Ben Saanane anavyoteseka na kivuli cha unafiki...

Ben Saanane anavyoteseka na kivuli cha unafiki...

Kwa hiyo wewe ulitaka juliana akae kimya?kwani hajatajwa hapa.Julina hana watu wa kumwambia kinachoendelea hapa jf?
Ben saanane aseme ni wapi alikutana na ZItto kama mAMUYA ALIVYOSEMA kuwa walikutana ARusha.
Ujue ben saanane ni mwongo kiasi gani.
unamtia aibu sana aliyekutuma,
kama wewe mwenyewe ndo muhusika unajitia aibu kupita kiasi,
umekua mzito kujenga hoja kutetea hichi mlichokusudia kukitetea.
Hii mitandao ya kijamii inawatia aibu sana. acheni huu upuuzi.
Maslahi binafsi hayawezi kufanikiwa mbele ya wanaharakati wengi wenye nia dhabiti.
 
kama ben anasema amerudi kundini baada yakuwa muasi basi anatumia uwongo ule ule aliokuwa anautumia wakujirekodi yeye mwenyewe mipango na mikakati yake na kisha kuwapelekea wahusika kwamba ni mipango ya masalia kuvuruga chama.that is nonsense
Tunataka Full package ya mkanda mzima na sio nusu nusu.Wewe Ben saanane unamjua kiundani.Tunataka umvue hapa jamvini nguo zake zote aumbuke.

Na kama unapicha na na meseji zake zote tunaziomba hapa.
 
kama ben anasema amerudi kundini baada yakuwa muasi basi anatumia uwongo ule ule aliokuwa anautumia wakujirekodi yeye mwenyewe mipango na mikakati yake na kisha kuwapelekea wahusika kwamba ni mipango ya masalia kuvuruga chama.that is nonsense
Wewe mdada wewe ndio mwepesi kabisa!!nirifikiri maneno yako yangekuwa na density kumbe pumba tupu.
 
Mkuu kunasehemu umeona Zitto amehusika na kuonana au kuzungumza au kufanya chochote na kikundi hicho au hao vijana? Zitto hahusiki na huu upuuzi,Sema uimara wake kisiasa Ben saanane akaona ni muhimi aushushe kwa aina hii aliyoihagua.

We bana acha kunichanganyia mambo. Nimefatilia stori zote mbili na mazingira yote yanayozunguka hizi stori na kwa upambanuzi wangu naweza kujua jema na ovu, sahihi na lisilo sahihi. Inasikitisha sana kuona kwa nafasi yake na ushawishi wake katika siasa za Tanzania jina lake linatumika kama kigawanyishi ndani ya chama. Na lugha yake ya mwili wala haonyeshi jitihada kurekebisha hali hiyo.
 

unamtia aibu sana aliyekutuma,
kama wewe mwenyewe ndo muhusika unajitia aibu kupita kiasi,
umekua mzito kujenga hoja kutetea hichi mlichokusudia kukitetea.
Hii mitandao ya kijamii inawatia aibu sana. acheni huu upuuzi.
Maslahi binafsi hayawezi kufanikiwa mbele ya wanaharakati wengi wenye nia dhabiti.

Kama ni upuuzi kaa pembeni.Sijatumwa nipo hapa kuanika hujuma ndani ya chama.Pilipili hii yangu inakuwashia nini wewe
 
What the f$##@#!!
Da toka nimeishi nawe ndani ya JF kwa mara ya kwanza UMETU- -na yani naimaigine umekunja shati kisha ukogonga meza whats this moda f$##@#!!.

Ndio hivyo MMK vijana wanazidi kukologa chumvi si chumvi, sukari si sukari!!!Nimemwabia dogo mwenzangu ukisikia Mwanakijiji anasema Poor Boy !!!Jua Kwishney sasa nakuja huku nakuta leo umeniongezea terminology nyingine inaitwa f$.............. hao ndio vijana wako wasio taka kusikia ya wazee,sasa imekuwa utumbo juu ya utumbo!!!
 
mbona mm sioni kama ben anaumbuka,,,mpaka sasa zitto 1 ben 3.tusubiri juliana kesho asubuhi nae aje kutoa ushuhuda wake labda utaongeza credit kwa zzk

