Battle: Dar es Salaam vs Nairobi

Walioruhusu bajaj na boda kuingia kati kati ya jiji la Dar ndiyo wameharibu mpango nzima wa kulifanya lionekane smart, plus ufinyu wa bara bara na ukosefu wa parking ni kituko kingine ambacho hatuwezi kujivunia kwamba tuna jiji safi na lililopangika vizuri. Ukipita mitaa ya kkoo watu utadhani ni mifugo ipo malishoni, full vurugu na harufu za maji taka kila sehemu
 
Kwanza karibu na ikulu unajengaje soko la samaki? Ni upuuzi kiasi gn aisee, shombo tupu la samaki, alafu hata ile station ya vivuko pale ferry ibomolewe, imeshaoza. At least Azam amejitahidi kujenga vzr, vyoo safi but the rest ni uchafu, na serikali kama imeshindwa huduma imuachie Azam lkn wawe wanapanga bei elekezi ili wananchi wasiumizwe.
 
Kwa miaka hiyo ilikuwa njema kipindi linaanza watu tulikuwa tunaenda Fanya utalii wa ndani buana, ni sasa hivi tu kwa sababu ya uongezeko la watu
Kwanza hata lile soko la samaki aliyeshauri lijengwe pale hakutumia akili yake sawasawa, halikupaswa kujengwa pale, lingejengwa upande wa pili ferry kule kwenye stand ya daladala za kwenda Geza ulole, mji mwema, kibada, tandika nk
 
Wangeweka chini mabasi yasingetosja , sasa hivi unaiona ndogo sababu kuna watu wanastend za vichochoroni ila wakisema kuwepo na marufuku ya kupakia vichochoroni hata sehem ya kuweka mabasi tutakosa
 
Yes. Na si mlisema Talanta is 100% owned by Chinese, tena mambo imechange ama?
Unajua maana ya PPP? sasa tuambie kama hiyo bond italipwa na GoK hiyo nayo bado ni PPP? huoni kuna walakini hapo? Dunia nzima inajua mradi ni wa PPP na pia tunatako kuona evidence kuwa hiyo bond ilikuwa issued when and where.
 
Kwa hivyo ukiwa na engine una gari, haya basi enda ununue engine uendeshe. 🤣 🤣
Kwani hayo magari mnayonunua si yanakuja na chassis engine na cabins. Kwani unafikiri hatuoni shape za Isuzu NQR mbele ya hayo makopo?
 
Kwani hayo magari mnayonunua si yanakuja na chassis engine na cabins. Kwani unafikiri hatuoni shape za Isuzu NQR mbele ya hayo makopo?
Hakuna gari inakuja kama imeunganishwa chassis, engine na cabins, hizo unataja ni parts za gari ambazo hua zinaletwa ili zitengenezwe kua gari kwa assembly plant ya Isuzu. Nyinyi ndio hua muna import magari zikiwa complete. Sisi hua tunatumiwa parts tunajijengea kwa assembly plants zetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…