Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa
Paul Matthysse
Pia anajulikana kama
P Funk, Majani, Kinywele Kimoja, Mdachi nk.
Asili yake
Tanzania
Aina ya muziki
Hip Hop na Bongo Flava
Kazi yake
Mtayarishaji
Ala
Kinanda,Guitar, Kinakilishi
Miaka ya kazi
mn. 1995 -
Studio
Bongo Records
Ame/Wameshirikiana na
Master Jay , Bonny Luv,Rajabu Marijani, Bizz
Man, Boznia nk.
Paul Matthysse ( P Funk ) ni mtayarishaji wa
muziki na pia mmiliki wa Studio ya Bongo
Records iliyopo jijini Dar es Salaam , Tanzania . P
Funk ambaye nusu Mtanzania nusu Mdachi,
kama miaka ishirini iliyo pita hivi .P Funk a.k.a
Majani, alikuwa na hisia za kupendelea muziki
na pindi hadi kuamua kufanya kweli.. kuvutiwa
kwake kupenda muziki ndio chanzo kikumbwa..
kilicho pelekea kufanikiwa vizuri katika muziki.
Kwenye Miaka 1991 - 92 wakati yupo bado shule
IST (International School Of Tanganyika. Alikuwa
mtundu mtundu kwenye studio za pale shule..
kupiga- piga midundo mbali mbali ya hapa na
pale na kufoka-foka(Rap music) na pia alikuwa
mbele sana kwa kupiga musiki kwenye Pati
mbali mbali.. na hapo alikuwa kupenda sana
musiki kwa ujumla.
Elimu ya Muziki na Uzoefu Wake
P-Funk alikwenda kimasomo ya Mlio (sound)
engineering kwa miezi 18 pale Amsterdam ,
Netherland kabla ajaingia kwenye kutayarisha
muziki. Alikuwa anajua kitu anachotaka kufanya.
Mwaka 1995 akiwa na vifaa vyake vichache
alianzisha kampuni yake ya kurekodi muziki
nyumbani kwake. Na ni katika kipindi hicho
hicho neno Bongolilipokuwa linatawala katika
misemo ya kiswahili cha mitaani na lilikuwa
linaelezea hali halisi ya maisha ya Dar es Salaam
na ndio kipindi hicho album ya Bongo
ilipozinduliwa. Akiwa bado ni mtayarishaji muziki
mdogo, amefanikiwa kupata umaarufu mkubwa
katika fani ya muziki na hasa katika milipuko ya
nyimbo zenye ladha ya Bongo.
Anakubali kuwa amepata sana utaalam na
mbinu kutokana na kufanya kazi watayarishaji
wengine wa muziki wa Kitanzania kama Master
J, Bonny Love na Rico. Mawazo yake na namna
ya kuyaoainisha na muziki ndio hasa ambacho
kinafanya muziki wake ufanikiwe.
Tuzo Alizopata
1 Kili Music Awards. ( 2003 )
2 Kili Music Awards. ( 2005 )
3 Kili Music Awards. ( 2006 )
Wasanii Aliowainua
Kwanza alianza kwa kumpandisha chati Juma
Nature ambaye ndio nyota wa nyimbo za Bongo
Flava na akaendelea kwa kutayarisha santuri ya
Solo Thang, AY , Zay B, Sista P, Mike T na pia
alishawahi kufanya kazi na Professor Jay alipotoa
santuri yake mwenyewe. P Funk ana wasanii
wengine wengi wanaotumia nembo ya kampuni
yake katika Utengenezaji wa albamu.
Pia Anajulikana Kama
P Funk
Halfani
Majani
Kinywele Kimoja
Mkono wa mungu. mia