BAVICHA Ifukuze waasi wote - Ben Saanane

BAVICHA Ifukuze waasi wote - Ben Saanane

Mjadala huu uko very clear na mimi naunga mkono wito huo kwa asilimia mia moja, lakini kwa ajili ya kuweka kumbukumbu sahihi nitalisemea hili la ubunge Ukonga.
So far sijaona kiongozi yeyote wa BAVICHA ndani ya jimbo la Ukonga anayeweza kuwa na ushawishi wa kisiasa zaidi ya Mikael P Aweda.

Kuna baadhi ya vijana wamejiingiza katika siasa siku za hivi karibuni na kujipa matumaini ya kwamba wanaweza kuwa wabunge bila hata kutafakari kama wanao uwezo wa kuwa wabunge. Na kwa mtiririko wamejikuta wakihaha kila kona kutafuta uwezeshaji na kutokana na hilo wameishia mikononi mwa ccm, na katika kuahidiwa kutimiziwa matakwa yao wamelazimika kuleta vurugu kwenye chama kwa kudhani kwamba watafanikiwa aidha kwa kupitia chadema, ama ccm incase wamefanikiwa kuivuruga Chadema ili kuirahisisha kazi ya ccm kwani kwa hali halisi ya sasa ni ndoto za mchana kwa ccm kushinda Ukonga.

Mkuu MM.
Naunga mkono mawazo yako kuwa kuna vijana wengi wamevamia siasa na kuamini wanauwezo kuwa wabunge si ukonga tu bali naamini karibia sehemu kubwa ya tz yote.
Simpingi aweda ila naamini kusema hakuna kiongozi yoyote wa bavicha ukonga mwenye ushawishi zaidi ya Aweda hayo ni mawazo yaliyokosa utukufu wa kisiasa ktk watu walio upande mmoja.
 
Last edited by a moderator:
Bavicha kuna uozo sana kwanza sijaona kazi walio ifanya mpaka sasa,mambo yote niheche pekeyake,viongoz wengind hata majina siwajui,heche analazimika kuzunguka nch nzima wenzie wamekaa tu.vijana wa Tz wanaijua BAVICHA?

Na wengine ni wajumbe wa kamati kuu wanadiliki kumtukana dr wazi wazi hivi watu wasio na nidham wana nafasi gani katika CHADEMA?timuwen wote wataka vyeo na waingia tamaa na wasaliti,Mbowe na Dr. Slaa ni majembe na wanaongoza vema ila kuna wajinga wajinga wanataka kufanya CHADEMA nikama CCM. Viongoz wajuu fukuzen hao bana maana huku mtaan CHADEMA nikila upande msihofu kuchukua maamuz magumu fanyeni kama katiba ya CHADEMA isemavyo CHADEMA ni chama tawala ifikapo 2015,ila tutapitia mabonde mengi sana tusife moyo ushind ushafika

hakuna taasisi muhimu kama baraza la vijana na baraza la wanawake.Kimsingi kuna maswali mengi sana kuhusu uhai wa chama cha CDM, sababu, baraza la vijana halijafanya kazi ipasavyo kupta matawi mengi, kujenga mfumo sitahiki, lakini uongozi upo.Ni kweli nakumbuka enzi za nccr kugawanyika serikali ya ccm ilitumia mamluki kutengeneza mgawanyiko huu, hivyo ni vyema kuondoa virusi kama tambwe hiza akina msabaha , dr.lamwaina wengine wengi.
 
Fukuza hao virus aina ya Trojan wanaotaka kuharibu chama siku zote vijana ndo walinzi wa Chama, BAVICHA onesheni uimara wenu kwa kuwa 'purge' hao mamluki!!!
 
Binafsi sio muumini mzuri wa CDM lakini kinachofanywa na vijana hawa si kizuri kwa upande wa CDM

Lakini haya yote ni matokeo ya uongozi mzima wa CDM ndio uliopelekea hali hii
Tatizo la kwanza ni uchaguzi wa BAVICHA ulijaa ubabe wa wenye chama dhidi ya wengine Zitto & the co
Wenye chama walilazimisha wanao wataka wao na baadhi kutoka kambi nyingine kapewa nafasi kama kuzuga

Tatizo la pili ni kadri siku zilivyo zidi kusonga mbele wateuliwa wa wenye chama wakaanza kuwaona wengine waliopitishwa kufunika kombe kama maadui wao
Hapo sasa wakaanza kutengwa kwenye maamuzi nk rejea tamko la heche dhidi ya Shibuda

