Ben Saanane anavyoteseka na kivuli cha unafiki...

Ben Saanane anavyoteseka na kivuli cha unafiki...

lakini ninyi hapa mna mu attack ben kwa kusema tu kwamba amesema uongo? Hamjajibu hoja zake.mwenzenu yuko tayari kwenda kwenye vikao vya chama.ninyi mnakimbia kivuli chake na leo mmetumwa na zitto kuja huku kwa kasi kumtetea.ben has evidence,nilitegemea kama una busara kama makamu m/kiti bavicha.ungeenda kupeleka suala hili kwenye chama.swali,kwa nini ulikua kwenye kikundi hicho,na mission yenu ilikuwa nini?
unawaonea kusema wametumwa na zitto. Wewe umetumwa na nani?.
 
Juliana Shonza napenda utuambie watanzania kuwa 1. kwa nini ulishiriki kwenye kikundi hichi? 2.Je mlikua mna matarajio gani ndani ya kikundi hichi? 3. kwa nini haukuwa tayari kuanika haya kabla ya nyie kupishana na Saa nane??

kinachonifurahisha ni kwamba Zitto na kikundi chake hawajibu hoja
 
Last edited by a moderator:
Hasira yako ya mimi kukushtukia na kuwaambia kina Mwampamba na Juliana kuwa wewe kila siku una warekodi na kwenda kuuza habari kwa kiongozi mmoja wa juu ambaye humtumia HAWARA WAKE kutuma SMS za matusi kwa watu, isiwe sababu ya kuanza kuwachafua watu ndugu yangu.


kama ben anasema amerudi kundini baada yakuwa muasi basi anatumia uwongo ule ule aliokuwa anautumia wakujirekodi yeye mwenyewe mipango na mikakati yake na kisha kuwapelekea wahusika kwamba ni mipango ya masalia kuvuruga chama.that is nonsense

Wewe bint ndiyo umeharibu kila kitu na kudhihirisha kuwa Mchange ni muongo. Mchange anatuambia kuwa yeye ndiye aligundua na kuja kuwaambieni kuwa Ben Saanane huwa anawa record, wewe unatuambia kuwa Ben alikuwa ana jirecord mwenyewe.
Je unamaanisha kuwa Mchange anataka kujipa sifa juu ya jambo ambalo si la kweli?
 
Habari, nimeona mchango wangu huu niuanzishie uzi ili tujadiliane kwa mapana..

Mpaka tuufikie tunaouita ukombozi wa pili, basi tuna kazi na safari ndefu sana!

Kama vijana tunaweza tukainuka na kuanza kuporomosha mashtaka na kutaja majina ya watu bila hata facts, basi kazi ipo ndugu zangu.

Ufahamu wangu ni kuwa ili tufanikiwe kuwaondoa CCM madarakani lazima tufanye kazi hiyo kama timu moja, mawazo yangu ni kuwa hatutaweza kufikia hatua yoyote ikiwa tutakuwa na vijana wa namna hii.

Vijana wa aina ya Ben Saanane wanaoweza kukaa, kutengeneza mgogoro, kubuni njia za kuuendesha mgogoro, kutafuta suluhu na hatimaye kwenda kuuza huo mgogoro kwa viongozi wengine huku akiamini kuwa anakinusuru chama hakika anakosea sana.

Vijana wa aina ya Saanane ambao kazi yao nikutumia muda na akili zao nyingi kuwarubuni na kuwagombanisha vijana wa chama na viongozi wa chama ni hatari pengine kuliko ukoma.

Kwa kuwa mara kadhaa amekuwa akinitaja kwenye mijadala yake yote. Bila hata kuangalia namna ninavyohusika, na kwa kuwa na leo hii ameamua kunitaja na kunihusisha moja kwa moja, na kwa kuwa viongozi, vijana na wanachama wengi wa chadema wamekuwa wakinihusisha mimi kuwa karibu sana na zitto kabwe. leo nitasema kitu kwenye hili.

