instanbul
JF-Expert Member
- Jun 26, 2016
- 12,544
- 19,491
Labda watu watwambie kama wana nchi yao nyingine tofauti na Tanzania.Tukisema tunaonekana tuna mapenzi na Magufuli. Wakati tunamaanisha ile style ya governing kwenye miradi.
Yaani vitu vinajiendea, watumishi wanajua kuanzisha matukio ya "Mama" basi.
Hata kama kusifiwa kulianzia kwa Magufuli ila alikua anawala vichwa wazi wazi wakishindwa kazi or wakienda kinyume na maagizo so wao ilikua sifia yao ipo kwenye kutelekeza miradi sio "Samia Run, samia boxing, samia dance, samia clinic"
Makonda aliyekua untouchable alipigwa chini kwa kukimbilia kuomba fomu na wamekatazwa either chagua kimoja utumishi or kula.
Kangi Lugola alikula kichwa.
Mwanri alikula kichwa same situation na Makonda.
TANESCO na PORT walikua hawana amani kabisa, Wizara ya Ujenzi nayo ilikua haina amani ghafla huyu hapa.
Plus watumishi wengi sasa waliona kusifia hakulipi zaidi ya utendaji ndio wakaacha.
Now ni kutengeneza mabango kunalipa, mtu anaachwa kisa Team Samia na unaleta wajinga Kina Dotto Magari etc kwenye mambo serious
Usishangae kusikia Keshokutwa kuna Uwekezaji kutoka Dubai kwenye reli ambayo ilitaka tu uangalizi wa karibu na ukali inaenda fresh or BRT.
Leaders of nowdays wanaifanya Tz kama sio kwao vile. No nationalism at all.
Hiv mtu unafurahia nini kununua majumba na magari wakati ukienda hata kwenye kampeni za mama city Centre unakanyaga kwenye mavumbi?
Unaweka macamera sijui CCTV kuangalia watu wanaokanyaga kwenye mavumbi, Barabara hazina sidewalks na manyaya ya umeme yamezagaa...hawajui hata hayo manyaya yanaweza kublock view?
Ule mradi wa SGR tunnel pale chang'ombe mbona uko slow sana. Yaani mimi ningekuww Rais...ile sehemu ilipaswa iwe imekamilika, wako kwenye testing ya treni za mizigo, kule Dodoma kuna bandari kavu, je kuna hata crane moja kule ya kushusha mizigo iliyoandaliwa?
Ni nini mtu unafurahia kuwa kiongozi wa nchi halafu no achievement yoyote ya kimaendeleo unasema hii nimelounch na imebadili lifestyle ya watz.
Yaani kimsingi viongozi wetu wanatufanya watz wote tuonekane incompetent