Juliana,Mwampamba na Kitila mkumbo wote watato ufafanuzi hapa nawaomba sana watoe.Ben saanane hela ya x mass hii utakula ukiwa umeumbuka
 
''Nimemwona saa nane anajitetea kutishiwa kuuawa, saa nane, ZITTO akiwa na mimi amenusurika kuuawa kwa ajali ya gari hivi karibuni tukitokea morogoro kwenda iringa(siku ya kumbukumbu ya kifo cha mwalimu nyerere) baada ya wapinzani wake ndani ya chama kwenda kufungua nati za tairi la nyuma ili afe, kweli zitto ameaga kwao, kweli zitto hataweza kufa kwa mipango ya mungu, hatukufika mbali tuliushtukia mchezo tukarudi morogoro mjini na zitto akaendelea na retreat yao mpaka kesho yake tukarudi dar wala hakuitangaza hii sababu aliwadharau na mbinu dhaifu''.

''Sio rahisi kuitoa roho ya mwanadamu mwenzio, sio rahisi kumuua zitto kama mlivyojaribu mara kadhaa na timu yenu'' ..

''Nasikitika sana kama vijana sasa tunaeza kusimama kidete na kuandika uwongo na kuutetea bila hata woga kama ndugu yangu Saanane''.

''Hasira yako ya mimi kukushtukia na kuwaambia kina Mwampamba na Juliana kuwa wewe kila siku una warekodi na kwenda kuuza habari kwa kiongozi mmoja wa juu ambaye humtumia HAWARA WAKE kutuma SMS za matusi kwa watu, isiwe sababu ya kuanza kuwachafua watu ndugu yangu''.


maandiko haya mchange ni makali sana aisee, unaweza kudadafua kidogo?.
 
We bana acha kunichanganyia mambo. Nimefatilia stori zote mbili na mazingira yote yanayozunguka hizi stori na kwa upambanuzi wangu naweza kujua jema na ovu, sahihi na lisilo sahihi. Inasikitisha sana kuona kwa nafasi yake na ushawishi wake katika siasa za Tanzania jina lake linatumika kama kigawanyishi ndani ya chama. Na lugha yake ya mwili wala haonyeshi jitihada kurekebisha hali hiyo.

Kunasehemu umekuta anahusika?
yeye hanahaki ya kufahamiana na vijana kama wewe?au ww ukifahamiana na zitto utakuwa mtu wa zitto?

Wamejishushia heshima sana..mwampamba,Julina shonza na kitila mkumbo to follow.Nadhani utakaa na kujua kwanini zitto anasakamwa sana chadema.
 
''Nimemwona saa nane anajitetea kutishiwa kuuawa, saa nane, ZITTO akiwa na mimi amenusurika kuuawa kwa ajali ya gari hivi karibuni tukitokea morogoro kwenda iringa(siku ya kumbukumbu ya kifo cha mwalimu nyerere) baada ya wapinzani wake ndani ya chama kwenda kufungua nati za tairi la nyuma ili afe, kweli zitto ameaga kwao, kweli zitto hataweza kufa kwa mipango ya mungu, hatukufika mbali tuliushtukia mchezo tukarudi morogoro mjini na zitto akaendelea na retreat yao mpaka kesho yake tukarudi dar wala hakuitangaza hii sababu aliwadharau na mbinu dhaifu''.

''Sio rahisi kuitoa roho ya mwanadamu mwenzio, sio rahisi kumuua zitto kama mlivyojaribu mara kadhaa na timu yenu'' ..

''Nasikitika sana kama vijana sasa tunaeza kusimama kidete na kuandika uwongo na kuutetea bila hata woga kama ndugu yangu Saanane''.

''Hasira yako ya mimi kukushtukia na kuwaambia kina Mwampamba na Juliana kuwa wewe kila siku una warekodi na kwenda kuuza habari kwa kiongozi mmoja wa juu ambaye humtumia HAWARA WAKE kutuma SMS za matusi kwa watu, isiwe sababu ya kuanza kuwachafua watu ndugu yangu''.


maandiko haya mchange ni makali sana aisee, unaweza kudadafua kidogo?.

