kuna mpuuzi mmoja mkenya amehoji issue ya kijinga ni kwanini tumeelekeza sana focus yetu SA kiasi kwamba hata wanamuziki wetu wa bongofleva wanaenda ku-shoot video zao huko.
ni bahati mbaya sana,lengo la thread hii si kujikita kueleza mahusiano ya kihistoria kati ya tz na nchi nyingine za afrika,vinginevyo tungejaza kurasa kulielezea hilo.
kwa kumuelimisha tu yule mpuuzi mkenya,ni kwamba tanzania ilitumika kuhifadhi wapigania uhuru wa nchi mbalimbali za kusini mwa afrika,ikiwemo south africa.
historia inasema,hata mzee nelson mandela,katika wakati fulani wa vuguvugu la kupigania uhuru wa SA na kuiondoa katika mikono ya makuburu,aliwahi kuishi tanzania eneo la Moshi mkoa wa kilimanjaro, akitumia passport ya tanzania kwa jina bandia la kitanzania.
kiufupi tu ni kwamba ukaribu au urafiki wa watz na wa-SA umejengwa katika misingi ya historia ya wazee wetu walioshiriki katika harakati za kupigania uhuru.
ukaribu huo au urafiki huo,umekuwa ukiendelea hivo toka kizazi mpaka kizazi ndio maana ni rahisi sana kwa mtz kwenda kufanya shughuli zake SA kuliko kwenda kufanya shughuli zake Kenya japo ni nchi jirani na tz kwa upande wa kasikazini-mashariki.