1. Naomba niweke wazi hapa leo, kuwa sikuwahi kumfahamu mtu anayeitwa Ben Saa nane kabla mwezi wa nne 2011.
sijawahi kumsikia jina wala kumuona sura yake.(hawezi kubisha kwenye hili)

2. Ben ndiye alikuwa wa kwanza kunipigia simu, kati kati ya kipindi cha kampeni za uchaguzi wa BAVICHA - 2011 mimi nikiwa nagombea uenyekiti na yeye akiwa ni mgombea wa kimkakati(alitumwa na baadhi ya viongozi kuja kuuvuruga uchaguzi-uthibitisho upo) ambapo aliponipigia simu na kunieleza kuwa tuna haja ya kukaa kama wagombea na kuangalia namna tunaweza shiriki salama kwenye huo uchaguzi kwa madai kuwa amepata tetesi makao makuu wanamgombea wao na wanajiandaa kukata majina ya watu, jina lake na langu yakikiwemo. Nilimsikiliza na kumpuuza.

3. Baada ya hapo sijawahi kuwasiliana nae tena ben saa nane, mpaka usiku wa siku jina langu limekatwa na kamati kuu ya chama, tena aliwasiliana na mimi kupitia grayson nyakarungu, aliyekuwa swahiba wake…cha kusikitisha ni kuwa mwana mkakati ben aliwashauri mwampamba, nyakarungu na kisandu kuungana, akanishirikisha na mimi. Huku nikijua dhamira yake kuwa ni unafiki. Nikamsikiliza kwa kuwa sikuwa tena na cha kupoteza (nimeshaenguliwa tayari).

Masikini ya mungu BEN akawahadaa vijana wa watu (Mwampamba na Nyakarungu) wakaenguliwa huku yeye akiwa ni wa kwanza kukiri kuwa wameamua kuongeza nguvu.

4. Unafiki wa Saanane uliendelea siku ya tatu baada ya kuisha kwa uchaguzi wa BAVICHA maana baada ya kukatwa jina langu, wanafiki wengi walifikiri ningetoa tamko la kukipinga chama ama kuhama chama, sikufanya hivyo, kwangu mimi uchaguzi ule haukuwa ligi, ilikuwa ni mechi tu ya kirafiki. Hapo mwenyekiti wa chadema wilaya ya Kibaha akaomba kukutana namimi, nikakubali, nikakutana nae ubungo plaza, tukiwa hapo tulikuwa na mwampamba na nyakarungu, aliposimuliwa saa nane kuwa tunaenda kukutana ubungo Plaza, akaandika humu jamii forums kwa kutumia ID fake yake kuwa tumekutana na mimi nina mpango wa kuhama chama.

Nlimwambia Mwampamba kuwa saa nane ana kazi maalum, mwampamba hakunielewa, akanipinga sana sana sana, naamini leo atanielewa vizuri sasa.

5. Kwa kipindi chote hicho saa nane alikuwa anaitisha vikao vya kila aina, saa nane anatukana na kutoa kejeli za kila aina kwa viongozi wa kuu hasa katibu mkuu na mwenyekiti (lengo ni kutaka kluthibitisha kuwa kuna vijana wanawapinga viongozi hawa). Ninataja maeneo machache ambayo saa nane alipenda kuitishia vikao vyake, KWA JOHN FEDHA-KINONDONI, BLUE PEARL HOTEL-UBUNGO PLAZA na LUCH TIME HOTEL-UBUNGO EXTERNAL….naomba nikiri hadharani hapa, si mimi, mwampamba wala Juliana anayemsema aliyewahi kwenda kukutana na saa nane akajinunulia kinywaji wala chakula…kwa saa nane huwa tukifika tunakula, tunakunywa mpaka tunapochoka saa nane yeye hulipia-tukambatiza jina tukamwita manji. (lakini siku zote nimekuwa nikiwaambia wenzangu kuwa kaeni chonjo na huyu jamaa ana kazi maalum---leo wamejionea)

6. kati kati mwaka jana 2011 mwenyekiti wetu wa taifa freeman mbowe alikamatwa kwa kilichodaiwa kutokutii amri ya mahakama hapa napo saa nane akafanya vitu vyake, kama kawaida yake, akawakusanya vijana wake wote ambao yupo nao kwa kazi maalum akaanza kuwajaza ujinga…naomba nikiri tena hapa kuwa usipokuwa makini ni rahisi sana kuingia kwenye kumi na nane za huyu jamaa. Ni lalzima uwe makini kama mchange kumshinda na ndio maana ananichukia sana sana.

