Inabidi ufike wakati (kama bado haujafika) waafrica tuamue kusimama kwa miguu yeti wenyewe na tuseme 'enough is enough', wale wanaokuja na misaada au mikopo ya kipuuzi tuwaambie hatuihitaji. Wanatusokomezea haya na mikopo ya mashariti ya kipuuzi kwa kuwa wanajua hatuna ubavu wa kukataa. Tunao uwezo kabisa wa kuwa maskini jeuri endapo tutaamua kupenda nchi zetu na kutumia vizuri kile tulichonacho ili kujiletea maendeleo. Wote, westerners na Chinese, siyo mwarobaini wa maendeleo yetu, sisi wenyewe ndo dawa ya maendeleo yetu.
Namkubali Magu kwa angalau kuliona hilo na kusema 'tukiamua tunaweza'. Najua ni kazi ngumu kubadilisha mtazamo wa watu toka ule wa utegemezi kwenda mtazamo positive wa 'we can do it', lakini hata kule kuanza kufikiria nje ya 'box la utegemezi' na kuanza kupandikiza mbegu ya kujitegemea na kujiendeleza wenyewe, ni hatua nzuri inayostahili kupongezwa.
(There's no free lunch, there's no lunch at all'; JPM 2018)