Na latatu ni kwamba hao wanaotengwa nao wameamua kujibu mapigo kwa kuonyesha chuki zao wazi wazi

Cha umuhimu hapa ni uongozi wa CDM kuangalia namna bora ya kumaliza mtiti huu walio uanzisha wenyewe
Leo hii ni rahisi sana kuwaona akina shonzi wasaliti kwakuwa tu watu wanaamini viongozi wao ni malaika hawakosei lakini uchaguzi ujao haya mambo yatajirudia tena maana mfumo wa maamuzi ya kibabe siku zote huleta makundi ndani ya chama "rejea CCM"

CDM inaweza kuwafukuza sawa lakini je chaguzi ijayo makundi ni lazima kwenye ushindani sasa kama yatajirudia tena mambo ya kudhani kundi linaloungwa mkono na fulani labda Zitto ni waroho na zikaanza hujuma na zengwe unadhani wagombea watakubali kukaa kimya....NOPE
Yatakuwa haya haya ya kuanzisha maneno wasaliti kwakuwa hawakuwa kundi la Mbowe, nawao watajibu mapigo kama wanavyojibu akina Shonzi

Unaweza ukawa muumizi mzuri sana wa demekrasia tena ukaodai kwa nguvu zote ikiwezekana watu wafe lakini binafsi ukashindwa kuiheshimu demokrasia pale unapokuwa wajibu wako kuitimiza
Hiki ndicho tunachokiona sasa
 
V.i.lenin aliwahikusema better few but better so its obvius kufukuza hawa wahujumu hakuzuiliki kwani ushindi ni pamoja na kuwashinda maadui wa nje na ndani.
 
Mwanasiasa kijana ndani ya chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA ambaye nyota yake iko juu Ben Saanane amelitaka Baraza la vijana CHADEMA BAVICHA kuwafukuza waasi wote wanatumiwa kukihujumu chama.

Namnukuu:

Kweli sasa kimenuka.Misimamo mikali kama hii ndiyo inayohitajika kwenye institutions
 
CCM ni chama kingine, kwa nini mwapenda kujondoa matatizo ya mfumo mbovu wa uongozi KISINGIZIO ni CCM!! Achaneni na unafiki, CHADEMA kimekosa dira na mfumo wa uongozi na utendaji ulio imara. Poleni sana mtazidi kulalama, CCM inasonga mbele kuelekea uchaguzi 2014 kabla ya kuwamaliza kabisa uchaguzi mkuu 2015

ww umeshikwa kubaya na cdm... ulalama kama Nape
 
Mimi pale mtu ambaye nitashtuka nikisikia amekula mlungula kufanya hujuma ni Slaa na Mnyika.
Wengine wote ni wajanja wajanja
tu watoto wa mjini kama alivyoimba Diamond.
 
Waasi wameibuka kimkakati!.. Mpango haujaibuka kwa bahati mbaya!.. Kuna hela ndefu chini ya nape!.. Wamesafirishwa toka mikoani na kuhudumiwa kwa gharama kubwa! Na bado wengi wataendelea kutoa matamko sawa na habari za gazeti la hoja na sauti huru!.. Wengine wamejiandaa kwenda CCM wakifukuzwa na wengine hawajui watafanya nini.
 
Fred Kavishe, ...aonywaye mara nyingi akishupaza shingo huvunjika ghafla. Bavicha waligombea wengi lakini kila nafasi anatafutwa mtu mmoja!.. Kushindwa na kugeuka adui wa chama chako ni usaliti. Watu hawa wamepewa mshiko wa nguvu na CCM!.. Hoja zao na msimamo wao unapatikana kwenye magazeti ya sauti huru na hoja. Pia hoja za Nape Nnauye wanazisimamia! Fuatilia nyendo zao na hoja zao kila wanapoitisha press conference!.
 
Makamanda wa Chadema wengi ni waganga njaa tu.

Mhh nafikiri hata aibu unaiona mwenyewe. Wengi walioko CDM ni wazelondo, hakuna ahadi kule wala fedha za walipa kodi au vyeo vya UDC.

Pro-Chadema JF ndio watakaozimisha Chadema ni suala la muda...ndani ya Chadema kila mtu ananulika tatizo bei tu.