Mimi nimefundishwa kuwafahamu wanafiki. Hasa ninapokuwa naongea nao uso kwa macho saa nane kwangu alikuwa mnafiki kwa hiyo sikumpa nafasi hata chembe.

7. katika kipindi chote hiko sijawahi kumsikia mwana mkakati saa nane akiwasema vizuri viongozi wa chadema. Mtu pekee aliyekuwa anamsifia alikuwa ni zitto.

SAA NANE NA ZITTO
Nimeshtushwa sana na maandishi aliyoyaandika Saanane leo, hii inatokana na ama kuchanganyikiwa au kujihami kutokana na kushushuliwa na kuonekana mwongo. Naomba nieleze vizuri hapa.

1. Ben Saanane ndiye alikuwa muitishaji mkuu wa vikao vya hotelini(makutano) akiwa na saa yake ya kurekodi aliyonunuliwa na kiongozi mmoja wa chama kwa kinachoitwa kazi ya ushushu. Yeye ndiy aliyekuwa mwenyekiti wa vikao na mwandishi wa kila kinachosemwa.

2. Ni BEN SAANANE ndiye aliyewashawishi na kuwalazimisha wenzie anaowasema leo ni wasaliti waunde kikundi. Hakuishia hapo, akakitunga mpaka na jina. Kuwa ni ‘’patriotic movement seven’’ na akakifupisha PM7. Akashawishi kikundi hicho kizunguke nchi nzima kuhamasisha viongozi wa huko kufanya mageuzi ndani ya chama. Saa nane unafiki utakupeleka pabaya.

3. Ni BEN SAANANE ndiye aliyegawa majina ya kuitana miongoni mwa wana kikundi hiko, yeye akajipa jina la COBRA, mimi akanipa MDUDE (kwa kuwa nilikuwa naijua dhamira yake niliendelea kumkeli)

4. Ni BEN SAANANE ndiye aliyeshauri namna ya kuhakikisha kikundi hicho kinapata pesa, wakati mimi nilimpinga ku anzia kuanzisha hiko kikundi mpaka namna ya kukusanya kwake pesa..wakati yeye alikuwa anasisitiza kwenye njia ya kukusanya michango, tena tuwachangishe viongozi wa chama na watu wengine maarufu.

5. Akiwa mkweli atakumbuka na kukiri kuwa nilimwambia kuanzisha kikundi hicho ni sawa na kuanzisha chama ndani ya chama, aliumizwa na misimamo yangu sana.

6. Ni BEN SAANANE ndiy aliyekuwa anasisitiza tuombe kukutana na zitto kabwe ili tumuombe ufadhili wa kufadhili kikundi chetu kilichoasisiwa na SAANANE na akanipa jukumu la kuhakikisha ninamwambia na kumshawishi zitto tukutane nae tufanye nae kikao, sababu yake kubwa ni kwamba Zitto ni rafiki yangu sana na itakuwa rahisi kumpata. Hapa tulirumbana sana, mimi nilielewa dhamira yake na nikiri leo hadharani kuwa nilimshauri zitto asikubali kukutana na kikundi hiki, na niukamwambia kabisa kuwa lengo la kikundi hiki ni kuthibitisha makundi ndani ya chama.-leo yametimia.

7. Ni SAANANE aliyewaapia kujito a kwenye kikundi alichokianzisha mwenyewe kwa sababu ya kutokumpata zitto kwenye kikao, siku ambayo saa nane alipendekeza zitto tukutane naye zitto alikwenda marekani kuzindua tawi la chadema, ni saa nane ndiye aliyenilaumu sana kuwa kwa nini sikumuarifu kuwa zitto hatokuwepo, nilimjibu sio wajibu wangu kuwaambia watu kuwa zitto yupo ama hayupo.

