Ben Saanane anavyoteseka na kivuli cha unafiki...

Ben Saanane anavyoteseka na kivuli cha unafiki...

na haikisaidii chama chao wala haiwasaidii wao wenyewe.
tatizo ambalo linanifanya nisipende kuongelea sana siasa ni kuwa kwanza huku ndani kuna watu wanakuwa na bias hata kwenye masuala ya msingi!penye ukweli ukisemwa watu hutoa mapovu,lkn huko chadema nadhani kuna matatizo makubwa,japo mashabiki hawataki kuyaongelea kabisaaa!!!
 
ila huu nao ni upepo,utapita tu tena bora umevuma mapema,thank God wanadamu tumepewa uwezo wa kusahau
 
tatizo ambalo linanifanya nisipende kuongelea sana siasa ni kuwa kwanza huku ndani kuna watu wanakuwa na bias hata kwenye masuala ya msingi!penye ukweli ukisemwa watu hutoa mapovu,lkn huko chadema nadhani kuna matatizo makubwa,japo mashabiki hawataki kuyaongelea kabisaaa!!!
ila kwa hali ya upepo inavyokwenda, nina hakika kila kitu kitakuwa wazi sasa hivi. naona wameanza kutupiana za uso
 
Mchange, kwanza uandishi wako umekosa mtirriko mzuri wa mawazo hata kama kuna ukweli wowote kati ya unayoyazungumza itakuwa ngumu sana ujumbe wako kueleweka. Pili, naona unataka kujisafisha lakini hausafishiki. Ona hapa ulichoandika:

"2. Ni BEN SAA NANE ndiye aliyewashawishi na kuwalazimisha wenzie anaowasema leo ni wasaliti waunde kikundi. Hakuishia hapo, akakitunga mpaka na jina. Kuwa ni ‘’patriotic movement seven’’ na akakifupisha PM7.
3. Ni BEN SAA NANE ndiye aliyegawa majina ya kuitana miongoni mwa wana kikundi hiko, yeye akajipa jina la COBRA, mimi akanipa MDUDE "

Unajua nini Mchange, watu wote wenye akili hawawezi kukuamini kwa haya unayoyaandika. You are being too pretentious, unatungatunga tu vijistori vya kubumba na watu wengi waliojiunga humu JF ni watu wazima wenye akili zao, wanaweza kupembua pumba na mchele. Zako hizi ni pumba.

mbona mimi nimemuelewa vizuri sana mkuu, kama anasema kuwa SAA NANE amewaingiza KING WENZIE sasa anataka kuwaacha kwenye mataa.
tuvute subira tusikie mengi zaidi
 
Dah, Zito kweli analo. Yaani hawa ndio watetezi wake? TUNTEMEKE a.k.a Gwakisa Burton, Mchange, ukisoma maandishi ya hawa jamaa unaona mapungufu mengi sana. Huitaji kuwa msomi mkubwa sana wa siasa za bongo kugundua Zito amefanya kosa kubwa sana kimkakati kama kweli anahusika nao.
 
Last edited by a moderator:
Vijana wa Kitz badala ya kupanga mikakati madhubuti ya kuiondoa CCM madarakani, wanapanga mikakati ya kumaliza wao kwa wao..hakika hatuwezi kufika kwa mtindo huu..!
 
naona kama unataka kututoa kwenye mjadala vile?..samahani lakini, hao uliowataja sioni kama wana husiana na masala yaliyoandikwa hapa saana ukiondoa bwana mchange ambaye ni mtoa mada. ukianza habari za hivyo unakuwa tayari umechagua upande na hautaweza kujadili kwa haki...hebu tuendelee kujadili huu mtanange wa kambi mbili zinazokinzana
 
Nimesoma hizi post tangu Juzi usiku ile ya Exaud Mamuya na jana ya Ben Saanane na leo hii nimesoma hii yako. Nilikuwa sijachangia lolote.

Baada ya kusoma pia na mjibu ya Zitto ya juzi usiku kwa Mamuya, nahisi kuna uvundo mkubwa kati yako na Zitto et al!

Sipendi migogoro na sipendi kushabikia Migogoro, lakini majibu yako yanafanana kwa kiasi kikubwa sana na alichokiandika Zitto kwa Mamuya Juzi. It seems you have something in Common with him.

Hujajibu hoja zozote za Ben Saanane so far, Ulichokifanya ni ku-revenge. Hebu jibu kile alichokieleza kwenye post yake ili tujue nani mkweli na nani muongo. Kumshambulia badala ya kujibu hoja zake kama alivyofanya Zitto juzi kushambulia badala ya kujibu MNAKOSEA!

