Battle: Dar es Salaam vs Nairobi

Mm nimekuuliza maoni yako nashangaa una panic tena unaanza kusema nina unafki wala sijauliza habari juu ya msimamo wa ufaransa ila nilichouliza maoni yako tu

🤣🤣🤣🤣 yani bro unapanic sana alaf hutakiwi kua hvo, kwani nchi ngapi zimepinduliwa na wala sio ajabu hata oman mtoto alimpindua baba yake alipoona mambo hayaendi sawa na akaja akaweka sawa kila kitu ni vitu vya kawaida na walioshindikiza nchi kupinduliwa ni wananchi so ni haki yao

Na ukiona nchi wananchi wanataka mapinduzi basi ujue kuna manyanyaso makubwa kama sio kwa viongozi wao basi kwa watu nyuma ya pazia wanaoshindikiza hayo manyanyaso
 
Vipi unauliza maoni yangu kuhusu Ufarasa na usiulize kuhusu ECOWAS ambao wametishia kupeleka jeshi kwenda kumrudisha rais aliyepinduliwa?. Mkuu, mbona ulisema USA ilikosea kwa kuzionya nchi rafiki zinazoshirikiana na maadui zake, lakini husemi lolote kwa nchi za Afrika ambazo zimetishia kupeleka majeshi kwa nguvu Niger kupingana na wananchi wa Niger?, kwani Niger sio nchi huru?, vipi hizi nchi za Afrika zinaingilia uhuru wa Niger na wewe upo kimya badala yake unaishitumu France?.

Mkuu wewe ni mnafiki Sana na unachuki za kupitiliza kwa nchi za Magharibi, katika dini yetu ya kiislamu, watu wanafiki Kama ninyi kamwe hamuwezi kuingia peponi[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sasa unadhani kwasababu Oman mtoto alimpindua baba yake, kwako hiyo ndio "role model" yako ya kuhalalisha mapinduzi?. Waarabu na waafrika ni miongoni mwa "Primitive societies" zilizobakia katika dunia ya Leo, kamwe hupaswi kutumia mifano ya nchi hizo.

Hebu taja ni nchi gani iliyoendelea (developed country), ambayo hadi Leo huu ujinga wa mapinduzi ya Kijeshi unaendelea.

Kwahiyo unadhani haya mapinduzi yanatokana na manyanyaso na taabu wanazopata raia kutokana na uongozi mbaya, jiulize maswali yafuatayo.
1)Ni raia wa Afrika pekee ndio wanaonyanyasika tu, kwanini huko duniani kwengine hawanyanyasiki?
2)Kwanini ni nchi za" Sahel" na nchi zenye asili ya uislamu kwa wingi ndio zenye fujo, mapinduzi na vita visivyokwisha hapa Afrika na Dunia nzima

Mkuu, tumia ubongo wako kwa kuchakata kwa undani Yale unayoyasikia, usiwe mtumwa wa fikra na itikadi za kidini au rangi. Badilika mkuu.
 
Mbona umepanic sana bro 🤣🤣🤣 nishakua mnafki tena mm, hebu rudia swali nililokuuliza yani sikutegemea mapovu kias hicho nilichokuuliza ni tofaut kabisa na unachonijibu

Hakuna nchi ilioingilia uhuru wa niger hata hao ecowas wametamka kwa maneno na sio vitendo na kutamka kwa maneno ni kwa shindikizo la ufaransa baada kusema ataanzisha vita ufaransa kwann kwann ufaransa katamka wazi kua ataanzisha vita niger ???

Mapinduzi yapo kwenye maisha na bahat uzuri wa mapinduzi ya niger niyakutoka kwa wananchi moja kwa moja kwamba wananchi wamechoshwa wameona wapindue sasa shida iko wapi??🤣🤣

Shida yako mkuu unapanic sana alaf unakwenda sana nje ya mada alaf unapenda sana kudhania kitu kabla ya kuthibitisha 😅😅😅😅
 
hizi nchi zote za kiislamu zenye vita chanzo chake ni nato ikiongozwa na huyo muonevu wa dunia ukichunguza kwa makini sana leo itazame libya au iraq au yemen au palestine, ww hujiulizi kwann dunia haiongelei uonevu wa israel kwa palestine, sadam husein alipotaka kuwasaidia wakamzushia ana silaha za maangamizi wakamvamia na kusabaratisha nchi leo hii unaona iraq inatawaliwa? leo unafkiri bila putin kuweka nguvu syria unafkiri ingekua kwenye hali gani??
 
naona na guinea nae kajiunga dhidi ya ecowas 😄 😄 😄
 
Hata USA walitamka tu kwa maneno kuwatishia nchi rafiki, Kama walivyotamka ECOWAS lakini wewe ukakasirika kwa sababu USA ilitamka kutishia, ila ECOWAS walivyotishia unaona sio tatizo ila Ufarasa ni tatizo kwako.

Ukweli ni wazi kwamba una uchuki kwa nchi za Magharibi, na sababu kubwa ni kwamba una chembechembe za udini na uarabu, unataka kutushirikisha ugomvi wa wazungu na waarabu, tumekustukia huko hatukubali.
 
ecowas wanaongea huku nyuma yao kuna hao hao wenye maslahi na africa na ww unawajua na mm nakwambia bro ecowas hawawez kufanya kitu hvi unajua ecowas ni nchi ngapi?? 😆 😆 😆 kuna nchi zilishajitoa ecowas hilo ulijue

kingine unarudia tena ya USA kutoa vitisho kwa nchi za africa zilizoenda urusi so kuhudhuria mkutano hahaha vitisho vya nn kwa nchi huru bro sioni matiki yoyote

mm siongelei udini au uarabu naongelea haki sehem inatakiwa kutendeka nothing else ila ww unanidhania tofaut kabisa na hapa mm sikulazmishi uamini navoamini lakini najaribu kukueleza haki inavopaswa kua na sio vinginevo

but tuko hapa wote tutashuhudia mengi sana haya ni machache sana 🤣🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…