Mtasubiri sana, Furaha yangu ni kwamba CCM ndio wanahemea ulimi, kumbuka kutoka kulala Bunge mkiamini mtarudi tu mpaka sasa mnakesha nani mumwangamize Dr, Mbowe, ZZT, Lissu< Lema, Kitila, Mnyika, Arfi, Prof safari mnachanganyikiwa. Mzimu wa safari Igunga unawasumbua sana. Vichwa vitupu kwenye safu ya Chadema.
 
Kumbu kumbu kwamba kuna siku alikuwa mwanachama wa CCM wakati ikiwa chama kinachotetea wanyone, walikuwa hawaamini kwenye ufisadi, wizi, uhujumu na ikulu kuwa pango la wezi, wanyang'anyi na kijiwe na majangili. Anakumbuka CCM ambayo binadamu wote walikuwa sawa na mtanzania alikuwa na farahi ya Utanzania wake sio dini, kabila, kanda, rangi nk.

Anaitunza ili awaambie watoto wake na wajukuu wake wawe makini sana na wote wenye tamaa ya mali ya wizi kwa mateso ya wanyonge. Anakumbuka nchi ilipolinda rasilima kwa manufaa ya wote. Anakumbuka utu, uwajibikaji na uzalendo wa wakati ule.

Leo akiingalia CCM anaona huruma na wote waliokumbatia humo ndani utaona wenye ukatili na wakiwa tayari kuona watanzania wote wanakufa ili wachache na familia zao wafaidi matunda ya wanyonge wengi. Anamwona Mkapa alivyojibinafsisha Mgodi wa kiwira kwa kodi zetu, Ana mwona Kikwete alivyoingia Ikulu kwa fedha harama za EPA, anamwona Lowasa anavyojisafisha kwa fedha chafu, na za damu za watanzania makanisani na misikini, anaona CCM iliyojaa rushwa na huwezi tena kuchaguliwa ndani ya CCM bila kununua kura. anaona masikitiko makubwa. Anaona viongozi wote wa CCM wanasukumwa na njaa badala na dhamira ya kweli ya kumkomboa mtanzania ndio maana Katibu mwenezi hana cha kueneza zaidi ya mipasho.

Ndio maana leo chama kilichokaa madarakani zaidi ya miaka 35 bado kina walipa ninyi kukipigia debe kila asubuhi bila kuwa na chakuonyesha zaidi ya uzushi.

Kumbu kumbu ni muhimu inakukupusha mateso na ulipopitia kama ulikosea au ulikuwa sawa.

Majanikv,
Ebu niambie faida ya Dr Slaa kuienzi kadi ya CCM.
 
Ukiana haya yote, CCM wanaweweseka, vijana wake wanapagawa, wanaropoka hovyo, wazee wake wanavuana ngua hadharani, utu unawatoka, povu linawajaa midomoni, matumbo yanawavimba Ujue mwisho wa CCM umefika na roho zinamtoka kila mmoja kwa style yake. Usiogope kaza mwendo ushindi umekaribia.
 
Pro-Chadema JF ndio watakaozimisha Chadema ni suala la muda...ndani ya Chadema kila mtu ananulika tatizo bei tu.

vipi sera ya kujivua magamba mmeachana nao sasa mnarukia chadema? mtabakia kama fisi anasubiri mkono wa binadamu udondoke, ndivo mnavosubiri chadema isambaratike!chadema inaongozwa na vichwa makini sio vichwa mbumbumb kama magamba! mkiwa wajannja wakati mpo madarakani boresheni magereza maana kuanzia 2016 patakuwa ndio makazi ya mafisadi wote na makuadi wao kama wewe!!
 
vipi sera ya kujivua magamba mmeachana nao sasa mnarukia chadema? mtabakia kama fisi anasubiri mkono wa binadamu udondoke, ndivo mnavosubiri chadema isambaratike!chadema inaongozwa na vichwa makini sio vichwa mbumbumb kama magamba! mkiwa wajannja wakati mpo madarakani boresheni magereza maana kuanzia 2016 patakuwa ndio makazi ya mafisadi wote na makuadi wao kama wewe!!

Mkuu Osokoni
Umempa za uso hatarudia tena.
 
Ila mwanangu Ben Saanane una hulka za kidikteta sana.

Mwangalie Kagame si mnamwita Dikteta? Ona alivyosambaratisha waasi wa kihutu na Intarahamwe.Na Chadema sasa inatakiwa kuchukua maamuzi ya kidikteta kusambaratisha virusi na vibaraka wa CCM waliojificha Chadema.
 
Back
Top Bottom