ilio na simanzi vimetawala katika viwanja vya Hospitali ya KCMC, mkoani Kilimanjaro wakati ndugu wakishuhudia majeneza 36 kati ya 42 yenye miili ya ndugu zao waliofariki dunia ajalini baada ya magari mawili kugongana na kuwaka moto Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro
Ndugu hao pamoja na waombolezaji wengine ambao wameanza kuwasili saa 3 asubuhi ya leo Alhamisi, Julai 3, 2025 katika viwanja hivyo wameshindwa kujizuia huku wakibubujikwa na machozi baada ya kuona majeneza yenye miili ya ndugu zao yakishushwa kwenye magari ya polisi
Hata hivyo, kutokana na wingi wa majeneza, miili hiyo imekuwa ikiletwa awamu kwa awamu katika viwanja hivyo kwa ajili ya taratibu ya kuaga na kisha kukabidhiwa kwa ndugu
Kila majeneza yalipokuwa wakishushwa katika magari na kwenda kuwekwa eneo maalumu lililoandaliwa, vilio kutoka kwa waombolezaji viliongezeka
Ajali hiyo ilitokea Juni 28, 2025 katika eneo la Sabasaba, Same mjini ikihusisha basi Kampuni ya Chanel One lililokuwa likitokea Moshi kwenda Tanga na basi dogo aina ya Coaster lililokuwa likitokea Same Mjini kwenda Moshi kugongana uso kwa uso
Soma,Pia: Idadi ya vifo katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Saba Saba vimefika 42
Baada ya kugongana, magari yote mawili yaliwaka moto, yakiwa na abiria ndani
Chanzo: Mwaanchi_official & Jambo TV