Battle: Dar es Salaam vs Nairobi

Target nyingi za serikali ni makisio tu.

Mfano, mambo ya mapato yanatokana na sheria za bunge au baraza la madiwani.

Na sheria nyingine wanazotunga, field hazitekelezeki, mfano sheria ya kodi za mabango.

Hapo huwezi kumlaumu mtu wa field kwa utekelezaji.

Lakini pia wafanyakazi wengi wa serikali, ukiacha mishahara yao, hawawezeshwi kufanya kazi.

Mfano: Zahanati ina daktari wawili, ina wagonjwa kibao. Huwezi kutegemea mtu hiyo huyo akeshe hapo siku 2, bila motisha yoyote.

Na mostly mtu huyo hiyo serikali haina nyumba amepanga, anadaiwa kodi ya nyumba, baada y kumtoa kwao Kigoma ukampa kazi Kilimanjaro.
 
Bado inawezekana ukimpa target lazima hata mkuu wake atapewa target kwa hiyo uwezeshwaji utapatina.
KInachotoekea sasa hivi mabosi hawabanwi na malengo, kwa hiyo hata wanabaki wanafikiria kuchuma badala ya kuwa creative.
Chukulia mfano tu inakuwaje hospitali za serikali pamoja na kuwa na wateja wengi ila zinaendeshwa kwa hasara?
Ili ziweze fanya KAZI Ondo ruzuku wabane kwenye mapato ma moi, mapato lazima yatapatikana maana itabidi watafute hata watu wa kujitolea ili walau kukuza kipato.
Hospitali zote kama za rufaa zilitakiwa ziendeshwe kwa mfumo wa kama halmashauri ila minus madiwani .
 
Kodi ya mabango inawezekana na ni rahisi tu wala haihitaji manpower kubwa sana kivile.
Maana mkishafanya sensa ya mabango inabaki ni kusukuma control number kwa wahusika na kuondoa kwa wale wasumbufu tu.
Labda Kodi ya majengo ndo mtihani Ile ingebaki kwenye umeme tu
 
Changamoto ni uwepo wa kodi na regulatory fees nyingi zinazo-target mtu mmoja.

Issue unaweza kutoa hizo control namba na watu wakafunga biashara, ukabaki unadaiwa wewe, maana zitaonekana kwa CAG.

Pili, wabongo wataondoa tu hayo mabango kuliko kulipia.
 
Bado inawezekana ukimpa target lazima hata mkuu wake atapewa target kwa hiyo uwezeshwaji utapatina.
Siku ukifika field kwenye hizi kazi ndio utajua shughuli zake.
KInachotoekea sasa hivi mabosi hawabanwi na malengo, kwa hiyo hata wanabaki wanafikiria kuchuma badala ya kuwa creative.
Ukimbana boss anafanya nini?

Maana hafiki huko field
Chukulia mfano tu inakuwaje hospitali za serikali pamoja na kuwa na wateja wengi ila zinaendeshwa kwa hasara?
Kwa mujibu wa sera ya afya ya 2007.

  • Wajawazito (Bure)
  • Watoto chini ya miaka 5 (Bure)
  • Chanjo (Bure)
  • Wazee zaidi ya miaka 60 (bure)

Na hao ndio wengi wanaoenda huko Hospitali.

Hizo pesa unategemea ni nani atalipa??
Ili ziweze fanya KAZI Ondo ruzuku wabane kwenye mapato ma moi, mapato lazima yatapatikana maana itabidi watafute hata watu wa kujitolea ili walau kukuza kipato.
Uondoe ruzuku gani??
Hospitali zote kama za rufaa zilitakiwa ziendeshwe kwa mfumo wa kama halmashauri ila minus madiwani .
Hata sasa hospitali zote na zahanati ziko kwa mfumo huo.
 
LAkin Lile ni tangazo la biashara ni sawa na kupeleka tangazo lako redion ambapo utalipie kwa siku au mwezi kwa gharama kubwa .
Kwa bei ya 10,000 kwa sq/ft mbona sip gharama sana zaid ya kwa redio.
MAkampuni mengi yanalipa na Ni chanzo kikubwa cha mapato.
Mfano Kuna sehemu niliona Airtel kalipia almost 8mil kwa kihalmashauri ambacho hata hakina mabango mengi na bado walikuwa wanaona wamepigwa
 
Ni biashara ngapi zinatangaza huko redioni au kwenye TV?

Mabango yenyewe ya Manispaa huko barabarani huwa yako TUPU.

Nakumbuka mpaka Azam wamewahi kubandua matangazo kwenye magari yao, unafikiri hawawezi kulipia?
 
Nimefanya KAZI hii sana nikiwa kama afisa mapato Tena kwa sehemu ambayo sikufikiria kabisa kama ningeweza fanikiwa ila nilipata bos mwelewa alikuwa ananiwezesha mpaka pesa ya watu wakunifanyia KAZI badala ya kutumia watendaji wa vijiji
Siku ukowa field kwenye hizi kazi ndio utajua shighuli zake.