Anyway nawatakieni mema kwenye chama chenu maana mie sio mwanachama wa chama chochote duniani. Lakini kiukweli, Zitto, wewe, akina Chagulani, Juliana Shonza na wengineo mlioko 'Masalia' mnayoibadili jina na kuiita PM7 leo mnatukatisha tamaa sisi vijana tunaohitaji mabadiliko.

Mzikubali kuongozwa na uchu wa madaraka kiasi hicho, msikubali kuongozwa na utumwa wa akili kiasi hicho na kumwabudu Zitto kama Mungu, msikubali kuingiza ushetani na kwenda kwa waganga katika mambo ya msingi kama haya. Unapokubaliana na Zitto kuwa ameaga kwao nazidi kuthibitisha kile alichosema Saanane kuwa mnaabudu ushirikina sana. Kijana anapokuwa mshirikina, mzee kama Kingunge afanye nini??? Shame on You!

Nimeongea kwa hasira kidogo sababu umeniudhi kushindwa kujibu hoja na badala yake unashambulia kama njia yako ya kujibu mapigo. Vijana huwa tunashindana kwa hoja ambapo hoja lazima ijibiwe kwa hoja na sio vinginevyo.

Nimeona post za Shonza Facebook akimtaka Zitto akae kimya na kuonyesha kuwa yeye ni kiongozi. Sawa, wewe inaonekana umetumwa na Zitto kujibu kwa niaba yake maana muda wote wa mchana ulikuwa wapi kujibu au tangu juzi alipotuma thread Mamuya na badala yake umeibuka saa saba hii usiku???

Ngoja niishie hapa kwanza naenda kulala nitarejea asubuhi kuona kama utakuwa umejibu hoja alizozisema Mamuya na Saanane dhidi yako wewe na Masalia wenzako plus bosi wenu Zitto.

Asalam Aleykum
 
Last edited by a moderator:
njooni wote mseme yoote tuwajue zaidi na mtueleze sababu ya sisi kuendelea kuwaamini kwenye harakati za chama. 1. Baada ya haya mnayoyafanya hapa JF itabidi mtueleze kwa nini hamkua tayari kuyazungumzia haya ndani ya vikao vya chama. 2. Baada ya haya mnayoyafanya hapa JF itabidi mtueleze kwa nini mliingia kwenye movement haramu ndani ya chama na mkaa kimya mpaka mmepishana ndo mnaanza kufichua harakati hii. 3. Baada ya haya mnayoyafanya hapa JF itabidi mtueleze kuwa intention ya hichi kikundi chenu ndani ya chama ilikua ni nini kabla ya nyie kupishana kwenye maslahi yenu. 4.Baada ya haya mnayoyafanya hapa JF itabidi mtueleza kuwa kwa nini tuendelee kuwaamini ndani ya chama chetu makini. CC to [MENTION=94608]ben Saanane Mchange Zitto Kabwe Exaudi Mamuya.
 
Last edited by a moderator:
Asante sana kamanda Mchange kwakuleta huu ufafanuzi, maana haya uliyoyaandika ndiyo nilkiyotaka kuyatolea ufafanuzi japo bado nitatoa ufafanuzi wangu kuhusu hizi shutuma ambazo kwangu mimi nachokiona ni sawa na mtu kuchimba shimo halafu akatumbukia yeye mwenyewe.

Suala la Ben kutumiwa kimkakati katika harakati zakumchafua zitto na sisi ambao wao hutuita masalia wala halijaanza leo, huu ni mkakati unaoratibiwa dhidi ya Zitto pamoja na vijana ambao wanamuunga mkono Zitto, nazidi kusisitiza kwamba Ben Saanane anatumia uongo kuuaminisha umma kwamba anamfahamu Zitto kitu ambacho hata nafsi yake nina hakika inamsuta.

Ben acha kukimbia kivuli chako, sio rahisi kumchafua Zitto kama unavyoweza kudhani, japo mnajitahidi sana lakini hamtofanikiwa.

Palipo ukweli, uwongo hujitenga .
 