Mhhh,Wamefika mwisho tena kwaaibu walianza kwa kelel sasa naona kadri muda unavyokwenda tutasikia makubwa,hadi wake za watu watatajwa hapa
 
Mchange na Juliana Shonza,

Mnaweza kutuambia hapa Wafadhili wenu wakubwa wa hilo kundi lenu walikuwa nani?

Kama hamkufikiria hilo wakati mnaandika na waliowafadhili ni CCM au TISS basi anzeni kuandaa mazishi yenu maana nyie watu hadi ninawahurumia. Kama hao waliowapa fedha wataona nyie ni watu hatari na wakataka kuwaondoa mashahidi, nina wasiwasi INTELIJENSIA ya nchi yetu itawafananisha sasa hivi na majambazi na mgongwe na kitu kizito chenye ncha kali sana kitakachorushwa sijui na nani?

Mnavyozidi kujivua nguo wenyewe kwa wenyewe, nina imani kuwa watu sasa hivi wataogopa kuumbuka na ili kulinda heshima zao, watawapotezea mbali.
Hadi sasa ninaweza kuwaamini zaidi Zitto na Saanane kwa aina fulani na zaidi Lyamuya maana ndiyo waliokuwa wa kwanza kuja hapa kusema yao ya moyoni. Nyie mmesubiri hadi mtajwe na ndiyo mnakuja hapa na kuanza kumshambulia Saanane.

Pia unaonekana unapenda sana vya bure. Kama Saanane alikuwa anawakaribisha hotelini kwenye vikao na anakulipieni kila kitu, hivi hamkufahamu kuwa "there is no free lunch in the world?" Ina maana hata ukiwa na Zitto ni yeye hununua kila kitu na wewe kubaki unakodoa macho wakati akilipa. Sasa kwa kuangalia Jeuri ya Pesa, Zitto lazima awe nazo nyingi kuzidi Saanane na zaidi hata ukiona tu nyumba yake ya Tabata. Kwa uwezo wa juu wa Zitto, ni offer ngapi ameshawapa/amekupa hadi leo hii? Huoni kuwa sisi tunapata picha kuwa umeona uwe na Zitto kwa Nguvu kubwa ya hela yake anayomzidi Ben?

Anyway, kama ukiweza kutuwekea majina 5 wakubwa ya waliokuwa wakichangia huo umoja wenu, nitakuamini kwa asilimia kubwa na utajenga imani kuwa uyasemayo ni kweli.
 
Last edited by a moderator:
Wewe mdada wewe ndio mwepesi kabisa!!nirifikiri maneno yako yangekuwa na density kumbe pumba tupu.

pumba anazo yule ambaye anakimbia kivuli chake,anayetaka kuuaminisha umma kwamba hatumiwi wakati huo huo maelezo yake yanajifunga,soma vizuri maelezo ya mchange utaelewa maana kamaliza kila kitu.bado sijafunguka nitakapo amua kufunguka nitafunguka kivingine,ila kwa leo dozi ya mchange inatosha
 

unamtia aibu sana aliyekutuma,
kama wewe mwenyewe ndo muhusika unajitia aibu kupita kiasi,
umekua mzito kujenga hoja kutetea hichi mlichokusudia kukitetea.
Hii mitandao ya kijamii inawatia aibu sana. acheni huu upuuzi.
Maslahi binafsi hayawezi kufanikiwa mbele ya wanaharakati wengi wenye nia dhabiti.

cha kuzingatia tusitoke kwenye mjadala jamani...kama kuna watu wana gomvi zao binafsi basi tafadhali tuachieni sisi wengine tuendelee kushuhudia hii muvie tuuone mwisho wake.
 
Habari, nimeona mchango wangu huu niuanzishie uzi ili tujadiliane kwa mapana..

Mpaka tuufikie tunaouita ukombozi wa pili, basi tuna kazi na safari ndefu sana!

Kama vijana tunaweza tukainuka na kuanza kuporomosha mashtaka na kutaja majina ya watu bila hata facts, basi kazi ipo ndugu zangu.

Ufahamu wangu ni kuwa ili tufanikiwe kuwaondoa CCM madarakani lazima tufanye kazi hiyo kama timu moja, mawazo yangu ni kuwa hatutaweza kufikia hatua yoyote ikiwa tutakuwa na vijana wa namna hii.

