Battle: Dar es Salaam vs Nairobi

Battle: Dar es Salaam vs Nairobi

What a fascinating article. Looks like the “church” is a cult.



Mfalme Zumaridi ni nani?​

Mfalme Zumaridi, mchungaji aliyeendesha ibada kwa kukanyaga migongo ya waumini wake​

February 28, 2022


View attachment 2134521

Jeshi la Polisi jijini Mwanza linamshikilia Diana Bulamba maarufu ‘Mfalme wa Zumaridi’(39) mkazi wa Mtaa wa Buguku, Kata ya Buhongwa kwa tuhuma ya usafirishaji haramu wa binadamu 149 na unyonyaji.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Ramadhan Ng’anzi, jana Jumapili alisema kuwa, tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 6:30 mchana katika Mtaa wa Buguku, Kata ya Buhongwa Wilaya ya Nyamagana.


Alisema watu hao waliosafirishwa 57 ni wanaume na 92 ni wanawake, wakiwemo watoto 24 wenye umri wa miaka kati ya minne hadi 17 na wametolewa kutoka sehemu mbalimbali na kisha kuwafungia nyumbani kwake na kuwatumikisha.

“Watoto hao ni wale waliokatizwa masomo yao kinyume cha sheria na amekuwa akiwahadaa kuwa yeye ni Mungu anayeponya, kufufua watu na kutatua matatizo yao,” alisema

Aidha Kamanda Ng’anzi alisema mtuhumiwa huyo alibainika baada ya Februari 23, mwaka huu polisi kupokea amri ya Mahakama ya Mwanzo Mkuyuni iliyowataka kumkamata mzazi wa kike wa mtoto Samir Abbas aliyetakiwa kufikishwa mbele ya mahakama hiyo baada ya kesi ya msingi kusikilizwa katika mahakama hiyo.


“Katika utekelezaji wa amri hiyo, polisi walifika nyumbani kwa mtuhumiwa Dianna Bundala ambapo ilidaiwa yupo mzazi wa kike wa mtoto huyo na mtoto aliyetakiwa kufikishwa mahakamani, lakini kwa mshangao mtuhumiwa akiwaongoza wafuasi wake waliwashambulia askari na kuwazuia kufanya kazi yao,” alisema.

Baada ya tafrani hiyo askari polisi waliondoka eneo la tukio kwa nia ya kuepusha kutotumia nguvu ambayo ingeweza kusababisha madhara na baadaye Februari 26, mwaka huu walirudi nyumbani kwa mtuhumiwa huyo na kufanikisha ukamataji kwa mujibu wa sheria.

Hata hivyo upelelezi wa kina wa tukio hilo bado unaendelea ili kubaini kiini cha watu hao kukusanyika katika nyumba ya mtuhumiwa ambayo siyo ya ibada wala sehemu rasmi ya kongamano.

Je Mfalme Zumaridi ni nani?

kanisa-Mwanzaaaaa-1.jpg

Mwaka 2019 alijizolea umaarufu mkubwa kutokana na alivyokuwa akiendesha ibada huko jijini Mwanza tofauti na makanisa mengine yanavyoendesha ibada.

Aina yake ya uendeshaji wa ibada ulikuwa gumzo kwani Mfalme Zumaridi haamini katika aina yeyote ya dini hali inayoleta maswali hadi sasa.


Ana wafuasi wengi wanaomuamini, na wanamwamini `Mfalme Zumaridi’ kama mwakilishi wa Mungu duniani ama `Yesu Kristo’ wa duniani.

Wakati huo wafuasi wake hulala chini huku mchungaji wao akiwakanyaga na kupita juu yao, wakati mwingine waumini wa kanisa hilo pia huonekana wakigaragara kwenye matope ya majaruba ya mpunga jirani na kanisa lao kama moja ya ibada ikiwa ni ishara ya kumshughulikia shetani.

Hata hivyo baada ya kuonekana video mbalimbali za mahubiri yake kanisani kwake, Serikali iliingilia kati na ndipo ikachukua uwamuzi wa kulifungia kanisa la Mfalme Zumaridi, ambapo pia iliamuru kutofanyika ibada kanisani hapo wala nyumbani kwa Mfalme Zumaridi.


Hatua hii pia ilikua ni baada ya uchunguzi kubaini kuwa baadhi ya maneno na matendo yyalikuwa yakifanyika kanisani kwa Mfalme Zumaridi yalikuwa na athari na madhara kwa waumini na watu wengine pamoja na umnwepo wa malalamiko kutoka kwa wananchi na viongozi wa taasisi zingine za kidini kuhusu ukiukwaji wa sheria, maadili na imani ya kidini.

what is this!!!!!!
 
Kama utani tu Ila jamaa wanaenda kuifanya DODOMA ya kijani .. barabara za mji wa serikali mtumba 👇
Screenshot_20220301-101310_1.jpg
hapa naona barabara za waendesha baiskeli, njia za waenda kwa miguu, mifereji ya maji taka na bustani, hiz barabara zitakua nzuri sana
 
Kama utani tu Ila jamaa wanaenda kuifanya DODOMA ya kijani .. barabara za mji wa serikali mtumba 👇View attachment 2134841hapa naona barabara za waendesha baiskeli, njia za waenda kwa miguu, mifereji ya maji taka na bustani, hiz barabara zitakua nzuri sana
halafu unakuta Mkunya anakenua 24/7 kuhusu ushuzi wa barabara zao! Naiona Dodoma ikifanana na Gaborone city haswa ukiangalia climate ya Dodoma!

 
Kenya kutajengwa data centre kubwa sana hivi karibuni na ICANN.

Kenya to host one of Africa’s two giant data hubs​


Kenya will host one of the two mega data centres in Africa that will increase Internet speeds and make it harder for hackers to bring down websites.

The new data centres, which will have multiple servers with a high bandwidth to deal with spikes in traffic, will offer the continent faster access and better protection from cyberattacks.

The Internet Corporation for Assigned Names and Numbers (ICANN), the non-profit corporation that coordinates the domain name systems, announced on Monday that it will set up two Root Server (IMRS) clusters, one of which will be in Kenya.

"The clusters ensure that Internet queries from Africa can be answered within the region, and not be dependent on networks and servers in other parts of the world, thus reducing latency and improving Internet user experience in the entire region,” the organisation entrusted with stewarding the Internet’s unique identifier systems in the world said.

ICT Cabinet Secretary Joseph Mucheru said the new infrastructure is in line with the African Digital Transformation Strategy (2020-2030) and more specifically with Kenya’s Digital Economy Blueprint, which identifies infrastructure as one of the five key pillars necessary for the digital transformation of the economy.

“We, therefore, thank ICANN for their confidence in choosing Kenya one more time as one of the hosts of this important infrastructure that would serve not only Kenya, but the rest of Africa and the world,” Mr Mucheru said.
 
Vyoyote tuu ila inafaa tupunguze ujenzi wa mahoteli kwenye hifadhi kwa sababu inakua haileti maana tunawaamisha wamasai kwenye hifadhi ili kujenga hoteli zaidi
Wamasai walipohamishwa 1960s walipewa sehemu Morogoro na Tanga. Kinachotokea sasa ni ukahidi wengi wamerudi na wengine wanatokea Kenya! Ngorongoro CA ina sheria zake yaani idadi ya watu ndani ya Ngorongoro haiupaswi kuwa zaidi ya 800! na mifugo haipaswi kuwa zaidi ya 50,000!
 
Back
Top Bottom