Basi la Kampuni ya New Force lapata ajali na kuua watu watano

wakukurupuka1

JF-Expert Member
Feb 17, 2023
525
1,186
1687353605844.png

Basi kampuni ya mwekezaji kutoka China, New Force/Golden Deer imepata ajali na kuua watu kadhaa.

Wakati ajali hiyo inatokea ndani ya mwezi huu itakuwa ajali ya 3 kwa kampuni hiyo baada ya last week kupata pia ajali maeneo ya Morogoro.

Chanzo ni mwendo wa mashindano.

======

Kamanda wa Polisi, Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP John Makuri amethibitisha tukio la ajali mbaya iliyotokea katika Eneo la Igando Wilaya ya Waging'ombe ikihusisha basi la NewForce lililokuwa linatoka Dar kwenda Sumbawanga.

Kwa mujibu wa Kamanda Makuri, bado idadi kamili ya Vifo na Majeruhi haijajulikana na kwa sasa bado wapo eneo la tukio huku Majeruhi wakipelekwa Hospitali ya Kanisa ya Ilembula

======

Watu watano wamefariki huku wengine wakijeruhiwa, baada ya basi la kampuni ya New Force, lenye namba za usajili T 173 DZU, kuanguka wakati likijaribu kulipita lori, kisha kupoteza uelekeo na kugonga daraja katika eneo la Kijiji cha Igando kilichopo wilayani Wanging'ombe mkoani wa Njombe.
 
Bus kampuni iliyochini ya mwekezaji kutoka china newforce/golden deer imepata ajali na kuja watu wengi

Wakati ajali iyo inatokea ndani ya mwezi huu inatakua ajali ya 3 Kwa kampuni iyo baada ya last week kupata pia ajali maeneo ya Morogoro

Chanzo kikuyu ni mwendo wa mashindano
Ni ajali ya 5 kama sio ya 4 mkuu. Pole kwa wafiwa na majeruhi tunawaombea wapone haraka.
 
Bus kampuni iliyochini ya mwekezaji kutoka China New Force/Golden Deer imepata ajali na kuja watu wengi.

Wakati ajali hiyo inatokea ndani ya mwezi huu inatakua ajali ya 3 kwa kampuni hiyo baada ya last week kupata pia ajali maeneo ya Morogoro.

Chanzo ni mwendo wa mashindano.
Linakwenda wapi!? Mbona unaharaka Sana!!
Anyway watu WA nyanda za juu hushangikia magari kukimbia!!
 
Back
Top Bottom