Vijana wa aina ya Ben Saanane wanaoweza kukaa, kutengeneza mgogoro, kubuni njia za kuuendesha mgogoro, kutafuta suluhu na hatimaye kwenda kuuza huo mgogoro kwa viongozi wengine huku akiamini kuwa anakinusuru chama hakika anakosea sana.

Vijana wa aina ya Saanane ambao kazi yao nikutumia muda na akili zao nyingi kuwarubuni na kuwagombanisha vijana wa chama na viongozi wa chama ni hatari pengine kuliko ukoma.

Kwa kuwa mara kadhaa amekuwa akinitaja kwenye mijadala yake yote. Bila hata kuangalia namna ninavyohusika, na kwa kuwa na leo hii ameamua kunitaja na kunihusisha moja kwa moja, na kwa kuwa viongozi, vijana na wanachama wengi wa chadema wamekuwa wakinihusisha mimi kuwa karibu sana na zitto kabwe. leo nitasema kitu kwenye hili.

1. Naomba niweke wazi hapa leo, kuwa sikuwahi kumfahamu mtu anayeitwa Ben Saa nane kabla mwezi wa nne 2011.
sijawahi kumsikia jina wala kumuona sura yake.(hawezi kubisha kwenye hili)

2. Ben ndiye alikuwa wa kwanza kunipigia simu, kati kati ya kipindi cha kampeni za uchaguzi wa BAVICHA - 2011 mimi nikiwa nagombea uenyekiti na yeye akiwa ni mgombea wa kimkakati(alitumwa na baadhi ya viongozi kuja kuuvuruga uchaguzi-uthibitisho upo) ambapo aliponipigia simu na kunieleza kuwa tuna haja ya kukaa kama wagombea na kuangalia namna tunaweza shiriki salama kwenye huo uchaguzi kwa madai kuwa amepata tetesi makao makuu wanamgombea wao na wanajiandaa kukata majina ya watu, jina lake na langu yakikiwemo. Nilimsikiliza na kumpuuza.

3. Baada ya hapo sijawahi kuwasiliana nae tena ben saa nane, mpaka usiku wa siku jina langu limekatwa na kamati kuu ya chama, tena aliwasiliana na mimi kupitia grayson nyakarungu, aliyekuwa swahiba wake…cha kusikitisha ni kuwa mwana mkakati ben aliwashauri mwampamba, nyakarungu na kisandu kuungana, akanishirikisha na mimi. Huku nikijua dhamira yake kuwa ni unafiki. Nikamsikiliza kwa kuwa sikuwa tena na cha kupoteza (nimeshaenguliwa tayari).

Masikini ya mungu BEN akawahadaa vijana wa watu (Mwampamba na Nyakarungu) wakaenguliwa huku yeye akiwa ni wa kwanza kukiri kuwa wameamua kuongeza nguvu.

4. Unafiki wa Saanane uliendelea siku ya tatu baada ya kuisha kwa uchaguzi wa BAVICHA maana baada ya kukatwa jina langu, wanafiki wengi walifikiri ningetoa tamko la kukipinga chama ama kuhama chama, sikufanya hivyo, kwangu mimi uchaguzi ule haukuwa ligi, ilikuwa ni mechi tu ya kirafiki. Hapo mwenyekiti wa chadema wilaya ya Kibaha akaomba kukutana namimi, nikakubali, nikakutana nae ubungo plaza, tukiwa hapo tulikuwa na mwampamba na nyakarungu, aliposimuliwa saa nane kuwa tunaenda kukutana ubungo Plaza, akaandika humu jamii forums kwa kutumia ID fake yake kuwa tumekutana na mimi nina mpango wa kuhama chama.

Nlimwambia Mwampamba kuwa saa nane ana kazi maalum, mwampamba hakunielewa, akanipinga sana sana sana, naamini leo atanielewa vizuri sasa.

