Mmmh sijui kama kuna wa kupewa pongezi
Alichofanya Western countries kwa Africa ndicho anachokifanya Mchina leo
Tofauti ya hawa wawili Technology imekua zaidi kulinganisha na miaka ya nyuma
Hakuna jema kwetu kama Taifa wote hawa ni wezi tu period!
Pascal Mayalla BAK
Wachina ni wabaya zaidi
Tunadanganyika na misaada na mikopo ya riba ndogo ya Wachina lakini wanayovuna Africa yanatisha
Mjerumani hata kama aliiba lakini alikua na jukumu kubwa la kuijenga nchi mana aliishi humu humu na hakuwa na mpango wa kuondoka ndio maana maeneo waliokaa yalipata maendeleo makubwa sana.
Na pia hata rasilimali walizoziacha karibu zote zimeshindikana kuendelezwa kwa kiwango walichokua wanakiendeleza na nyingine mpaka leo zimebaki historia tu na hazijulikani zilipo.
Kifupi Mjerumani alidhulumiwa lakini alikua na nia nzuri kuliko makoloni mengine ikiwemo koloni jipya la CCM na Mchina wake.
Madhara yoyote yatakayokuaja kuipata Tanzania chini ya Ukoloni mpya wa Mchina wa kulaumiwa ni CCM mana wao ndio makuwadi wa rasilimali zetu kwa mchina wakati tulishapata Uhuru na kumfukuza mgeni tuliyedhani anatunyonya japo kiukweli sisi ndio wanyonyaji kupitia watawala wetu tangu ujima.
Haijawahi Mtawala mweusi akawa sawa na Mwananchi wake rangu kuumbwa kwa dunia hii.
Watawala wa kiAfrika ni hatari sana kwa watu wao kuliko kiumbe Chochote kilichoumbwa na Mungu tangu ujima.
Wamisionari waliwakuta Machifu wa Kiafrika zamani hizo wakipora mpaka wake za watu na ng"ombe walionona .Wamosionari ndio waliosimama Kidete kupinga ujinga wa machifu kupitia walinzi wao na wapambe wao kupora wake za watu na ng'ombe zao na kwenda kula.
Mjerumani akaweka sheria Kali kudhibiti ushenzi wa Mwafrika .Hili ni lazima tuliseme ili tujenge historia mpya njema. Historia za kweli zilipotoshwa kuwatukuza watu waliopaswa kulaaniwa na kuwalaani waliopaswa kusifiwa. Ndio maana mpaka leo Afrika ni maskini na hawawezi kamwe kusimamia rasilimali zao wenyewe bila kuwaita ama hao wakoloni wapya wa kichina au kuendelea kushirikiana na zimwi likujualo.
Mjerumani kwa karne moja iliyopita na muda mfupi aliokaa alifanya makubwa sana ukilinganisha Teknolojia ndogo ya wakati huo.
Waliijenga Afrika wakijua kuwa wameshafika nyumbani hawoandoki.
Mjerumani ameikuta jamii ndogo kama ya Wachaga ikiwa imegawanyika kwa kuwa na vita ya makundi madogo madogo kwa karne nyingi.
Vikabila vingi,koo nyingi, lugha nyingi ndani ya maeneo madogo sana na mila tofauti tofauti Afrika ni ushahidi kuwa hatukuwa wamoja kama tunavyodanganywa na akina Prof. Blablah.
Sijawahi kumkubali Mchina kabisa mana naina atakua ni hatari sana bora Mzungu mana mfano Mmarekani kuna waafrika wenzetu wengi kule na wananafsi kubwa kwenye Taifa hilo lenye uchumi mkubwa Duniani.
Hata majeshi yao yana waafrika wengi sana. Na kila nyanaja waafrika wenzetu wameshika sana hilo Taifa lenye watu mchanganyiko tofauti na Mapatina wa CCM wachina ambao hata hao CCM wenyewe hawajawahi kuishi huko au kuwaweka ndugu zao au wake zao wafanye kazi au kujenga China au kuoa au kuewa China.
Au hata kuwa na imani inayofanana na ya watu wetu wengi inayomjua Mungu wa Nabii Ibrahimu na sheria za Mussa.
Sasa hiyo thamani ya waChina kwetu inatoka wapi??
Kama kawaida CCM inatutengenezea Janga kubwa sana kwa vizazi vijavyo kwa faida ya madaraka yao ya leo. China inawapa kiburi cha kuua demokrasia bila kujaua kuwa wanalinda uongozi wa kiimla kwa gharama ya kuumiza na kumwaga damu za watanzania wenzao kama anavyohamasiasha muovu mmoja anayeitwa Msiba mkuu na Mwenyekiti wa UVCCM.
Kupanga ni kuchagua; kama tumeamua kuachana na ushirika na utegemezi kwa mataifa makubwa basi tusijidanaganye kuwa China ni Taifa salama kwetu.Ni hatari Mara mia moja ya wazungu ambao kiukweli wana utu angalau kidogo ndio maana hata sheria zao sio za kikatili sana kama China; mana Serikali ya China wanajijua kuwa watu wao wana Tabia za kishetani hivyo wanapaswa kuwekewa sheria na adhabu za moto ili wakae kwenye mstari.