Battle: Dar es Salaam vs Nairobi

Battle: Dar es Salaam vs Nairobi



EiksXWhXcAA-H7b
 

Attachments

  • Screenshot_20200923-150353.jpg
    Screenshot_20200923-150353.jpg
    85.1 KB · Views: 7
  • Screenshot_20200923-150412.jpg
    Screenshot_20200923-150412.jpg
    80.8 KB · Views: 7
  • Screenshot_20200923-150412.jpg
    Screenshot_20200923-150412.jpg
    80.8 KB · Views: 11
  • Screenshot_20200923-150353.jpg
    Screenshot_20200923-150353.jpg
    85.1 KB · Views: 9
Ujenzi hospitali ya Uhuru wafikia 87%

UJENZI wa Hospitali ya Uhuru wilayani Chamwino mkoani Dodoma umekamilika kwa asilimia 87 baada ya serikali kutekeleza ahadi yake ya kuzielekeza takribani Sh bilioni 2.3 zilizotolewa na Kampuni ya Bharti Airtel ya India kujenga hospitali hiyo.

Hayo yamebainishwa na mhandisi wa ujenzi wa jengo la Hospitali ya Uhuru, Girimu Kanansi wakati Ofisa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando alipotembelea hospitali hiyo kuangalia maendeleo ya ujenzi wake.

Kanansi alisema jengo hilo lililokamilika kwa asilimia 87 linajengwa kwa weledi na Kampuni ya Suma JKT kupitia vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), kinyume cha awali ambako majengo makubwa kama hayo yalikuwa yanajengwa na kusimamiwa na wageni kutoka nje ya nchi.

“Kazi inayoendelea ni kutengeneza sakafu, kuweka mifumo ya umeme na kuskimu kuta, hivyo ninaishukuru Serikali ya Awamu ya Tano na Kampuni ya Mawasiliano ya Airtel kuona umuhimu wa kupeleka huduma za afya karibu na wananchi hususani mkoani Dodoma ambako ndiko Makao Makuu ya nchi,” alieleza Kanansi.

Alisema jengo hilo lilitarajiwa kukamilika Mei mwaka huu, lakini ilishindikana kutokana na changamoto ya msimu wa mvua nyingi uliosababisha kutokuwa na mazingira rafiki ya kusafirisha vifaa kwenda eneo la ujenzi.

Aidha, kutokana na hali hiyo mkandarasi aliomba kuongezewa muda na anatarajia kukamilisha ujenzi Oktoba mwaka huu iwapo hakutakuwa na changamoto yoyote itakayojitokeza ikiwemo ya kutofika kwa vifaa vya ujenzi kwa wakati.

Mbando alisema kam- puni yao imekuwa na utaratibu wa kutembelea eneo hilo la ujenzi kuona maendeleo kwa kuwa ni sehemu ya kufanikisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo hususani miradi ya afya ikiwemo Hospitali ya Uhuru ambayo kupitia mbia mwenza Bharti Airtel ya Tanzania ndio iliyotoa Sh bilioni 2.3 kwa serikali iliyozielekeza katika ujenzi wa hospitali.

Alisema Kampuni ya Airtel Tanzania kwa kutambua uhitaji wa huduma ya mawasiliano, tayari imefungua maduka manne wilayani Chamwino likiwemo eneo la Hospitali ya Uhuru yatakayoendelea kutoa huduma ikizingatiwa kuwa baada ya hospitali kuanza kufanya kazi huduma za fedha zitahitajika.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati Kampuni ya Airtel Tanzania ikitoa gawio kwa serikali, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James, alisema serikali ya Tanzania ilianza uchunguzi wa umiliki wa Airtel Tanzania na baadaye kufanya mazungumzo na kampuni mama ya Bharti Airtel ya India kuanzia mwaka 2018 na kufanikisha serikali kumiliki asilimia 49 ya hisa za kampuni hiyo.

Alisema makubaliano hayo yaliyowezesha kunufaika kwa pande hizo mbili ndiyo yalimfanya Mwenyekiti wa Bharti Airtel ya India, Sunil Mittal kutoa Sh bilioni 2.3 kwa serikali, ikiwa ni shukrani kwa kuanza makubaliano mapya yenye tija.

Katibu Mkuu alisema serikali iliona ni vema fedha hizo zipelekwe kujenga Hospitali ya Uhuru mkoani Dodoma inayotarajiwa kukamilika Oktoba mwaka huu.

Screenshot_2020-09-23-16-45-41.jpeg
 
Back
Top Bottom