Teargass
JF-Expert Member
- Apr 23, 2018
- 26,960
- 27,950
We know your politicians with lies.Laggard, that 75% for Kenya is equivalent to percentage of villagers connected to power in Tanzania
MRADI WA UMEME VIJIJINI NAIBU WAZIRI WA NISHATI TAARIFA VYOMBO VYA HABARI TAARIFA YA HABARI TANZANIA MPYA+ UMEME VIJIJINI WAZIRI WA NISHATI WIZARA YA NISHATI
TANZANIA INAONGOZA AFRIKA UUNGANISHAJI UMEME VIJIJINI – DKT KALEMANI
February 14, 2020 Matokeo ChanyA+Comment(0)
- Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani, amebainisha kuwa kwa sasa, Tanzania inashika nafasi ya kwanza katika kuunganisha umeme vijijini ikiwa imefikia asilimia 74 ya vijiji vyote.
- Ameyasema hayo Februari 13 mwaka huu, wakati akizungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara, akiwa katika ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme.
- “Awali, Nigeria ndiyo ilikuwa ikiongoza ikiwa na asilimia 72 lakini tumeipita, tukiwa tumefikia zaidi ya asilimia 74 na hivyo tunaongoza Afrika kwa sasa,” amesema Waziri.
![]()
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nagaga, Kata ya Namalenga, wilayani Masasi, Mkoa wa Mtwara wakati wa hafla ya kuwasha rasmi umeme kijijini hapo, Februari 13, 2020.
- Akieleza zaidi, Dkt Kalemani amesema kuwa, jumla ya vijiji 9,001 nchini vimeshaunganishiwa umeme na kwamba, kati ya hivyo, vijiji 3,559 vimeunganishiwa umeme kupitia Mzunguko wa kwanza wa Awamu ya Tatu ya Mradi wa Umeme Vijijini (REA III-1), unaoendelea hivi sasa.
- Amesema, Mradi wa REA III-1 utakamilika Juni mwaka huu lakini serikali imekubaliana na wakandarasi wote wanaotekeleza mradi huo nchi nzima, kukamilisha kazi husika miezi miwili kabla, hivyo wanatarajiwa kukabidhi kazi kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), ifikapo Aprili 31, 2020.
- Kwa upande wa Wilaya ya Masasi pekee, Dkt Kalemani ameeleza kuwa serikali iliamua kurejea mpango-kazi na kufanya mabadiliko ambayo yaliwezesha kuongeza idadi ya vijiji vitakavyonufaika na mradi huo wilayani humo.
![]()
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (katikati), akimpongeza mmoja wa wakazi wa kijiji cha Matogolo, Kata ya Mbuyuni, wilayani Masasi, Mkoa wa Mtwara, baada ya kumuwashia umeme kwenye nyumba yake, Februari 13, 2020.
- “Niwe mkweli kuwa, katika mpango wa awali, ni vijiji vichache tu vya Masasi ndivyo vilikuwa vinufaike na mradi huu. Hii ni kwa sababu vijiji vingine viko katika Halmashauri za Miji na siyo Wilaya hivyo vilikuwa vinakosa sifa kwani vilikuwa na hadhi ya Mitaa na siyo vijiji.”
- Aliendelea kubainisha kuwa, kwa ushawishi na jitihada za Mbunge wa eneo hilo, Rashid Chuwachuwa, serikali iliamua kufanya marejeo na kuongeza idadi ya vijiji katika mpango wa REA, hususan vile vilivyo na taswira ya miji-vijiji, yaani ni mitaa lakini kiuhalisia maisha ya watu wake ni sawa na walioko vijijini.
- Akijibu hoja za wananchi wa vijiji vya Namikunda A na B, Nagaga na Matogolo kuhusu changamoto ya umeme kukatika mara kwa mara, Waziri, kwa nyakati tofauti alieleza kuwa tayari serikali imeshughulikia tatizo hilo kwa kuunganisha baadhi ya maeneo ya Mtwara katika gridi ya Taifa.
- Ameyataja maeneo hayo kuwa ni Tunduru, Masasi na Nanyumbu na kwamba yameunganishwa kupitia mradi wa umeme mkubwa wa Makambako – Songea (kilovoti 220).
![]()
Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Selemani Mzee, akiwasilisha kwa Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani, taarifa ya hali ya upatikanaji umeme wilayani humo. Waziri alikuwa katika ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme Februari 13, 2020.
- Katika ziara hiyo ambayo Waziri aliviwashia umeme vijiji vya Nagaga na Matogolo, ametoa hamasa kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kulipia ili waunganishiwe umeme.
- Aidha, ametoa onyo kali kwa mameneja wa TANESCO nchi nzima ambao wanalalamikiwa kutopokea malipo ya wananchi wanaohitaji huduma ya umeme kwa madai kuwa hakuna vifaa au sababu nyingine ya aina hiyo, huku akiweka wazi kuwa watakaobainika, watachukuliwa hatua kali.
- Waziri amewataka wananchi kutumia simu zao za mkononi kuwapiga picha na kuwarekodi mameneja wanaogoma kupokea malipo husika wakati umeme umeshafika kwenye maeneo yao na kuziwasilisha wizarani kama ushahidi ili wachukuliwe hatua za kinidhamu.
- “Kamwe hatutawavumilia mameneja wa aina hiyo kwa sababu siyo tu wanalikosesha shirika mapato lakini pia wanaichonganisha serikali na wananchi kwa kuchelewa kuwapatia huduma husika,” amesisitiza.
- Katika hatua nyingine, Dkt Kalemani amewasihi wananchi kuwa wavumilivu pale inapotokea huduma ya umeme imekatwa hususan katika kipindi hiki cha mvua huku akieleza kuwa hali hiyo inasababishwa na kufanya ukarabati wa miundombinu ambayo imekuwa ikiathiriwa na mvua.
- Hata hivyo, amewataka watendaji wa TANESCO kuhakikisha wanatoa taarifa kwa wananchi kwa wakati pindi wanapolazimika kukata umeme ikiwa ni pamoja na kufanya matengenezo hayo kwa muda mfupi ili kurejesha huduma ya umeme kwa wananchi.
- Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Selemani Mzee pamoja na Mbunge, Rashid Chuwachuwa, wamepongeza uwajibikaji wa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Magufuli, ambao umekuwa na matokeo chanya kwa wananchi.
- Katika ziara hiyo, Waziri aliambatana na viongozi na wataalamu mbalimbali wa Wizara, TANESCO na REA. Veronica Simba – Masasi
![]()
TANZANIA INAONGOZA AFRIKA UUNGANISHAJI UMEME VIJIJINI – DKT KALEMANI
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani, amebainisha kuwa kwa sasa, Tanzania inashika nafasi ya kwanza katika kuunganisha umeme vijijini ikiwa imefikia asilimia 74 ya vijiji vyote. Ameyasema hayo Feb…matokeochanya.co.tz
Sent using Jamii Forums mobile app