Battle: Dar es Salaam vs Nairobi

Battle: Dar es Salaam vs Nairobi

View attachment 2362056
Kuna mtu ameona hii picha adi amekojoa bila kukojoleshwa hahahaaaaa
Hii sehemu ya Makumbusho tumeijua siku mingi sana, hatubabaiki, Dar tunaijua nje na ndani kilaza.., ngoja miaka 25 mbele kisha uje tujadiliane 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂
1663675697495.png

1663675809196.png

1663675360604.jpeg


Nairobi outside CBD..,
1663677883615.png

1663677850002.png

1663677927542.png

1663677820702.png

1663677780849.png

1663677796541.png
 
Unapost road section 🤣🤣 while barabara ya masaki ni 5 km long .. au ulikua unajaribu kulinganisha hizo michoro .? Hakuna estate yenye barabara kali kuliko Masaki EA yote .. huna budi kuridhika na ukweli mzee
And the resident madman has come back.
 
TUPITIE HII KIDOGO

Nimeona maoni ya watu wengi Tanzania, Kenya na Afrika kwa ujumla wakikwazika na kukereka kitendo cha marais na viongozi kadhaa wa kidunia hasa Afrika kusafirishwa kwa mabus kwenda eneo la Westminster Abbey ilikofanyika ibada ya mazishi ya Malkia Elizabeth wa pili.

Naomba nitoe maoni na shule kidogo kuhusu mambo haya ya kiitifaki kidunia. Kwa msingi wa itifaki ya kibepari ya kiingereza. Mwaliko wa kuhudhuria Mazishi kigezo cha kwanza katika itifaki kiilizingatia kitu kiitwacho "First Countries". Na ifahamike na kueleweka vizuri, nchi za dunia ya kwanza "First Countries" duniani ni mbili tu. Hizi nchi za Marekani na Urusi huwa zinaitwa "Superioty". Ama tunaita Magharibi na Mashariki, Upande wa Kushoto na Upande wa kulia. Ujamaa na Ubepari. Yaani Marekani na Urusi. Sasa kwakuwa Urusi anaugomvi mkubwa na Marekani kutokana na kuzidiana ujanja na kuharibiana maslahi kule Ukraine baada ya Urusi kuanzisha Oparesheni yake Ukraine, Hivyo katika tukio la msiba huu, First Country kabaki mmoja tu ambae ni MAREKANI.

Ifahamike na kueleweka kuwa Upande wa Marekani kuna NATO na wafuasi wengine ambao hawa mwelekeo wao unategemea kiwango cha njaa tu tumboni, na Upande wa Urusi kuna Uchina na BRICS na huku kuna rundo la wafuasi ambao mwelekeo wake unategemea zaidi kiwango cha uumaji wa njaa. Nchi ambazo ni wafuasi wa upande wa Marekani na nchi nyingine ambazo ni wafuasi wa Urusi zinaitwa Infirioty countries.

Sasa ikiwa kigezo cha kwanza cha kiitifaki kilikuwa ni nchi za dunia ya kwanza, na hapo yuko Marekani pekee, basi bila shaka huyu ndie angeingia na msafara wake moja kwa moja hadi Westminster Abbey. Na ndivyo ilivyotokea. Ni Rais wa Marekani Joe Biden na mkewe tu ndio wameingia na msafara wao binafsi wa gari maalumu (armoured vehicle, nicknamed The Beast)

Niliwahi kueleza msingi wa Superioty na Infirioty siku nilipokuwa najadili kuhusu Urusi kuendesha oparesheni yeke nchini Ukraine ilipokuja hoja ya Sovereing State, nimelieleza hili hata kwenye kitabu changu kipya kijacho cha Oparesheni Moscow - Ukraine. Nilieleza kwamba Dunia hutazamwa katika mapande mawili, Superioty na Infirioty. Dunia haijawahi kuwa tambarare kama mnavyojifariji.

