Battle: Dar es Salaam vs Nairobi

Kwa kiasi kikubwa migogoro ya nchi hiyo inasababishwa zaidi na wakubwa, sababu ikiwa ni mafuta, madini na siasa za kimataifa. Hilo eneo la bahari ya sham ni la kimkakati (trade route), teyari kuna kambi za majeshi ya Marekani na China. Sasa maajuzi warusi walikubaliana na serikali ya Sudan kujenga kambi ya jeshi hapo, ndo unaona RSF wakileta chokochoko.
 
Mkuu sikubaliani na wewe, ni mgogoro wao wenyewe na sababu kubwa ni ubaguzi na ukabila. Ethiopia wanapigana kwa sababu ya ukabila, Somalia ni mambo ya ubaguzi wa Koo na Koo.

Mkuu Sudan ni nchi yenye ubaguzi mkubwa Sana kati ya waarabu na watu weusi, watu weusi wanadharauliwa Sana Sudan, yaani Sana Sana Sana na zaidi ya Sana.

Kenya wanabaguana Sana, kwamba kabila mbili au tatu ndizo zenye haki ya kuwa rais wa Kenya, chokochoko zinaanza taratibu, baada ya miaka 5 Kenya lazima watapigana, na bado tutasingizia mataifa makubwa.
 
Nilipokujibu mwanzo nilitumia maneno haya, "kwa kiasi kikubwa". Ni kweli matatizo ya ubaguzi wa kikabila, kiukoo, rangi na kidini yamekuwepo maeneo hayo toka enzi na enzi ila kwa sasa yanakuzwa zaidi kwa maslahi ya watu wa nje.

Wachina wana ambitions zao za belt and road hapo shamu, warusi nao wameanza kujenga base yao hapo, sasa nchi za magharibi hazitaki hawa jamaa wawe na ushawishi hapo. Ndiyo maana serikali ya Sudan ilipowakaribisha tuu warusi ikaletewa kivumbi na kikosi cha RSF.

Hivi unafikiri warusi wakiwa na base yao hapo na wakaaamua kuzuia meli za mafuta kupita, kuna atakaye pita? Unadhani ulaya kitakalika kwa kukosa mafuta? Haya mambo ni makubwa kuliko unavyodhani kaka.
 
Mbona Warusi wako Sudan siku nyingi?
 
Kwahiyo Kule Darfur ambako hao RSF(Janjawed) walipokua wanaua watu weusi walitumwa na mataifa makubwa?, au kulikua na njia ya kupitisha mafuta?. South Sudan walivyopigana kutaka kujitenga pia kulikua na mkono wa mataifa makubwa?, Somalia wanapigana tangu 1991, au Oromo wanavyopigana kutaka kujitenga pia ni mataifa makubwa?, vita vya Tigrey na Serikali ya Ethiopia pia ni mataifa makubwa, huko DRC zaidi ya vikundi 200 vya waasi, nako ni mataifa makubwa, Cameroon nchi Yao imegawanyika pande mbili, nako huko Je?. Mkuu Africa bado Sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…