8. Ni Saanane huyu huyu mnafiki tuliyerumbana naye hasa mimi nay eye juu ya namna ya kumshirikisha zitto kwenye michango ya kikundi chake cha PM7. Naomba ninukuu mabishano yetu..mimi ‘’ kama swala ni kukusanya pesa, kwanini tumfuate Zitto kwanza na sio mtu mwengine yeyote’’?...saa nane..’’kwa sababu zitto ni kijana na ana mitazamo chanya kwa vijana wenzie na pia tunafanana nayo mitazamo hiyo sio kamakina mnyika wao status quo’’…mimi..’’kama Zitto tumemwomba tuonane naye na amesafiri bila kutujibu hauoni kuwa anatuudharau, kwanini tujipeleke kwa zitto tunayemnung’unikia kila leo?’’..saa nane.. ’’ hapana ni lazima atusaidie, zitto kwa vyovyote lazima agombee uenyekiti, na hatuwezi fanya hii kazi tukamfungulia milango bila nay eye kutoka jasho lake, ni lazima atupe pesa’’….mimi sasa kwanini tunakataa wenzetu kutumiwa halafu na sisi tunajitumikisha wenyewe kwa zitto?’’…saa nane..’’Mchange, hakuna jinsi tunaweza acha mshirikisha zitto, mwisho wa siku zitto atakuwa beneficiary kwenye huu mpango’’… …………………ukifuatilia kwa makini mazungumzo yetu ambayo kwa bahati nzuri nimeyarekodi kuanzia siku ya kwanza mpaka ya mwisho utaweza kumuelewa SAANANE kuwa alikuwa na kazi maalum.

Niseme hapa kuwa wote kwa pamoja, saa nane na zitto kila mmoja ameniambia kwa mdomo wake kuwa hawajawahi kuonana uso kwa macho, zitto yeye anasema kuwa anaweza akakutana leo na saa nane barabarani na akapishana nae bila kumfahamu.

Wote kwa pamoja wameniambia kuwa mawasiliano yao huwa ni kwa simu hasa SMS na mara chache kwa emails.

Na moja kati ya malalamiko aliyokuwa ananipa saa nane nimpe zitto ni kuwa..
1.kwa nini hapokei simu za wapiganaji wake akiwemo yeye?...
2..kwanini anakuwa na mpiganaji kama saa nane na hataki kuonna nae….
3…kwanini hataki kukifadhili kikundi cha PM7.?

Kwa mtiririko wa matukio ulivyo, na kwa jinsi SAA NANE alivyoandika mashtaka yake dhidi ya zitto huku akizani anamchafua, hakika amejidharirisha sana.

Mtu mmoja mpinzani mkubwa sana wa zitto amenitumia sms kwenye facebook, ananiambia JF vipi maana COMPUTER YANGU HAIFUNGUI..huyu nae ni mjinga sababu anashabikia ujinga.

Kumshambulia zitto kwa mashtaka ya uwongo namna hii kuna mfanya zitto awe na nafasi ya kuonekana anasingiziwa mamba mengi sana hasa ndani ya chama.

Kwa mimi ninayemfahamu Saanane nje na ndani, na ninayefahamiana na kufanya kazi na Zitto, kwa mashtaka haya ya uwongo, basi hakika nitazidi kumuamini Zitto.

Nitazidi kuamini kuwa Zitto amesingiziwa mambo mengi sana ndani na nje ya chama, ninazidi kumuamini na kumtia moyo kwamba hizi ni hatua za mwisho za watu wanaokupinga, wakishindwa kukupinga kwa facts, watakupinga kwa uwongo…saa nane amekubali kutumika vibaya kwa kisingizio cha kuwa anakilinda chama na viongozi wake.

Napata mashaka kama anakielewa anachokisema, huwezi kumtenganisha zitto na uongozi wa chama. Zitto ni naibu katibu mkuu wa chama, hivyo sio rahisi kumchafua zitto ukaacha kukichafua chama.