Nimamaanisha kwamba, duniani kuna nchi kiongozi na nchi ongozwa. Hakuna sovereign State duniani, bali kuna Super power state with parmanent interest. Uhuru wa nchi za dunia ya tatu (sovereign state) ni tofauti sana na watu wengi wanavyotafsiri, mamlaka kamili ya nchi yoyote yanategemea na msimamo wa dunia ya nchi za kwanza, Tunaweza kusema Uhuru wa Tanzania unamipaka na mipaka hiyo isivuke maslahi ya Ubepari au Ujamaa, msimamo wa hili kwamba dunia ina upande wa walala hoi na wa lala heri.

Hawa wenye heri agenda yao ni moja, vita vikitokea ni mgongano tu wa maslahi ya hawa wa lala heri. Maslahi hapa ni yale USA iliyoyatafuta Iraq, Afghanistan, Kuwait, Cuba, Vietnam nk ndio maslahi hayo hayo yanayolindwa na Urusi kule Georgia, Chechnia, Ukraine, Cremia, Donetsk, Luhansk, na kwingine kutakaofuata. Mfano hai Vita vya Uganda tulishinda kwasababu Wajamaa (Urusi) walikuwa upande wetu, na palipo na mjamaa, mbepari asingeweka pua. Misaada ya kijeshi mingi ilitoka Ujamaa pamoja na danganyatoto ya kutofungamana na Ujamaa au Ubepari.

Hawa Super power state with parmanent interest (USA +NATO, na Russia +BRICS) Uhuru wao ni "parmanent" yaani ni sovereign state halisi, uhuru wao hauhojiwi wala kuingiliwa na yeyote. Lakini wao wanaithibati ya kuingilia popote ambapo maslahi yao yanaguswa hasa katika nyanja za Usalama wao. Hivyo ndivyo dunia inavyozunguka, upende au usipende, ulie ama unune, ukikomaa chagua mji. Dunia ni ya Superioty vs Infirioty full stop. Sasa sisi Dunia ya Infirioty tunaopandishwa mabus, tunawajibu wa kuchagua upande, uwe kushoto ama kulia,

Tukirejea huko Westminster Abbey, utaratibu wa viongozi kufika ukumbini ilikuwa katika mtindo wa kipekee na wa uangalifu sana.
Wakuu wa nchi, mawaziri wakuu na mabalozi kutoka kote ulimwenguni walisafiri hadi Hospitali ya Royal Chelsea, kabla ya kupanda mabasi kwa safari ya maili mbili kuelekea ibada ya saa tano asubuhi (11:00am) huko Westminster Abbey.

Viongozi wa Afrika walikuwa miongoni mwa marais na mawaziri wakuu wa kwanza kuwasili eneo la Hospitali ya Royal Chelsea na kupanda bus la pamoja, wakiwa sambamba na kiongozi wa kijeshi wa Sudan Abdel Fattah al-Burhan majira ya saa moja na nusu hivi asubuhi (7:30 asubuh).

Msafara uliofuata ni wa wajumbe kutoka Malawi na Nigeria wakitumia gari moja kwa pamoja. Marais na mawaziri wakuu zaidi walifuata katika msururu wa magari yenye usalama wa hali ya juu ya kifame, akiwemo Taoiseach Micheal Martin wa Ireland na Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen. Hawa wote walitumia magari madogo "Range".

Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier alipanda gari la kifahari la BMW lenye giza nene. Huyu alikuwa katika msafara wa pekee yake. Muda mfupi baadaye, rais wa Italia Sergio Mattarella aliwasili akitumia gari aina ya Maserati ya ubalozi wake,

Kisha mfalme Philippe wa Ubelgiji akiwasili akiwa amevalia sare ya sherehe yenye kola ya dhahabu akitumia gari maalumu ya kifalme, huku Mfalme Felipe na Malkia Letizia wa Uhispania wakipungia mkono umati huo mdogo katika msafara wenye gari dogo la kifalme..