5. Kwa kipindi chote hicho saa nane alikuwa anaitisha vikao vya kila aina, saa nane anatukana na kutoa kejeli za kila aina kwa viongozi wa kuu hasa katibu mkuu na mwenyekiti (lengo ni kutaka kluthibitisha kuwa kuna vijana wanawapinga viongozi hawa). Ninataja maeneo machache ambayo saa nane alipenda kuitishia vikao vyake, KWA JOHN FEDHA-KINONDONI, BLUE PEARL HOTEL-UBUNGO PLAZA na LUCH TIME HOTEL-UBUNGO EXTERNAL….naomba nikiri hadharani hapa, si mimi, mwampamba wala Juliana anayemsema aliyewahi kwenda kukutana na saa nane akajinunulia kinywaji wala chakula…kwa saa nane huwa tukifika tunakula, tunakunywa mpaka tunapochoka saa nane yeye hulipia-tukambatiza jina tukamwita manji. (lakini siku zote nimekuwa nikiwaambia wenzangu kuwa kaeni chonjo na huyu jamaa ana kazi maalum---leo wamejionea)

6. kati kati mwaka jana 2011 mwenyekiti wetu wa taifa freeman mbowe alikamatwa kwa kilichodaiwa kutokutii amri ya mahakama hapa napo saa nane akafanya vitu vyake, kama kawaida yake, akawakusanya vijana wake wote ambao yupo nao kwa kazi maalum akaanza kuwajaza ujinga…naomba nikiri tena hapa kuwa usipokuwa makini ni rahisi sana kuingia kwenye kumi na nane za huyu jamaa. Ni lalzima uwe makini kama mchange kumshinda na ndio maana ananichukia sana sana.

Mimi nimefundishwa kuwafahamu wanafiki. Hasa ninapokuwa naongea nao uso kwa macho saa nane kwangu alikuwa mnafiki kwa hiyo sikumpa nafasi hata chembe.

7. katika kipindi chote hiko sijawahi kumsikia mwana mkakati saa nane akiwasema vizuri viongozi wa chadema. Mtu pekee aliyekuwa anamsifia alikuwa ni zitto.

SAA NANE NA ZITTO
Nimeshtushwa sana na maandishi aliyoyaandika Saanane leo, hii inatokana na ama kuchanganyikiwa au kujihami kutokana na kushushuliwa na kuonekana mwongo. Naomba nieleze vizuri hapa.

1. Ben Saanane ndiye alikuwa muitishaji mkuu wa vikao vya hotelini(makutano) akiwa na saa yake ya kurekodi aliyonunuliwa na kiongozi mmoja wa chama kwa kinachoitwa kazi ya ushushu. Yeye ndiy aliyekuwa mwenyekiti wa vikao na mwandishi wa kila kinachosemwa.

2. Ni BEN SAANANE ndiye aliyewashawishi na kuwalazimisha wenzie anaowasema leo ni wasaliti waunde kikundi. Hakuishia hapo, akakitunga mpaka na jina. Kuwa ni ‘’patriotic movement seven’’ na akakifupisha PM7. Akashawishi kikundi hicho kizunguke nchi nzima kuhamasisha viongozi wa huko kufanya mageuzi ndani ya chama. Saa nane unafiki utakupeleka pabaya.

3. Ni BEN SAANANE ndiye aliyegawa majina ya kuitana miongoni mwa wana kikundi hiko, yeye akajipa jina la COBRA, mimi akanipa MDUDE (kwa kuwa nilikuwa naijua dhamira yake niliendelea kumkeli)

4. Ni BEN SAANANE ndiye aliyeshauri namna ya kuhakikisha kikundi hicho kinapata pesa, wakati mimi nilimpinga ku anzia kuanzisha hiko kikundi mpaka namna ya kukusanya kwake pesa..wakati yeye alikuwa anasisitiza kwenye njia ya kukusanya michango, tena tuwachangishe viongozi wa chama na watu wengine maarufu.

5. Akiwa mkweli atakumbuka na kukiri kuwa nilimwambia kuanzisha kikundi hicho ni sawa na kuanzisha chama ndani ya chama, aliumizwa na misimamo yangu sana.