Nimemwona saa nane anajitetea kutishiwa kuuawa, saa nane, ZITTO akiwa na mimi amenusurika kuuawa kwa ajali ya gari hivi karibuni tukitokea morogoro kwenda iringa(siku ya kumbukumbu ya kifo cha mwalimu nyerere) baada ya wapinzani wake ndani ya chama kwenda kufungua nati za tairi la nyuma ili afe, kweli zitto ameaga kwao, kweli zitto hataweza kufa kwa mipango ya mungu, hatukufika mbali tuliushtukia mchezo tukarudi morogoro mjini na zitto akaendelea na retreat yao mpaka kesho yake tukarudi dar wala hakuitangaza hii sababu aliwadharau na mbinu dhaifu.

Sio rahisi kuitoa roho ya mwanadamu mwenzio, sio rahisi kumuua zitto kama mlivyojaribu mara kadhaa na timu yenu ..

Nasikitika sana kama vijana sasa tunaeza kusimama kidete na kuandika uwongo na kuutetea bila hata woga kama ndugu yangu Saanane.

Hasira yako ya mimi kukushtukia na kuwaambia kina Mwampamba na Juliana kuwa wewe kila siku una warekodi na kwenda kuuza habari kwa kiongozi mmoja wa juu ambaye humtumia HAWARA WAKE kutuma SMS za matusi kwa watu, isiwe sababu ya kuanza kuwachafua watu ndugu yangu.

Mchafue Zitto kama unahisi una sababu ya kufanya hivyo kwa mambo ambayo una ushahidi nayo.

SAANANE acha tabia ya KUBUNI MGOGORO, KUUANZISHA, KUUENDELEZA, NA KISHA KUUTUMIA KAMA CHANZO CHAKO CHA KUPATA PESA.

SAA NANE, Waislam wanasema sifa za mnafiki tatu (ayatul munafiq tharasa).
1. akiongea huongea uwongo..
2..akiaminiwa hajiaminishi/hudhiaki..na ..
3..akiahidi hatimizi..

mwisho wa siku wasaliti wote mtashindwa Mchange ulichoandika hapo ni upuuzi na uthibitisho kwamba wewe na kundi lako ni wasaliti lakini chadema ni mpango wa Mungu.
 
Taswira,
Wewe umejulia wapi kwamba Dr. Slaa anamwogopa Mchange? Au ndiyo yale yale ya kuchafua uongozi wa chama?

achana nae huyu naona nae amekuja kutoa backup ya kutosha
 
kujiunga na pm 7 unapewa how much sina hela ya sikukuu nahitaji kujiunga@Ben saanane
 
HAdithi za kutunga ndo mtaji wa CCM kuisambaratisha Chadema. Kulingana na WAsira kuwa CDM itasambaratika soon sasa ndo naona ndo kipindi chake. Walishaweka mitego yao muda mrefu na kwa kuwa Mtu kama ZITO amekuwa naye haeleweki [ kutangaza kugombea urais wakati wenzako wako kwenye kampeni ngumu Arumeru]ndo mwanya wa kumumaliza kabisa. Hiki kikundi mbona kirahisi sana kukiua.

Ondoa hawa wote bakiza Zito kwa uchunguzi na asishirikishwe katika kazi muhimu za chama kwa muda then kwisha habari. Kafulila alipoondoka jamaa akatengeneza movie ya wachezaji wapya.

Huyu Saanane na mamuya fukuzia mbali huku nje kuna vijana wanataka kupiga kazi ya chama sio hao masalia.
 
umeenda off-key kabisa kabisa...mimi si wa aina hiyo, weka mbele facts ntakuelewa, hasira zako subiri mijadala mnayokutana na watu wa aina yako na sio mimi.
HOJA HAPA NI KWANINI SAA NANE ALIKUBALI KUTUMIWA KUMCHAFUA ZITTO?. AMETUMIWA KWA MASLAHI YA NANI NA KWANINI?

acha unafiki we masalia wa MP7.
 