Mshikemshike ulitokea katika msafara wa Gari lililombeba kiongozi wa Qatar Bwana Emir, gari lake pekee ndilo lililopeperusha bendera yake ya taifa kutoka kwenye boneti yake, lililazimika kusubiri mbele ya kamera za televisheni kwa dakika 20 kwenye kituo cha ukaguzi huku maafisa wa polisi wakizungumza huku na huko kwenye redio zao wakitaka kuzua msafara huo. Hatimaye, iliruhusiwa kuingia.

Makamu wa rais wa Uchina Wang Qishan, aliwasili katika kituo cha ukaguzi kwa mwendo wa kasi katika msafara wa magari kadhaa ya kifahara madogo.Tofauti na viongozi wenzake, Bw Wang hata hakulazimika kusimama ili kukaguliwa alipitiliza na msafara wake hadi Westminster Abbey

Rais wa Marekani Joe Biden alikuwa wa mwisho kuwasili, alisafiri kando ya misafara ya viongozi wengine kwa gari maalumu la kivita, lililopewa jina la utani The Beast, lililokuwa limezuiliwa kwa muda kwenye barabara ya kuelekea Abbey ili kupisha viongozi wengine watangulie kwanza, msafara huo wenye msururu wa magari maalumu 5 uliwasili muda mfupi baada ya saa nne kamili asubuhi (10:00 asubuhi) akiwa na ulinzi maalumu, msafara wake haukukaguliwa wala kusimama hadi lango kuu la ukumbi wa Westminster Abbey.

Ni viongozi wa afrika na baadhi wachache wa ulaya, asia na Amerika kusini ndio wamesombwa kwa makundi kama wanafunzi kwa mabus ya kifalme kadhaa. Wengine wote walipewa magari ya kifahari madogo presidential car wakasafiri wawili ama mmoja mmoja. Na rais wa Marekani pekee ndie kaenda na gari maalumu na ulinzi wake maalumu hadi langoni. Na Makamu Rais wa China akapewa magari madogo matatu pekee yake katika msafara wake. Rais Putin wa Urusi angekuwepo basi angehudumiwa kwa itifaki aliyohudumiwa Rais Joe Biden.
 
Hii sehemu ya Makumbusho tumeijua siku mingi sana, hatubabaiki, Dar tunaijua nje na ndani kilaza.., ngoja miaka 25 mbele kisha uje tujadiliane 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂
View attachment 2362665
View attachment 2362667
View attachment 2362662

Nairobi outside CBD..,
View attachment 2362698
View attachment 2362697
View attachment 2362699
View attachment 2362696
View attachment 2362694
View attachment 2362695
Hilo Jumba la mwisho la Dar (TanHouse) huwa ugly Sana. Sijui ni Msanifu gani aliyelibuni.
 
Unapost road section while barabara ya masaki ni 5 km long .. au ulikua unajaribu kulinganisha hizo michoro .? Hakuna estate yenye barabara kali kuliko Masaki EA yote .. huna budi kuridhika na ukweli mzee
Tafuta video ya that road in kilimani to kileleshwa na ngong road utapata majibu, that road has road studs with active lighting usiku utadhani ni rabbit runway lights
 
Hv we jamaa kazi unafanya saa ngp? Kuanzia asubuhi mpaka usiku ni JF tu, from Monday to Sunday duuhhh
Mimi sio watchman kama wewe who is needed to be attentive all the time. Again I thought you said that you are going to ignore me, how come you are quoting me again? I just want all Tanzanians in this thread to ignore me so I get a good time kuwanyoorosha vizuri without disturbance.
 
Unapost road section 🤣🤣 while barabara ya masaki ni 5 km long .. au ulikua unajaribu kulinganisha hizo michoro .? Hakuna estate yenye barabara kali kuliko Masaki EA yote .. huna budi kuridhika na ukweli mzee
Hii Masaki moja yenye ukitoa mainroad ni vumbi tupu?🤣🤣
 
Back
Top Bottom