joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,111
- 46,621
Tatizo la Makonda anachanganya ulokole wake na uongozi wa nchi, huu ni mwanzo tu, lazima Marekani ionyeshe mfano hapa duniani kwanini watu wengi duniani wanapenda kwenda Marekani kuishi na kuzikimbia nchi zao, kwani wamarekani hawana dini?, lakini mbona wanavumiliana na kuheshimiana?Tatizo hapa sio kuhusu kukubali au kukataa Ushoga maana hakuna nchi yoyote katika dunia hii ambayo haina mtu hata mmoja anaye-identify kama LGBT. Tatizo ni njia inayotumiwa ku-enforce sheria tena sheria anazotengeneza DC. Fikiri mtu atume jina lako kwenye sms kumwambia makonda na team yake kuwa wewe ni shoga. Hebu fikiri tu maana mtu yoyote anaweza kukufanyia hivyo japokuwa wewe sio shoga na watu watakuja nyumbani kwako kukuchukua na utaenda kufanyiwa anal examinations ambazo sijui hata wanazifanyaje. Huu ni udhalilishaji wa kupuuzi sana. Ndio maana siku chache baada ya bashite kuanzisha crackdown yake serikali ilitoa tamko na kusema kuwa kitu anachokifanya sio NIA ya serikali KUU.
Sent using Jamii Forums mobile app