Ukimbana boss anafanya nini?
Ukimbana letsay bos kama mkurugenzi kuwa kipimo chake ni mapato na ukawapa target lazima watajenga ukaribu na watu wamapato , hivyo lazima uwezeshwaji upo.
Mfano tu mtu kama mchengerwa Kuna siku unashangaa simu hiyo anaulizia kwanini hela ya pos haijapelekwa benki.
Pitia halmashauri yoyote uijuayo uone watu wanavyoziogopa hela za pos sasa hivi na hata mapato yalivyoongezeka.

Maana hafiki huko field

Kwa mujibu wa sera ya afya ya 2007.

  • Wajawazito (Bure)
  • Watoto chini ya miaka 5 (Bure)
  • Chanjo (Bure)
  • Wazee zaidi ya miaka 60 (bure)
Ni Bure sawa lakini Huwa kuna record zake, sasa hivi watu wengi wenye hela wanakimbilia private wakati walipaswa wavutiwe na huduma nzuri kwa hospitali za serikali. Ukienda sehem kama dodoma rufaa na benjamini mkapa hospital, idadi ya wagonjwa wanaofuata huduma benjamini ni kubwa sana wakati dodoma rufaa inanafasi ya kujitanua na kuwabeba hao wagonjwa
Na hao ndio wengi wanaoemda huko Hospitali.

Hizo pesa unategemea ni nani atalipa??

Uondoe ruzuku gani??
Zahanati ziko kwa mfumo huo lakini laiti tukizipa nafasi watu waziendeshe kwa ufanisi kuliko sasa hivi, Zina nafasi ya kuingiza kipato kikubwa sana.
Zahanati nyingi hasa za vijijini bado zinatumia vibuntu kukusanyia mapato , unafikiri tutapata hela hapo
Hata sasa hospitali zote na zahanati ziko kwa mfumo huo.
 
Ni biashara ngapi zinatangaza huko redioni au kwenye TV?

Mabango yenyewe ya Manispaa huwa yako TUPU.

Nakumbuka mpaka Azam wamewahi kubandua matangazo kwenye magari yao, unafikiri hawawezi kulipia?
Ni Bora walipie wachache kuliko kuacha uhuru wa manyani , itakuwa ni vurugu labda gharama ipunguzwe
 
Nadhani regulation tukizisimamia vyema zinaweza kuwa manufaa kwetu kuliko hasara
 
Ni Bora walipie wachache kuliko kuacha uhuru wa manyani , itakuwa ni vurugu labda gharama ipunguzwe
Sijajua unaposema uhuru wa manyani unamaanisha nini?

Maana kodi ndio DAMU ya serikali.

Na ili mfanyabiashara alipe kodi, ni lazima na apate wateja, na ili apate wateja anatakiwa ajitangaze.

Sasa ukibana kila anapojitangaza maana yake gharama za kufanya biashara zinakuwa kubwa.

Hiyo biashara haitapiga hatua hata siku moja.

Au watu wataanza kufanya biashara za BLACK MARKET.

Hata kidogo ambacho serikali ingeweza kupata HAIPATI.
 
Sometimes regulation zinasaidia , vitu unavyooana haviwezekani Leo bado vinawezekana.
tukiweka Sheria za targets ndo kiwe kipimo cha ufanyakazi wako na kukawa Kuna kipercent inaambulia lazima mabadiliko yataonekna.
Tumetoka mbali sana ambapo watu walikuwa na uwezo wa kupokea hela ya barabara wakapita nayo nzima bila hata kuacha senti
 
Nimefanya KAZI hii sana nikiwa kama afisa mapato Tena kwa sehemu ambayo sikufikiria kabisa kama ningeweza fanikiwa ila nilipata bos mwelewa alikuwa ananiwezesha mpaka pesa ya watu wakunifanyia KAZI badala ya kutumia watendaji wa vijiji
Maana yake wewe ulikuwa unafanya kazi field mbali, na unatumia nguvu.

Watendaji wa vijiji lazima wawe diplomatic kwasababu wanaishi na hao watu.
Ukimbana letsay bos kama mkurugenzi kuwa kipimo chake ni mapato na ukawapa target lazima watajenga ukaribu na watu wamapato , hivyo lazima uwezeshwaji upo.
Ofisi za mapato field wilayani. Ina lazima ofisi hizo zipewe posho, gari na mafuta kwasababu zinaenda field.

Ila nakupa mfano.
Una biashara ya Nyama au Vipodozi👇

Halmashauri inataka:
  • Leseni
  • Service levy
  • Ushuru wa taka
  • Ushuru wa bango.
  • Kama unanunua mnyama unatembeza unapaswa kulipa kibali cha movement
  • Ushuru wa machinjio

FIRE
- Wanataka fees ya ukaguzi na ununue fire equipments

TBS
  • Wanataka usajili wa premises kwa 50,000 -100,000 kwa mwaka.
  • Bodi ya nyama wanataka fees kwa mwaka

Hapa, kila taasisi inakuja kwa wakati wake, bila kujali jana kuna taasisi nyingine ilipita kwako.

