BBC: Magufuli prefers Chinese to Western

BBC: Magufuli prefers Chinese to Western

Binafsi simpingani na hoja ya rais hata kidogo. Ni jambo zuri Sana Kama sisi Kama sisi tukijitegemea ama tukimpenda kupokea mikopo yenye masharti nafuu zaidi toka kwa wachina. Binafsi sikubaliani na kuambiwa eti tutambue haki za mashoga ama ndoa za jinsia moja. Na kwenye kumbukumbu zangu nakumbuka kikwete alikuwa na hekima Sana kulikataa hili swala la mikopo yenye masharti magumu.

Swali la kujiuliza je rais kea kulisema hili pale udsm mahali ambapo 3/4 ya wahadhiri wake wanasomeshwa na hao wazungu je haoni kuwa Lina direct impact kwenye elimu Zaid kuliko kwenye miradi ya maendeleo?

Je hakukuwa na namna nyungine nzur Zaid ya kuisifia mikopo hi zaidi ya kutumia kauli hii?
 
tahadhari: western hung'ata na kupuliza. mchina yeye hung'ata tu.
 
Umewahi kuona shoga yoyote akilazimishwa kufanya huo uchafu? Hayo ni makubaliano ya watu kwa matumizi ya miili yao. Hayana madhara kwa taifa kwenye maendeleo wala amani yetu. Huyo jamaa anawakimbilia wachina kwani wao huwa hawahoji ubazazi unaofanywa na viongozi wa kiafrika dhidi ya wananchi wao.
Mungu akusaidie
 
tahadhari: western hung'ata na kupuliza. mchina yeye hung'ata tu.
Hizi fedha za western toka zilipoanza kuja zilikuwa zinaishia kwa vibaraka wachache hata chaki hazinunui. Lakini za China walau makabwela tunaziona, madaraja tunapanda n.k
 
tahadhari: western hung'ata na kupuliza. mchina yeye hung'ata tu.
Hizi fedha za western toka zilipoanza kuja zilikuwa zinaishia kwa vibaraka wachache hata chaki hazinunui. Lakini za China walau makabwela tunaziona, madaraja tunapanda n.k
 
Tatizo la Nchi za Ulaya ni kutoa misaada na mikopo ya masharti nafuu wakitupangia na mitindo ya maisha. Kwa mfano tumeshaona mara kadhaa wakiitishia Uganda kuipotezea kwakuwa tu Serikali na jamii kwa ujumla haiungi mkono ndoa za utotoni na ushoga, vitu ambavyo wao Ulaya wamevibatiza jina la "haki za binadamu". Rais Museveni aliwapa makavu kwamba hayo mambo hayana nafasi Uganda na wala sio utamaduni wa Kiafrika. Lakini maisha yanasonga hadi sasa misaada haijakatwa wala nini.
Ni vizuri watuone kwenye rangi zetu kama hivi, na si vizuri kubabaika kwa kila mkwara unaochimbwa. Nakubaliana kabisa na Pascal Mayala kwamba "we are not that poor", kiasi kwamba tukubali kila upuuzi kutoka huko.
 
Kwahili namuunga mkono John, mtu anakupa msaada na masimango kibao, misaada si afya kwa Taifa ila wanatufanya mazuzu mno kwa kutupangia lifestyle
Hakuna misaada isiyo na masharti. Au unadhani hiyo misaada tunapewa bure? Kama Hutaki misaada jenga uwezo wa kujitegemea na uhakikishe unajitegemea. Subiri uone hao wachina watakavyowafanya mtakaposhindwa kuilipa hiyo misaada. Na wakati huo huyu mnayedai mnampongeza atakuwa keshaondoka madarakani mnabaki kujuta tu
 
...brainwashed. Mlishindwaje kufanya ubunifu kwa miaka 30 ya 'demokrasia ya kuwa chini ya maelekezo kutoka kwa wazungu au nchi za magharibi?

Hapa utadhani umetoa hoja kabambe, kumbe ni upuuzi mtupu.

Nipe mfano mmoja tu wa nchi yoyote duniani iliyokuwa ya demokrasia au ukandamizaji iliyoendelea ndani ya hiyo miaka 30 unayoizungumzia, sijui hata hiyo 30 umeiokota wapi?

