Naushuhuda mmoja Miaka mi 3 iliyopita
Kuna rafiki yang ni dereva wa bus kampuni X bus za safari ndefu Sasa weekend nilikua naenda nae Bukoba tukifika ushirombo ananiachia niendeshe nilichokua nainjoy ni kukimbizana na bus zingine tulizotoka nazo Arusha nilikua sifikirii kabisa maisha ya watu bahati mbaya hata njia ilikua siijui vizuri.
Tukitoka Bukoka ye anaendesha Hadi singida na tukitoka singida kwenyee saa kumi na mbili jion ananipa mi naenda napeleka chuma had Arusha hapo mi siyo dereva wa hilo bus wala mmiliki hanijui ila ushkaji tu na michezo ya kipuuzi ndo tuliweka mbele Sasa ilikua ni mwendo wa kukimbizana tu, Na kila mkoa tuliokua tunaingia stand Kuna mashabiki wengi ukiwa wa kwanza shangwe ni kubwa balaa
siku moja nikawa nateremka mlima mmoja una kona Kali sana kabla hujaingia babati nikakuta ajali mbaya sana
baada ya kushuhudia ile ajali nilijiona sina tofauti na mtu anaejaribu kucheza na roho za watu niliamua kuacha kabisa ule mchezo niliokuanafanya jamaa akawa ananitafuta weekend nikawa natengengeneza sababu tu ilimradi nisiende.
kwahiyo huku barabarani kuna mambo mengi sana yanaendelea upande wa ma bus kuna ligi ambazo zina mashabiki zaidi ya ligi ya Uefa champions league, watu wanashabikia mwendo kasi wapo tayari wasilale had saa 6 usiku wasubiri bus stand waone Nani kawa wakwanza kufika washangilie
Aina hii ya maisha tuliyoamua kuishi tusipokua makini tutaendelea kushuhudia ajali mbaya sana.