzi ya Mungu,kwamba wamesikitika sana kuona Ben alipona kwenye ile ajali.Mtabaki mnaumia Mungu hapangiwi juu ya utendaji wake wa kazi...!!!!!

CC. Faiza Foxy,Mingoi,Tony Gwanko
 
Back
Top Bottom