6. Ni BEN SAANANE ndiy aliyekuwa anasisitiza tuombe kukutana na zitto kabwe ili tumuombe ufadhili wa kufadhili kikundi chetu kilichoasisiwa na SAANANE na akanipa jukumu la kuhakikisha ninamwambia na kumshawishi zitto tukutane nae tufanye nae kikao, sababu yake kubwa ni kwamba Zitto ni rafiki yangu sana na itakuwa rahisi kumpata. Hapa tulirumbana sana, mimi nilielewa dhamira yake na nikiri leo hadharani kuwa nilimshauri zitto asikubali kukutana na kikundi hiki, na niukamwambia kabisa kuwa lengo la kikundi hiki ni kuthibitisha makundi ndani ya chama.-leo yametimia.

7. Ni SAANANE aliyewaapia kujito a kwenye kikundi alichokianzisha mwenyewe kwa sababu ya kutokumpata zitto kwenye kikao, siku ambayo saa nane alipendekeza zitto tukutane naye zitto alikwenda marekani kuzindua tawi la chadema, ni saa nane ndiye aliyenilaumu sana kuwa kwa nini sikumuarifu kuwa zitto hatokuwepo, nilimjibu sio wajibu wangu kuwaambia watu kuwa zitto yupo ama hayupo.

8. Ni Saanane huyu huyu mnafiki tuliyerumbana naye hasa mimi nay eye juu ya namna ya kumshirikisha zitto kwenye michango ya kikundi chake cha PM7. Naomba ninukuu mabishano yetu..mimi ‘’ kama swala ni kukusanya pesa, kwanini tumfuate Zitto kwanza na sio mtu mwengine yeyote’’?...saa nane..’’kwa sababu zitto ni kijana na ana mitazamo chanya kwa vijana wenzie na pia tunafanana nayo mitazamo hiyo sio kamakina mnyika wao status quo’’…mimi..’’kama Zitto tumemwomba tuonane naye na amesafiri bila kutujibu hauoni kuwa anatuudharau, kwanini tujipeleke kwa zitto tunayemnung’unikia kila leo?’’..saa nane.. ’’ hapana ni lazima atusaidie, zitto kwa vyovyote lazima agombee uenyekiti, na hatuwezi fanya hii kazi tukamfungulia milango bila nay eye kutoka jasho lake, ni lazima atupe pesa’’….mimi sasa kwanini tunakataa wenzetu kutumiwa halafu na sisi tunajitumikisha wenyewe kwa zitto?’’…saa nane..’’Mchange, hakuna jinsi tunaweza acha mshirikisha zitto, mwisho wa siku zitto atakuwa beneficiary kwenye huu mpango’’… …………………ukifuatilia kwa makini mazungumzo yetu ambayo kwa bahati nzuri nimeyarekodi kuanzia siku ya kwanza mpaka ya mwisho utaweza kumuelewa SAANANE kuwa alikuwa na kazi maalum.

Niseme hapa kuwa wote kwa pamoja, saa nane na zitto kila mmoja ameniambia kwa mdomo wake kuwa hawajawahi kuonana uso kwa macho, zitto yeye anasema kuwa anaweza akakutana leo na saa nane barabarani na akapishana nae bila kumfahamu.

Wote kwa pamoja wameniambia kuwa mawasiliano yao huwa ni kwa simu hasa SMS na mara chache kwa emails.

Na moja kati ya malalamiko aliyokuwa ananipa saa nane nimpe zitto ni kuwa..
1.kwa nini hapokei simu za wapiganaji wake akiwemo yeye?...
2..kwanini anakuwa na mpiganaji kama saa nane na hataki kuonna nae….
3…kwanini hataki kukifadhili kikundi cha PM7.?

Kwa mtiririko wa matukio ulivyo, na kwa jinsi SAA NANE alivyoandika mashtaka yake dhidi ya zitto huku akizani anamchafua, hakika amejidharirisha sana.

Mtu mmoja mpinzani mkubwa sana wa zitto amenitumia sms kwenye facebook, ananiambia JF vipi maana COMPUTER YANGU HAIFUNGUI..huyu nae ni mjinga sababu anashabikia ujinga.

Kumshambulia zitto kwa mashtaka ya uwongo namna hii kuna mfanya zitto awe na nafasi ya kuonekana anasingiziwa mamba mengi sana hasa ndani ya chama.

Kwa mimi ninayemfahamu Saanane nje na ndani, na ninayefahamiana na kufanya kazi na Zitto, kwa mashtaka haya ya uwongo, basi hakika nitazidi kumuamini Zitto.

