Bashungwa hutoshi!

Usumbufu wa taratibu za maandalizi, wapenzi na mashabiki kufika na kuingia uwanjani mapema kuzuia kukanyagana milangoni, matayarisho yawalinzi wetu, wapenzi wameingia jijini toka mikoani, gharama zote hizi nani analipa?
Gharama ipo kwa Yanga tu?
 
1620491564721.png

Yanga hiyoooo!
 
Kwa mtu makini akimuangalia Bashungwa sekunde 25 au fanyeni utafiti chukueni picha au video ya Bashungwa mmwangalie tu kuna kitu utagundua kuhusu akili ya huyu jamaaa
 
Mimi si mpenzi kinda kinda wa Yanga lakini huwa naifuatilia sana.

Leo ilikuwa tuwafunge Simba ila pambano likaahirishwa kutokana na kujitokeza kwa shughuli nyingine ghafla ya kuzindua kitabu cha Mzee Ruksa.

Tatizo langu liko hapo!
Taratibu za kuahirisha pambano inabidi taarifa itoke masaa 24 kabla.
Sasa haya tunayoyaona niuswahili uliokithiri.
Hatuwezi kwenda namna hii.

Taarifa ya shughuli ya Mzee Ruksa haikujulikana mapema?

Usumbufu wa taratibu za maandalizi, wapenzi na mashabiki kufika na kuingia uwanjani mapema kuzuia kukanyagana milangoni, matayarisho yawalinzi wetu, wapenzi wameingia jijini toka mikoani, gharama zote hizi nani analipa?

Wizara husika na michezo imeleta furugu kwa wapenzi wa mpira YANGA na SIMBA.

Waziri na Wizara ikicheza na miamba hii ya soka nchini , hautaeleweka kamwe.

Na hapo ndio nasema Bashungwa anatakiwa kuwajibika, hatoshi.

View attachment 1777815
Wanatakiwa washitakiwe na kulipa gharama za wadau mbalmbali, wanaendesha Ligi kama club ya mpira inayo milikiwa na mtu binafsi
 
Nakasirika kukiri kwamba kama Bi mkubwa hata up her game mapema baada ya miezi 6 watu watakua wanafanya watakavyo.

Mama amekuwa soft sana hadi inaogopesha, nadhani angechukua baadhi ya Wizara aziweke katika close watch la sivyo ategemee ma EPA na ma ESCROW kama yote. Atathibitisha kwamba yule Daktari aliyeangukia pua alikua yupo sahihi sana
 
Kweli Yanga ameonyesha matatizo makubwa ya maamuzi ya pupa.
Masopyakindi, sijui kama hii taarifa naielewa vizuri. Saidia mkuu.

Mchezo umeahirishwa (ghafla), kwa sababu zipi, uzinduzi wa kitabu?

Kama hivyo ndivyo, mbona nawe leo nakuona ukishangilia uozo wa ajabu namna hii? Hii itakuwa serikali ya namna gani hii, si ndio tutakuwa "Banana kabisa hata kuliko tulivyowahi kuwa wakati wowote?

Hata kama kuna sababu muhimu zaidi ya hiyo, Yanga, kufuatana na barua yao hiyo wapo sahihi kabisa.

Nami nashangaa kuona mtu mwenye uelewa wa mambo kama wewe ukiwashutumu wanaofuata taratibu!

Tukienda hivi, huko serikalini kutakuwaje miezi sita toka sasa!
 
Soma vizuri mkuu mimi namlaumu Bashungwa na Wizara yake kwa kucheza na unazi wa Watanzania kwa suala la soka, hasa YANGA na SIMBA.
Watu wana bet wake zao kwa unazi wa mechi hizi.
Wasituchezee.
Utaratibu ni every thing.
 
Hivi Bashungwa huko aliko anajiskiaje baada ya kutuahirishia mechi?

Amefaidika na nini sasa?......

Hizo hasara zote na hao watu waliopigwa mabomu anawafidiaje?

Hawa wahutu sijui wana akili gani yaani
 
Back
Top Bottom