Vijana wa Kitz badala ya kupanga mikakati madhubuti ya kuiondoa CCM madarakani, wanapanga mikakati ya kumaliza wao kwa wao..hakika hatuwezi kufika kwa mtindo huu..!

kweli ndugu yangu. tena kama kijana unakubali kwenda kuwarekodi vijana wenzako kisa ujira wa mwiha, itatutengenezea taifa bovu sana..labda saa nane awe anasingiziwa na leo
 
Huyu sijui saa nane ama tisa ni wakufukuzwa tuu kwenye chama mnafiki na mchumia tumbo kwanza hana ubavu wa kusmama mbele za makamanda heche mnyika lema sugu hana hata ubavu wa kuongea mbele ya mdee na ukimuona mtu anataka huruma ya watu ujue ndio mwongo y asipeleke tuhuma zake kwenye kikao kikajadiliwa hawa ndio vijana feki wenye akili za samaki si moja alimpakazia arfi kama amekula rushwa yuko wapi ashapigwa na chini hawa ni mamluki kwenye mwamvuli wa bavicha nakwambieni nyinyi kina saa tisa na kundi lenu hamutaweza kuitereresha mbio za ukombozi na hamutaweza kui dhoofisha chadema abadan na laana ya mungu iwe juu yenu
 
Dah, Zito kweli analo. Yaani hawa ndio watetezi wake? TUNTEMEKE a.k.a Gwakisa Burton, Mchange, ukisoma maandishi ya hawa jamaa unaona mapungufu mengi sana. Huitaji kuwa msomi mkubwa sana wa siasa za bongo kugundua Zito amefanya kosa kubwa sana kimkakati kama kweli anahusika nao.
Naona umekubali sasa kwamba Ben sanane na Mamuya wameishia kutumika na kuua chama.
Hao unao wataja hapo juu epuka ban,majina ya watu na fake acount
 
njooni wote mseme yoote tuwajue zaidi na mtueleze sababu ya sisi kuendelea kuwaamini kwenye harakati za chama.

1. Baada ya haya mnayoyafanya hapa JF itabidi mtueleze kwa nini hamkua tayari kuyazungumzia haya ndani ya vikao vya chama.

2. Baada ya haya mnayoyafanya hapa JF itabidi mtueleze kwa nini mliingia kwenye movement haramu ndani ya chama na mkaa kimya mpaka mmepishana ndo mnaanza kufichua harakati hii.

3. Baada ya haya mnayoyafanya hapa JF itabidi mtueleze kuwa intention ya hichi kikundi chenu ndani ya chama ilikua ni nini kabla ya nyie kupishana kwenye maslahi yenu.

4.Baada ya haya mnayoyafanya hapa JF itabidi mtueleza kuwa kwa nini tuendelee kuwaamini ndani ya chama chetu makini.

CC to ben Saa nane Mchange @Zito Kabwe Exaudi Mamuya.

kama alivyosema mchange ndivyo, basi naona saa nane anatakiwa atoe ufafanuzi zaidi kuhusu hii mipango yao. vinginevyo watakiingiza chama kwenye migogoron isiyokwisha na kutufanya sisi tusio wanachama kuendelea kudharau bupinzani. kuna haja ya vijana wetu kuanza kufundwa kisiasa
 
Huyu sijui saa nane ama tisa ni wakufukuzwa tuu kwenye chama mnafiki na mchumia tumbo kwanza hana ubavu wa kusmama mbele za makamanda heche mnyika lema sugu hana hata ubavu wa kuongea mbele ya mdee na ukimuona mtu anataka huruma ya watu ujue ndio mwongo y asipeleke tuhuma zake kwenye kikao kikajadiliwa hawa ndio vijana feki wenye akili za samaki si moja alimpakazia arfi kama amekula rushwa yuko wapi ashapigwa na chini hawa ni mamluki kwenye mwamvuli wa bavicha nakwambieni nyinyi kina saa tisa na kundi lenu hamutaweza kuitereresha mbio za ukombozi na hamutaweza kui dhoofisha chadema abadan na laana ya mungu iwe juu yenu

Ben saanane,Kazi yake rasmi ni kusafirisha umbea na kutunga hadithi za akadabladabla juu ya viongozi wa chama
 
Bw. Mchange, nina kaswali kamoja tu kadogo.
Kama ulishambaini Saa Nane kuwa mtu wa hatari, mbona uliendelea kuwasiliana naye? Mimi watu kama hao huwa nawapotezea mara moja, lakini inaonekana umeendelea kuwa na mawasiliano ya karibu na mtu huyu ambaye tangu mwanzo hukumwamini.
 
Naona umekubali sasa kwamba Ben sanane na Mamuya wameishia kutumika na kuua chama.
Hao unao wataja hapo juu epuka ban,majina ya watu na fake acount

mbona unasema as if unahukumu tayari mkuu, lazima hivi vyote vipatiwe uthibitisho. mchange yeye ametusaidia party B ya story, tusubiri mwendelezo wake.
 
Back
Top Bottom