"-----miaka 30 ya 'demokrasia ya kuwa chini ya maelekezo kutoka kwa wazungu----". Kwa hiyo hapo unataka maelekezo kutoka kwa waChina? Hao waChina walileta maendeleo ndani ya miaka 30? Hivi kichwani zimo au ni yai tupu?
 
Hakuna misaada isiyo na masharti. Au unadhani hiyo misaada tunapewa bure? Kama Hutaki misaada jenga uwezo wa kujitegemea na uhakikishe unajitegemea. Subiri uone hao wachina watakavyowafanya mtakaposhindwa kuilipa hiyo misaada. Na wakati huo huyu mnayedai mnampongeza atakuwa keshaondoka madarakani mnabaki kujuta tu
Hujaelewa hoja yangu,irudie kuisoma then ucomment
 
Raisi magufli (as a person) ameprove kua moja ya viongozi wenye ujasiri wa hali ya juu sana kutokea nchini kwetu. serikali kama taasisi iweke mfumo mzuri wa kumuongoza na kumchallenge (kuweka checks and balance) kwa manufaa ya ustawi wa Tanzania kama nchi...maana hao westeners anaowaambia ukweli kiuhalisia wana nguvu kuliko nchi moja moja ya kiafrika. viongozi wengi wa kiafrica waliojaribu kupambana nao walishindwa ( refer Mugabe alipojaribu nini kiliikuta sarafu yake, refer pia Ghadafi alipowagusa nini kiliikuta libya) na afrika ikawa inatizama tuu. si mbaya kuwa jeuri kwa maslai mapana ya nchi yetu..lakini kwa mazingira tuliyopo ya kimataifa hili lifanywe kwa utaalam na uangalifu mkubwa sana maana afrika ukibuma umebuma mwenyewe hamna umoja wala uzalendo wa kusupportiana zidi ya kutoa matamko ya 'kulaani vikali' na kutoa pole
Magufuli ajifunze kwa mchina mwenyewe bado hata haonyeshi ngebe za Magufuli na nguvu aliyonayo japo utajiri wake ni sawa tu na jimbo la Calfornia kwanza sisi hatukuwahi kuchukuwa upande tulikuwa ni non alliance yaani wote wetu sasa yeye anataka kuacha kizazi hiki na kijacho kikiwa kimesambaratika kwa kutopoka ropoka tu naamini alivyojisema mwenyewe ni kichaa kweli kwelibajeti ipi ya mchina inasaidia afya elimu maji kilimo biashara elimu ya juu uvuvi mazingira kuliko hao wa western maskini jeuri asiye na maono anaendesha nchi kaa kipofu tuu
 
Wazungu wana tofauti gani?
mchina ni brutal anadharilisha hana utu mikopo yake isiyo na masharti nchi kama cambodia srilanka zambia na wengineo zimeanza kuwatokea puani Magufuli awe anajisomea yeye ni ropo ropo kaa mwanawe bashite
 
mchina ni brutal anadharilisha hana utu mikopo yake isiyo na masharti nchi kama cambodia srilanka zambia na wengineo zimeanza kuwatokea puani Magufuli awe anajisomea yeye ni ropo ropo kaa mwanawe bashite
Mzungu ni brutal pia, au umeshasahau historia ya ukoloni mara hii?
 
Haya ndio mambo akina sisi tunayompogezea rais Magufuli, asikubali kupangiwa cha kusema eti tuu kwa kuogopa kunyimwa mikopo na misaada yenye masharti.

Yes sisi ni masikini as beggars as we are lakini sisi ni masikini jeuri, we are not that poor
Je, Tanzania ni masikini hivi kuendelea kupokea mikopo na misaada yenye masharti kinyume cha uhuru wetu?, au tukatae kama Nyerere?. - JamiiForums

Kumbe watu wa Nyerere bado wapo na wana misimamo kama Nyerere. Hongera MFA, Dr. Mahiga kwa msimamo, tusikubali kuyumbishwa - JamiiForums

P
Misimamo ya Nyerere ilitufikisha wapi? We have to learn kwa wanaotuzidi si kushupaza shingo wakati mfukoni unazama kwenye lindi la umasikini.

Msimamo ni mzuri ila bila step msimamo ni ujinga mno
 
Back
Top Bottom