Lengo langu ilikuwa kufikisha ujumbe kwamba SGR italeta ushindani kwake, sema kosa langu nimeanzia katikati na kusikutaja madhaifu yake.
Mabasi yao ni mazuri, madereva wana kauli nzuri ila sasa kuna sehemu wana mapungufu inabidi wayarekebishe ili waende sawa na wengine.
Ni kama route ndefu hajaizoea. Dar lux tulimshauri lakini hakusikia i sasa hivi yuko wapi?
Ebu fikiria mnapanda basi Urafiki mkifika Mbezi mnafaulishwa ili mpande basi lingine la kwenda Bukoba au Musoma, kwenye kupanda hakuna anayejali mizigo ya abiria, ni usumbufu tu.
Mnaanza safari mkifika Morogoro mnapelekwa gereji kwao kujaza mafuta, hapo hapo nje kuna magenge mnaambiwa mnununue chochote.
Pamekaa kiswahili sana,vitu ni local,wakimaliza kujaza mnaingia ndani ya basi safari inaanza hao mpaka Kahama wanaamua kulala hapo hapo mpaka kesho alfajiri ndio mnaanza safari.
Njiani sasa basi ni kama daladala kuna abiria wanapanda na kuku, kuanzia Kahama,Nyakanazi, Biharamulo, Muleba kote huko ni kusanya kusanya. Mpaka mfike saa 7 mchana au saa 8 kasoro. Kumbuka ambao hawakulala Kahama wanafika saa 12 alfajiri.
Sasa hata kama wewe unampenda Abood karaha hizi utazivumilia?