Ugonjwa wa Kuota Vinyama Sehemu za Siri (Bawasiri/ Hemorrhoids): Chanzo, Dalili, Tiba na Kinga

Ni muda sasa hili tatizo linanisumbua ,ilianza kama kinyesi kinakua cha pingilipingili kigumu.kikiwa kimechanganyikana na damu,wakati wa kunya ni shida,maumivu makali sana,,wakati mwingine muwasho ile mbaya nikaenda hospital nikapewa dawa tatizo likapotea.pia kuna dawa za kienyeji nilikua natumia .
Hali imejirudia,niliweka kioo kuangalia nikaona nyuma ya mfereji wa tundu la mkundu kuna kanyama kameota,kana fanana na ngozi tu ya kawaida,nisipo kunya nikakaa kama siku mbili pale panaacha kuuma,nikinya baada ya nusu saa maumivu yanaanza kwa ndani ,na pembeni pamevimba kama jipu ,na zaidi ya wiki sasa,nifanyaje ndugu zangu?,namawazo sana,je ntapona kweli?
Pole mkuu vp uko kiumeni nn pende za Ukonga??
 
Hiyo ni hemmorhoid/piles au bawasiri in Swahili and tiba zipo za hospital, za kubadili lifestyle ya kula, maji kwa wingi, matunda yenye fibers kama ndizi,maembe

Dawa za hospital ni kuna suppositories za Ku insert inside the anus na kuna cream za kupaka ambazo zinatoa muasho,uvimbe na maumivu

So nenda tafuta dawa in any community pharmacy ulizia preparation H suppository or cream huku ukiwa unakula vyakula vya fiber
Zingatia maana hiyo hali ikiwa sugu zaidi italuletea shida zaid kwenye colon na hata kuleta cancer ya colon.
 
Pole Mkuu,kwa maelezo uliyotoa inawezekana ikawa bawasiri..hata hivyo nikutie moyo kwamba tatizo lako linatibika.nenda hospital yoyote iliyo karibu nawe.
 
Mkuu, huwezi kusoma comments za kuelewa? Watu watu wawili wamethibitisha kuwa utomvu wa mgomba ama ndizi ni dawa nzuri na inaponesha kwa mapema mno kuliko hayo madawa yanayotembea kwa wiki 3 mpaka 4.

Nadhani Mkuu ni vyema ukafuata njia ambayo wenzeko waliitumia maana wana uthibitisho.
Sure mkuu
 
Utomvu huu ni wa matawi au hadi nikate kile cha katikati? Please help kuna mtu wangu wa karibu anahitaji msaada haraka
Kwenye tawi kuna majani ya mgomba yale ya kijani ambayo huwa yanatumika kubanikia wali uive vizuri sasa acha hayo kata kipande kinachoyashikilia hayo majani utoe utomvu wake AU kata gome la chini teketeke ilimradi tu upate utomvu wake .

AU

Tafuta malimao ukamue maji yake then apakae kila anapoenda kuoga au kulingana na maumbile ya nyuma yalivyo akate limao katikati then awe anasugua kwenye eneo husika
 
Kwenye tawi kuna majani ya mgomba yale ya kijani ambayo huwa yanatumika kubanikia wali uive vizuri sasa acha hayo kata kipande kinachoyashikilia hayo majani utoe utomvu wake AU kata gome la chini teketeke ilimradi tu upate utomvu wake .

AU

Tafuta malimao ukamue maji yake then apakae kila anapoenda kuoga au kulingana na maumbile ya nyuma yalivyo akate limao katikati then awe anasugua kwenye eneo husika
Shukrani mkuu! Migomba nyumbani ipo, nitampa hii lesson
 
Kwenye tawi kuna majani ya mgomba yale ya kijani ambayo huwa yanatumika kubanikia wali uive vizuri sasa acha hayo kata kipande kinachoyashikilia hayo majani utoe utomvu wake AU kata gome la chini teketeke ilimradi tu upate utomvu wake .

AU

Tafuta malimao ukamue maji yake then apakae kila anapoenda kuoga au kulingana na maumbile ya nyuma yalivyo akate limao katikati then awe anasugua kwenye eneo husika
Inamaana hata limao pekee linatibu?
 
KUTOKWA NA KIJINYAMA SEHEMU YA HAJA KUBWA ( HEMORRHOIDS)
MIWASHO, MAUMIVU NA VIMBE KATIKA TUNDU LA HAJA KUBWA

Bawasiri ni ugonjwa ambao unatokana na kuathirika kwa mishipa ya sehemu ya ndani na nje ya tundu la haja kubwa na hupelekea wakati mwingine kutoa damu wakati wa kutoa haja kubwa.

