Ben Saanane na wenzake wapata ajali mbaya

TUTASHINDA TENA

Senior Member
Aug 12, 2014
141
77
Habari tulizopata muda huu ni kuwa Ben Saanane amepata ajali mbaya eneo la Maili moja Kibaha wakielekea Rombo Kilimanjaro kwa ajili ya kampeni pamoja na Marafiki zake wawili.

Gari inayomilikiwa na Allan Meshili aina ya Prado T377ACG iligongwa na gari nyingine na kupoteza mwelekeo kisha ikavaana uso kwa uso na gari ya aina ya scania ya mafuta.

Kuna watu wapo eneo la tukio watatutumia taarifa zaidi
===================

JamiiForums imethibitisha kutokea kwa ajali hii, Ben yupo salama lakini Patrick anadaiwa kuwa katika hali mbaya sana.

Taarifa zaidi zitafuatia


Na Ben Saanane
Ardhi ni katili,Nimepoteza zawadi...Nimepoteza lulu ya thamani Allan Meshili na Faith. Ni muda mchache uliopita nilikua nanyi,tukicheka,Kutaniana na kupeana moyo katika ndoto zetu Allan Patrick Meshili ,Umetangulia.Umeniacha rafiki yako uliyeniahidi utakua nami hadi tone la Mwisho. Umeniachia msiba mkubwa Moyoni.Sijawahi kuwa na Rafiki wa Kweli kushinda kipimo chako Allan.Umetimiza Ahadi yako hadi Pumzi yako ya Mwisho Faith Makundi,Nilihama siti ya mbele nikahamia kiti cha nyuma ili nisome kitabu ulichoniletea kama zawadi "Banker to the Poor"-Profesa Muhammad Yunus .

Kumbe ilikua ni zaidi ya kubadilishana siti!
Uliniahidi kutumia likizo yako kuhakikisha kipindi hiki tunapanga na kutekeleza yote tuliyokubaliana hasa proposal yangu ya kutumia VICOBA phasewise na kuanza mchakato wa kutengeneza network kwa ajili ya kuanzisha Benki ya Maendeleo ya Watu wa Rombo.Ulinishawishi nichukue likizo pia kipindi hiki kama wewe na Allan kabla hujarudi Afrika Kusini ili tuweke akili,taaluma na uzoefu wetu pamoja tufanye kazi kwa ajili ya jamii .Tulienda Rombo kwa ajili ya kampeni lakini pia kupata practical experience ya hali ya Rombo. Sasa mmetangulia,bado huko mliko mnataka nichukue Likizo? kwa ajili ya nini sasa?

Sikuamini kama mwisho wetu ungekua hivi,mbele ya Scania ya Mafuta.Aliyetugonga na kukimbia,hajakimbia hukumu bado...!Ni picha za kutisha na kuhuzunisha!

Washirika wangu,watu muhimu katika safari yangu nimewapoteza kwa mkupuo mbele ya Macho yangu. Sitamkufuru Mwenyezi Mungu,Ana mipango yake.
Ni machozi ya uchungu,Sina wa Kumlilia zaidi yako wewe Mwenyezi Mungu uwalaze pema peponi Allan na Faith Familia zinahuzunika na kuwalilia.Ni msiba mkubwa kwetu sote.

Nahisi Moyo wangu unazimia kwa huzuni.Ni uchungu mkali Moyoni.

Asanteni Makamanda mlioahirisha safari zenu na kuungana nami hadi Muhimbili.Mlinitambua kwa Tshirt ya M4C mkaungana nasi hadi muda huu tunapotoka Muhimbili.Wapo marafiki zangu wa kwenye mitandao ‪#‎Gabriel‬ na Mkewe ‪#‎Joyce‬ Mungure.Asanteni sana Namshukuru Mungu kwa kuniponya katika ajali hii....!Ni wewe pekee Unayejua kwanini umeniponyakatika ajali hii ya tatu katika maisha yangu .Sitakuhoji.! Kwa leo sina mengi ya kusema.

Mungu awabariki wote mlioungana nasi Muhimbili na marafiki wote mlioko Mbali.

Jina la Bwana lihimidiwe !
 
Hii picha aloweka huyu haihusiani na ajali ya Ben saanane, bali picha wameitoa kwenye hii habari


ajali.jpg

Watu 10 jana walipoteza maisha katika ajali ya gari ambayo ilitokea KM65, Benin. Ajali hiyo ambayo ilitokea baada ya Lori la mizigo lenye namba ya usajili LSR 649 XK kugongana na Toyota Hiace ya kampuni ya usafirishaji yenye namba ya usajili WWR 625 XA.
Ajali kati ya Toyota Hiace na lori

Miongoni wa watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo ni Jane na Oyemwen Igbinoba ambao walikuwa katika maandalizi ya harusi yao iliyokuwa ifanyike mwezi ujao na majeruhi walifikishwa katika hospitali ya Shilo.
Roho za marehemu wote zipumzike kwa amani!
 
Back
Top Bottom