Mchange kuna kitu umesahau............................ ulituhumiwa kupenyeza rushwa kwa M-PESA na tiGO kwa wapiga kura mikoani na wilayani na hii ni uwongo?
Wewe umekiri unamfahamu Zitto, wakati Exaud Mamuya alikiri kuwa walikuwa wote na Zitto ndo alikuwa coordinator wa mgogoro wa madiwani wa Arusha.
Nashawishika kusema kwa matatizo ya Madiwani wa Mwanza kuna mkono wa mtu Zitto)
 
Last edited by a moderator:
Swali la msingi....je Zitto amedanganya JF kuwa hamjui Ben?? Maelezo yanaelekea kuonyesha kumchafua ZZK zaidi na si Chama.
 
Inaonekana viongozi wa CHADEMA wamemtuma Ben,jana walikesha kwenye ile thread kuangalia upepo unakwendaje hapa simuoni hata mmoja........

Hilo liko wazi kabisa ,kumbe hata chadema wana mitandao kama ya CCM ya akina Membe,Lowasa ,Sitta.
Hata kama hao kina Machage walikua wapambe wa Zitto ,ukweli na uhalisia wa mambo ni kuwa hata hao wengine akina Slaa ,Mbowe lazima wana wapambe.

Alichofanya Ben ni ku Infiltrate and distablise kambi ya Zitto ambao yeye mwenyewe ndo alijaribu kuiasisi.
Huyo Ben atakua ama anafanya kazi ya Mbowe au Slaa.

Ndo maana watu husema siasa mchezo mchafu.HAKUNA CHA USALITI WALA NINI.
 
shimo la panya limemwagiwa maji ya moto.
ngoja tione hili game la madogo litaishia wapi.
 
Mnafiki Mkubwa wewe
Hii migogoro imeanza baada ya uchaguzi wa 2010 hivyo unaposema kuna baadhi ya viongozi wakuu ambao kwao ili chama kiende lazima kuwe na migogoro ni upotoshaji ambao hautofautiani na namna mnavyorusha miguu hapa kujitetea.

Nyie ni wanafiki wakubwa sana, post zenu zote kuanzia kwa kigagula wenu mnajifanya kusimamia kwenye misingi ya umoja na kuiondoa ccm madarakani. mtaumbuka mwaka huu
YAWEZEKANA U MGENI KWENYE SIASA ZA CHADEMA, MIGOGORO YA CHADEMA HAIKUANZA BAADA YA UCHAGUZI KAMA UNAVYODAI...LABA NIKUKUMBUSHA KIDOGO...
1. Walianza na kaborou, wakamshambuliaaaaaa mpaka akahama chama.
2. wakahamia kwa akwilombe, naye wakamshambuliaaaa mpaka akahama chama
3. wakaja kwa kina Mzirai, Mng'ong'o na wenzao wakawashambulia mpaka wakawafukuzza uanachama..
4. lakini kubwa zaidi ni CHACHA WANGWE, walimshambulia, wakamwita msaliti, amenunuliwa, amehongwa mpaka akauawa kitatanishi tatanishi, cha kushangaza ni kwamba baada tu ya kuuawa kwake wakaacha kumuita msaliti, akaanza kuitwa KAMANDA...
5. Wamehamia leo kwa zitto, wanamshambulia ili ahame chama, kinachowauma sasa in zitto kuwapuuza, ndio maana wanalazimika kubuni kila aina ya njia za kumshusha lakini wanashindwa....

kitu cha msingi na kuzingatia ni kwamba kwenye chadema woooooote wanaweza kuitwa wasaliti isipokuwa wawili tu.
 
njooni wote mseme yoote tuwajue zaidi na mtueleze sababu ya sisi kuendelea kuwaamini kwenye harakati za chama. 1. Baada ya haya mnayoyafanya hapa JF itabidi mtueleze kwa nini hamkua tayari kuyazungumzia haya ndani ya vikao vya chama.