Nitazidi kuamini kuwa Zitto amesingiziwa mambo mengi sana ndani na nje ya chama, ninazidi kumuamini na kumtia moyo kwamba hizi ni hatua za mwisho za watu wanaokupinga, wakishindwa kukupinga kwa facts, watakupinga kwa uwongo…saa nane amekubali kutumika vibaya kwa kisingizio cha kuwa anakilinda chama na viongozi wake.

Napata mashaka kama anakielewa anachokisema, huwezi kumtenganisha zitto na uongozi wa chama. Zitto ni naibu katibu mkuu wa chama, hivyo sio rahisi kumchafua zitto ukaacha kukichafua chama.

Nimemwona saa nane anajitetea kutishiwa kuuawa, saa nane, ZITTO akiwa na mimi amenusurika kuuawa kwa ajali ya gari hivi karibuni tukitokea morogoro kwenda iringa(siku ya kumbukumbu ya kifo cha mwalimu nyerere) baada ya wapinzani wake ndani ya chama kwenda kufungua nati za tairi la nyuma ili afe, kweli zitto ameaga kwao, kweli zitto hataweza kufa kwa mipango ya mungu, hatukufika mbali tuliushtukia mchezo tukarudi morogoro mjini na zitto akaendelea na retreat yao mpaka kesho yake tukarudi dar wala hakuitangaza hii sababu aliwadharau na mbinu dhaifu.

Sio rahisi kuitoa roho ya mwanadamu mwenzio, sio rahisi kumuua zitto kama mlivyojaribu mara kadhaa na timu yenu ..

Nasikitika sana kama vijana sasa tunaeza kusimama kidete na kuandika uwongo na kuutetea bila hata woga kama ndugu yangu Saanane.

Hasira yako ya mimi kukushtukia na kuwaambia kina Mwampamba na Juliana kuwa wewe kila siku una warekodi na kwenda kuuza habari kwa kiongozi mmoja wa juu ambaye humtumia HAWARA WAKE kutuma SMS za matusi kwa watu, isiwe sababu ya kuanza kuwachafua watu ndugu yangu.

Mchafue Zitto kama unahisi una sababu ya kufanya hivyo kwa mambo ambayo una ushahidi nayo.

SAANANE acha tabia ya KUBUNI MGOGORO, KUUANZISHA, KUUENDELEZA, NA KISHA KUUTUMIA KAMA CHANZO CHAKO CHA KUPATA PESA.

SAA NANE, Waislam wanasema sifa za mnafiki tatu (ayatul munafiq tharasa).
1. akiongea huongea uwongo..
2..akiaminiwa hajiaminishi/hudhiaki..na ..
3..akiahidi hatimizi..

Ndugu Machange asante sana kwa hayo uliyotuandikia ila kumbuka si kila mwanajamvi huridhika na physical answers kuna physical evidence za Zitto kuwa msaliti kwa chama ila kwa busara za viongozi wa chama wamekuwa wakifumbia macho baadhi ya hayo mambo naninajua ww ilo walijua pia......
 
tatizo ambalo linanifanya nisipende kuongelea sana siasa ni kuwa kwanza huku ndani kuna watu wanakuwa na bias hata kwenye masuala ya msingi!penye ukweli ukisemwa watu hutoa mapovu,lkn huko chadema nadhani kuna matatizo makubwa,japo mashabiki hawataki kuyaongelea kabisaaa!!!

Mkuu kunaneno umelitamka hapo MASHABIKI HAWATAKI KUYAONGELEA KABISAA!!!
Ndio ukweli mashabiki ni wengi kuliko great thinkers.Wengi wanatumia moyo kuliko ubongo kwenye kuongea mambo.
Ila bora hao kuliko Mamuya na Ben saanane walioamua kujitundika kitanzi kwa dau la x mass.
 
pilipili ni mboga na huwa nazitafuna kila baada ya masaa sita.
Hoja hujibiwa kwa hoja, kauli zako zimejaa upambe flani wa kujivua ufahamu.
Jipange sana mkuu, unamtia aibu aliyekutuma
Nipe hoja nikujibu kwa hoja.Naona unahamu ya kusikia hoja kutoka kwangu
 
Back
Top Bottom