Ugonjwa huu unasababisha muwasho na maumivu makali katika tundu la haja kubwa. Ila kwasasa ugonjwa huu unawaathiri mpaka watoto wa umri wa chini kabisa:

CHANZO CHA UGONJWA WA BAWASIRI
Bawasiri ni tatizo linaloanzia kwenye mfumo wa mmeng'enyo wa chakula. Huu mfumo ukishakua mbovu hupelekea kutokupata choo vizuri(Haja kubwa)

Mfumo mbovu wa mmeng'enyo wa chakula unasababisha chakula kisimeng'enywe vizuri kwenye utumbo mdogo na hivyo kupelekea chakula kupiliza kwenda moja kwa moja kama kilivyo kwenda kwenye utumbo mkubwa ambapo maji maji kutoka kwenye chakula hufyonzwa na kuacha chakula kikiwa kikavu.Inapofikia wakati wa kupata choo; choo kinakua kikavu hivyo unatumia nguvu nyingi kukisukuma choo kitoke.

Hali hii hupelekea misuli ya haja kubwa kutanuka na kupelekea kukwanguliwa na choo kigumu na hivyo kinyama kuanza kujitengeneza, Hivyo husababisha kuanza kusikia maumivu na miwasho kwa ndani, na mara nyingine kupata choo chenye damu.

Hivyo basi kadri unavyoendelea kupata choo kigumu misuli ya tundu la haja kubwa huendelea kuathirika zaidi k mpaka kinatokeza.
Mtu mwenye afya nzuri anapata choo kulingana na milo aliopata kwa siku. Kama unauwezo wakupata milo mitatu kwa siku, unasitahili kupata choo mara tatu kwa siku, tena choo chako kitoke na urefu sawa wa ndizi mbivu, bila kujikatakata kama kile cha mbuzi.
Bawasiri pia huweza kusababishwa na:

-Kufanya mapenzi kinyume na maumbile,
- Ujauzito
- kuhara kwa mda mrefu
-Kutopata choo kwa mda mrefu

DALILI ZA UGONJWA WA BAWASIRI
- Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa. Huu muasho unakuja kwa kujirudia mara kwa mara baada ya muda furani

- Kukatishwa kwa haja kubwa na kurudi ndani wakati wa kujisaidia. Kitendo hiki huongeza msuguano katika mishipa ya ndani ya tundu la haja kubwa.

- Kujitokeza kwa uvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa. Uvimbe huu unaanza kuota kama upele na huambatana na miwasho na maumivu makali.

- Kujitokezea kwa kijinyama katika tundu la haja kubwa. Kinyama hiki kinaanzia ndani ya tundu la haja kubwa na kutokea nje ya Tundu la haja kubwa. Hatua hii huashiria tatizo limesha kuwa kubwa na una hili tatizo la bawasili kwa muda mrefu, na linaweza kusababisha vifo vya gafla kwa sababu mishipa inayosafirisha damu ndio inakwanguliwa na mwishowe kuathirika.

Chukua tahadhari mapema kabla hujaathirika sana au upoteze maisha; kwasababu hiki ni chanzo cha kupatwa na magonjwa mengine mengi ya kiafya.

- Kujisaidia kinyesi chenye damu na kunuka kwa harufu mbaya sana
- Kupumua na kushindwa kuzuia kinyesi wakati ukipumua(kujamba na kutoa haja kubwa)

MADHARA YA UGONJWA WA BAWASIRI
  • Upungufu wa damu mwilini
  • Kupata maumivu makali wakati wa kujisaidia haja kubwa na kusababisha mishipa ya sehemu ya haja kubwa kukwanguliwa.
  • Kuna uwezekano mkubwa wa kupata saratani ya utumbo (Cancer) kwasababu kile kinyama kinakaa kama kidonda
  • Kutopata hamu ya tendo la ndoa kwa jinsia zote. Yaani Mwanamke na Mwanaume.
  • Kuathirika kisaikolojia na hupelekea kuptojiamini katika hadhara ya watu hasa pale miwasho inapoanza.
  • Kuvuja damu, maumivu ya mda mrefu na hupelekea kushindwa kukaa.
  • Maumivu ya mgongo ya mara kwa mara na kiuno.
 
Back
Top Bottom