Bado baba lao TRA.

Biashara haitaweza kukua hata siku moja. Na possibility ya kufa kama huho mtu analipa kila kitu ni rahisi sana.
Mfano tu mtu kama mchengerwa Kuna siku unashangaa simu hiyo anaulizia kwanini ya posi haijapelekwa benki.
Pitia halmashauri yoyote uijuayo uone watu wanavyoziogopa hela za pos sasa hivi na hata mapato yalivyoongezeka.
Huwezi kula pesa za POS lazima zipote kwenye MFUMO.
Ni Bure sawa lakini Huwa kuna record zake, sasa hivi watu wengi wenye hela wanakimbilia private wakati walipaswa wavutiwe na huduma nzuri kwa hospitali za serikali.
Huduma nzuri zinatokana na uwekezaji.

Huduma afya za serikali hazisaidii Vituo kununua vifaa bora vingi, mpaka vipelekwe na serikali kuu.

Na pia huko private, watu wanaenda kulipa ila wakikosa pesa ndio wanaenda serikalini.
Ukienda sehem kama dodoma rufaa na benjamini mkapa hospital, idadi ya wagonjwa wanaofuata huduma benjamini ni kubwa sana wakati dodoma rufaa inanafasi ya kujitanua na kuwabeba hao wagonjwa
Hilo ni sawa.

Na kwakuwa Wizara ya afya ndio msimamizi, wanaweza kuboresha.

Ingawa Benjamin Mkapa inasimamiwa na Mkapa Foundation.
Shida siyo kuziendesha.

Shida ni HUDUMA za bure.

Hata ukimpa mtu mwingine, bila mapato hawezi kufanya maajabu.
 
Sijajua unaposema uhuru wa manyani unamaanisha nini?
Uhuru wa manyani ni kuwa ,ukiondoa ushuru wa mabango kesho Kila mtu atataka kuweka bango mwisho wa siku itakuwa ni takataka na mapato hayatapatikan kama ilivyokusudiwa
Maana kodi ndio DAMU ya serikali.
Ushuru wa mabango ni ngazi serikali za mitaa, kumbuka ukiondoa Kodi za tra , halmashauri inapata service levy na leseni ya biashara tuu.
Leseni ni mara moja kwa mwaka
Service levy ni 0.3% ya mauzo .
Na kiuhalisia ni wachache sana wanaolipia hii Kodi ,
Kumbuka halmashauri ndo Kila kitu kwa ngazi ya wilaya. Na kiukweli halmashauri nyingi nje ya zile za mijini hazipati mapato kwenye biashara sanasana mazao. Hakuna effect yoyote kwenye ushukaji wa kipato bali ili tuongeze ni kupunguza gharama au kuwe na bei fixed kwa mwaka
Na ili mfanyabiashara alipe kodi, ni lazima na apate wateja, na ili apate wateja anatakiwa ajitangaze.
Anaweza akatumia hata mdomo kujitangaza , mabango mengine yanaweza kuwa kero kwa watu kwahiyo hapo anakuwa amelipia na gharama ya kero kwa majirani
Sasa ukibana kila anapojitangaza maana yake gharama za kufanya biashara zinakuwa kubwa.

Hiyo biashara haitapiga hatua hata siku moja.

Au watu wataanza kufanya biashara za BLACK MARKET.
Hatapata wateja kama pale atakapokuwa ameweka bango.
Mfano wewe unalodge yako usipoweka bango nani atajua tunauza vyumba , solution ni kuwepo na bei fixed kwenye mabango au ipunguzwe atleast 2000 kwa sq/ft
Hata kidogo ambacho serikali ingeweza kupata HAIPATI.
 
Uhuru wa manyani ni kuwa ,ukiondoa ushuru wa mabango kesho Kila mtu atataka kuweka bango mwisho wa siku itakuwa ni takataka na mapato hayatapatikan kama ilivyokusudiwa
Lazima lengo liwe wazi.

Serikali inataka biashara, ili hizo biashara zilipe mapato.

Sasa mtu akifunga hiyo biashara serikali inanufaika nini?
👇👇
Anaweza akatumia hata mdomo kujitangaza , mabango mengine yanaweza kuwa kero kwa watu kwahiyo hapo anakuwa amelipia na gharama ya kero kwa majirani
Hiyo vita yote ya nini?

Mtu awe huru afanye biashara, na serikali ipate chake, maisha yaendelee.


Hatapata wateja kama pale atakapokuwa ameweka bango.
Asipopata wateja serikali inapata faida gani?
Mfano wewe unalodge yako usipoweka bango nani atajua tunauza vyumba , solution ni kuwepo na bei fixed kwenye mabango au ipunguzwe atleast 2000 kwa sq/ft
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…