Bei ya mahindi kuua wafugaji wa kuku Tanzania

bid2015

JF-Expert Member
Sep 6, 2011
306
59
Ndugu watanzania bei ya mahindi mwisho wa Feb 2023 ilikua kwa jumla 1, 120 kwa Dar Es Salaam lakini bei ya leo 6 March 23 yamepanda kufikia 1, 330 kwa kilo moja.

Ongezeko hili ni hatari kubwa kwa wafugaji wafugaji wa kuku na wengineo kwa sababu ongezeko hili ni sawa na 5, 000 kwa mfuko wa chakula cha kuku ambao tayari upo juu sana.

Pamoja na sera nzuri za mama samia tunaomba serikali iliangalie hili kwa haraka sana tofauti na hvyo serikali ijue inawachimbia kaburi wajasiria mali wadogo wadogo

Serikali zote duniani kazi ya kwanza ni kulinda biashara zisife ili uchumi uendelee kukua. Serikali inahitajika hapa kulinda wafugaji

Asanteni naomba kuwasilisha
 
Tuzuie mahindi kwenda njee wakulima wapate maimivu ili mfuga kuku na mkazi wa mjini wanufaike!

Badge will go down as the best waziri kilimo ever
 
Tuzuie mahindi kwenda njee wakulima wapate maimivu ili mfuga kuku na mkazi wa mjini wanufaike!
Badge will go down as the best waziri kilimo ever
Saizi kuna mkulima gani ana mahindi ndani au sokoni?

Mabwanyenye ndio wamerundika mahindi kwenye maghala huko
 
Saizi kuna mkulima gani ana mahindi ndani au sokoni?

Mabwanyenye ndio wamerundika mahindi kwenye maghala huko
Inawezekana hata hao mabwanyenye walishawauzia kina wasomali, wao wametengeza demand kwa nguvu kupitia nafasi zao, sasa ni muda wa wao kujilimbikizia mali kwa gharama za wananchi wote
 
Mbona hueleweki?

Kwani wakulima wa Tanzania hawapaswi kulindwa?

Unataka walindwe wafugaji wa kuku kwa gharama ya kuvunja moyo wakulima?
 
Unga unazidi kupanda leo bei imekuwa 47k kwa 25kg kuna mashine nimeenda kuuliza naambiwa 53k jwa 25kg.
 
Daaah asante sana kwa ushauri huu....maana nilikuwa na mgongano wa mawazo ...

1-Nianze na kilimo.

2-Nianze na ufugaji.

Ila kura zinaelekea kwenye kilimo kwanza
 
Back
Top Bottom