Tuusan, napenda sana kuona kwamba watu wameanza kujadili hapa mambo bila kuweka ushabiki.
Nchi inapounda miundo msingi raia wake hunufaika, mtu alisema hapa. Baabara mbaya maisha mabaya, sisi tumeamka kwa vifo vya wanafunzi 15 na walimu 4 kule Karatu mkoani Arusha, Mimi kama mwalimu nahusunika, ila hapa ukiangalia sio sana kosa la dereva, wala gari, barabara ndio mbovu, ingekuwa nzuri hawa watu wasingepoteza maisha, wangeenda kujenga uchumi, na wanafunzi baadae kuhitimu na kujenga nchi. Lakini ona sasa, Serikali lazima iwajibike