2. Baada ya haya mnayoyafanya hapa JF itabidi mtueleze kwa nini mliingia kwenye movement haramu ndani ya chama na mkaa kimya mpaka mmepishana ndo mnaanza kufichua harakati hii. 3. Baada ya haya mnayoyafanya hapa JF itabidi mtueleze kuwa intention ya hichi kikundi chenu ndani ya chama ilikua ni nini kabla ya nyie kupishana kwenye maslahi yenu. 4.Baada ya haya mnayoyafanya hapa JF itabidi mtueleza kuwa kwa nini tuendelee kuwaamini ndani ya chama chetu makini. CC to ben Saanane Mchange Zitto Kabwe Exaudi Mamuya........

Kama mabishano haya ni taswira ya yaliyoko chumbani mwa CHADEMA basi ukombozi wa nchi hii ni ndoto. Ninachokipata kwenye malumbano haya yoote ni vita vya kupigania madaraka ambavyo kwa dimension zote vinaashiria mambo mabaya kwa mustakabali wa ukombozi wa nchi yetu.

Nyerere alipokuwa na wenzake kutaka kumwondoa mkoloni na kupata uhuru vita ilikuwa moja tu ambayo ni kumtoa mkoloni na kupata uhuru.

Nasema wanaharakati wa uhuru akiwemo Nyerere na wale wazee wa Magomeni na Kariakoo, Tabora na kwingineko wange kuwa na na hii tabia inayoonyeshwa na akina Saanane, Zitto na kikundi chao tungekuwa hadi leo hatuna uhuru.

Naomba hawa jamaa wa CDM wasome historia ya ukombozi wa nchi yoyote ; ni kwamba ukombozi hauletwi na watu wasiokuwa na lengo moja, hamwezi kuwa mmegawanyika katika malengo mkawa na ndoto ya kuleta ukombozi.

Kinachoendelea CHADEMA kinaaonyesha kuwa harakati za kuleta ukombozi kwa ajili ya mtanzania ili awe na maisha mazuri zinaelekea kugonga mwamba na sisi tulioko nje tukitazama tunachelea kuendelea kutoa support nakuamua kuendelea na hali iliyoko.

Najiuliza kama Vita ya madaraka ni kubwa namna hiyo kabla hamjashika nchi je vita dhidi ya kukwapua rasilimali za nchi itakuwa kubwa kiasi gani mtakapoingia kushika hatamu.

CHADEMA mnatupoteza Imani kabisa kwa sababu kwa mtu mwenye lengo jema na hii nchi hawezi kuasisi mapinduzi ya mwanaharakati mwenzake kwa sababu lengo ni kumtoa common enemy ambaye ni ukandamizwaji na si nani aongoze na nani asiongoze.

Mimi ningesema aongoze yule anayekubalika na wananchi. Si kila atakayesimama kwenye Kampeni za urais atakubalika kwa wananchi kama Dr. Slaa.

Awe Saanane au Zitto au nani wanaweza kusimama ila uungwaji mkono utakuwa kiduchu sana na watakuwa wameshusha popularity ya CHAMA na hatimaye kukitumbukiza shimoni kama ilivyo NCCR Mageuzi na TLP
.
 
kwa mala ya kwanza nitaweka nilichokiona ktk post zote kuanzia ya mamuya,Saanane na hadi hii ya mchange' ni kwamba kwa kawaida yai likipasuka kiini chake hapo 2natalajia kupata kifaranga'but hilo yai likipasuka kuanzia nje ya cover litakuwa limeharibi na hatutarajii chochote' .

Hawa vjana wote wana2mika, last wk saanane alim2humu julliana jana kaja na zitto nasema binafsi nguvu hizi mngezielekeza vijijini hakika mngepata wafuasi huko kwa hadhari 2 ni kuwa cjawahi kumsikia huyo zitto aki2kana viongozi wenzake kama ambavyo ckuwahi kumsikia Chacha Wangwe aki2kana viongozi.

Kilicho mtesa Wangwe ndicho kinachomtesa Zitto kupigania usawa na haki na pesa kugawanywa hadi kwenye matawi kuendeleza uhai wa chama.

Na katika hili hata sitashangaa mzee Arfi alipo2pa kadi ya chama chini na wakijitoa wote hawa 2naotaka hakutakuwa na chama.
 
Back
Top Bottom