Basi la Kampuni ya New Force lapata ajali na kuua watu watano

Basi la Kampuni ya New Force lapata ajali na kuua watu watano

Ndio wanabeti kwa kupewa 100,000 kwa dereva anayewahi kufika pale Uyole au Msamvu au Magufuli. Hizi wapo madereva wa SAULI na Newforce. Kwa sisi tunaotumia barabara ya TANZAM, Hayo mabasi yalitakiwa yafungiwe muda na tumelalamika sana kuwa yachukuliwe hatua wenye mamlaka wananyamaza tu. Natamani leo dereva awe amekufa, kuwe na ndugu wa kiongozi yoyote wa nchi au awemo Polisi mmoja amayechukua rushwa ya 1000 kisha kufumbia macho huo upuuzi.

Kuna siku nilikuwa nasafiri na nipo kwenye V8 jamaa wakatupita wanakimbizana na hatukuweza wakutana hadi tumefika pale kwenye cheki point ya uhamiaji Makambako. Jamaa wanakimbiza hovyo, wana overtake hovyo n.k. Siku tulikutana na SAULI anashuka kitonga pale, aiseeeee.
Kwa inavyoonekana pale sijui kama dereva alipon labda aruke napo ni hatari pia.
 
Ndio wanabeti kwa kupewa 100,000 kwa dereva anayewahi kufika pale Uyole au Msamvu au Magufuli. Hizi wapo madereva wa SAULI na Newforce. Kwa sisi tunaotumia barabara ya TANZAM, Hayo mabasi yalitakiwa yafungiwe muda na tumelalamika sana kuwa yachukuliwe hatua wenye mamlaka wananyamaza tu. Natamani leo dereva awe amekufa, kuwe na ndugu wa kiongozi yoyote wa nchi au awemo Polisi mmoja amayechukua rushwa ya 1000 kisha kufumbia macho huo upuuzi.

Kuna siku nilikuwa nasafiri na nipo kwenye V8 jamaa wakatupita wanakimbizana na hatukuweza wakutana hadi tumefika pale kwenye cheki point ya uhamiaji Makambako. Jamaa wanakimbiza hovyo, wana overtake hovyo n.k. Siku tulikutana na SAULI anashuka kitonga pale, aiseeeee.
Ila ajali isikie tu niliwahi shuhuda ajali ya Rungwe express DNN pale Iyovi kipindi hiko ziko mbichi dah noma sana
 
Yule jamaa ukikimbiza gar huna kazi

lakin hua anamoja hiyo ya asubuhi ndo inaruusiw kukimbizana na BM pale Arusha na ni ile ya zaman plate no A
Ila kuna kipindi 2019 mbona alikua anaweka ligi na Sauli,Deer..

Katika kampuni zote Kampuni niliyoshuhudia wana overtake za kishenzi ni SAULI.
 
Hiyo midude inakimbia yaani ukipanda roho mkononi?!

Kuna lile lijamaa linaitwa linyama au (Ndugu abiria) na mwingine wa Sauli anaitwa Titho wajinga wanakanyaga moto mpk unaacha wosia kimoyo moyo [emoji24][emoji24]
 
Naushuhuda mmoja Miaka mi 3 iliyopita
Kuna rafiki yang ni dereva wa bus kampuni X bus za safari ndefu Sasa weekend nilikua naenda nae Bukoba tukifika ushirombo ananiachia niendeshe nilichokua nainjoy ni kukimbizana na bus zingine tulizotoka nazo Arusha nilikua sifikirii kabisa maisha ya watu bahati mbaya hata njia ilikua siijui vizuri.

Tukitoka Bukoka ye anaendesha Hadi singida na tukitoka singida kwenyee saa kumi na mbili jion ananipa mi naenda napeleka chuma had Arusha hapo mi siyo dereva wa hilo bus wala mmiliki hanijui ila ushkaji tu na michezo ya kipuuzi ndo tuliweka mbele Sasa ilikua ni mwendo wa kukimbizana tu, Na kila mkoa tuliokua tunaingia stand Kuna mashabiki wengi ukiwa wa kwanza shangwe ni kubwa balaa
siku moja nikawa nateremka mlima mmoja una kona Kali sana kabla hujaingia babati nikakuta ajali mbaya sana

baada ya kushuhudia ile ajali nilijiona sina tofauti na mtu anaejaribu kucheza na roho za watu niliamua kuacha kabisa ule mchezo niliokuanafanya jamaa akawa ananitafuta weekend nikawa natengengeneza sababu tu ilimradi nisiende.

kwahiyo huku barabarani kuna mambo mengi sana yanaendelea upande wa ma bus kuna ligi ambazo zina mashabiki zaidi ya ligi ya Uefa champions league, watu wanashabikia mwendo kasi wapo tayari wasilale had saa 6 usiku wasubiri bus stand waone Nani kawa wakwanza kufika washangilie

Aina hii ya maisha tuliyoamua kuishi tusipokua makini tutaendelea kushuhudia ajali mbaya sana.
 
Golden deer na New force nadhani mmiliki wake ni shemeji ya mkubwa Fulani huko LATRA..
hizi Basi zinaenfeshwa rafu lkn hakuna RTO anayethubutu kuyakemea.
ma RTO Moro, Iringa, Mbeya, songe semeni ukweli, mmiliki hua anawaona Mara kwa Mara!
Sisuseni
 
Naushuhuda mmoja Miaka mi 3 iliyopita
Kuna rafiki yang ni dereva wa bus kampuni X bus za safari ndefu Sasa weekend nilikua naenda nae Bukoba tukifika ushirombo ananiachia niendeshe nilichokua nainjoy ni kukimbizana na bus zingine tulizotoka nazo Arusha nilikua sifikirii
Tunaishi Maisha ya kila kitu kamali na michezo ya kubahatisha!!
 
LATRA Wana kila sababu ya kulaumiwa kwa ajali za mabasi. Juzi tu hata wiki haijaisha waliyapa mabasi ya Ally's na Katarama adhabu ya kitoto.

Basi linahatarisha maisha ya watanzania wasio na hatia linapewa adhabu ya kubadilishiwa masaa ya kuondoka. Nonsense, siku wakifa ndugu zenu LATRA mtatia akili.
 
Kwenye Ile video nimeona mkono wa mtu ukiwa umechomoka kama mdoli...........

Mungu awatie nguvu majeruhi na awalaze pema waliopoteza ndugu zao......

Hawa watu wanakimbia utadhani wamebeba ng'ombe vile.......

Niliwahi kupanda New force naenda Tunduma nikashukia Ilula.....nilikuwa naona kabisa uhai wangu ukiwa rehani......nikasema pesa zinatafutwa....
Siku nimekula NewForce tulipata kipengele Kitonga pale gari ilipasuka kioo cha site mirror tu hamna alieumia. Tukaendelea kibishi ila mwendo wa ni wa hatari sana.
 
Back
Top Bottom