Dar: Polisi Wakamata Watuhumiwa 161 wanaojihusisha na wizi wa vifaa vya magari, pikipiki na uvunjaji

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
956
1,000
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI

JESHI LA POLISI TANZ
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA 161 WANAOJIHUSISHA NA WIZI WA VIFAA VYA MAGARI, PIKIPIKI NA UVUNJAJI.


Ndugu Wana habari, Mnamo tarehe 20.04.2021 na 24.04.2021 nilitoa taarifa kwa umma za mafanikio ya Oparesheni Maalum ya ukamataji wa wezi wa Magari,vifaa vya magari na Pikipiki.

Mnamo tarehe 26.04.2021 hadi 02.05.2021 Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam liliendelea na oparesheni maeneo mbali mbali ya Jiji na kufanikiwa kukamata watuhumiwa 161.

Katika idadi ya watuhumiwa hao 161 kuna watuhumiwa watano vinara wa wizi wa pikipiki wamekamatiwa Zanzibar wakiwa na pikipiki 40 za wizi, watuhumiwa hawa wamekuwa wakiiba pikipiki hapa Jijini Dar es Salaam, Morogoro na Pwani na kuzipeleka Zanzibar kutafuta wateja.

Watuhumiwa hao wataletwa hapa Dar es Salaam kutoka Zanzibar pamoja na vielelezo na watafikishwa mahakamani baada ya kukamilisha taratibu zote za kisheria.

Aidha, katika oparesheni hiyo tulifanikiwa kukamata magari mawili aina ya Toyota Noah lenye namba T 770 ACY na Toyota IST yenye namba T 137 DMM magari haya yote yaliibiwa mwezi Aprili na kupatikana mwezi Mei 2021.

Vile vile tulikamata silaha ndogo bastola aina ya BROWNING COURT yenye namba B113558 TZ CAR 110526 ambayo iliibiwa tarehe 07/04/2021 huko maeneo Chanika Lubakaya nyumbani kwa mtoa taarifa, ambapo kikosi kazi cha Jeshi la Polisi kilifanya ufuatiliaji na kufanikiwa kuikamata silaha hiyo tarehe 01/05/2021 maeneo hayo hayo ya chanika.

Pia katika oparesheni hiyo tulifanikiwa kukamata vitu mbalimbali vidhaniwavyo kuwa ni vya wizi kama ifuatavyo:-

 • Pikipiki 91
 • TV za aina mbalimbali, Ving’amuzi vyake, Subwoofer na Computer .
 • Pikipiki za matairi matatu (Bajaji) 04
 • Bello 24 za nguo za mitumba .
 • Vifaa vya umeme
 • Simu za mkononi
 • Mitungi ya Gesi
 • Vipuri vya magari kama vile milango ya magari, taa za magari, mabampa ya magari, Power window, Gia box, n.k.
Ndugu wana habari, oparesheni hii ni endelevu, itaendelea kufanyika ili kuhakikisha jiji letu linaendelea kuwa shwari.

Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linamshikilia mzee mwenye miaka 61 kwa tuhuma za wizi kwenye Maghala na maduka kwa kutumia funguo bandia, Mzee huyo anayefahamika kwa jina la Said Abdallah (61) Mkazi wa Mbagala Kilungule, alikamatwa tarehe 04/05/2021 huko Mbagala Kilungule akiwa na funguo bandia 83, misumari ya aina mbalimbali 47 ambayo ni malighafi za kutengenezea funguo bandia.

 • Mtuhumiwa alihojiwa na kukiri kufanya uhalifu tangu mwaka 2013 maeneo mbalimbali ya Jiji kwa kutumia funguo bandia.
Onyo, Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linatoa onyo kwa wale wote waliotoka Jela/gerezani kwa sababu mbalimbli na watu wengine wanaojihusisha na vitendo vya vya uhalifu waache kujihusisha na vitendo hivyo, kwani hatutashindwa kuwakamata na kuwachukulia hatua kali za kisheria.


 • POLISI KUIMARISHA ULINZI UWANJA WA MKAPA KATIKA MPAMBANO WA WATANI WA JADI KATI YA SIMBA NA YANGA
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama limejipanga kuimarisha ulinzi na usalama katika mchezo wa watani wa jadi kati ya Simba na Yanga utakaochezwa uwanja wa Mkapa tarehe 08/05/2021 kuanzia majira ya saa 11 jioni.

Tumejipanga kuimarisha ulinzi kwa kuweka askari wa kutosha katika maeneo yote yanayozunguka uwanja wa Mkapa na barabara zinazoingia na kutoka uwanjani hapo.

Aidha, Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linatoa wito kwa wazazi/walezi wanaopenda kwenda na watoto uwanjani kuwaangalia kwa karibu au kuwaacha kabisa nyumbani ili kuepusha madhara yoyote yanayoweza kujitokeza

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linatoa wito kwa mashabiki na wapenzi wa soka kufika uwanjani mapema ili kuepusha msongamano wakati wa kuingia uwanjani hapo kwani milango ya uwanja itafunguliwa mapema na ulinzi utakuwepo wa kutosha.

Pia tunawataka mashabiki kushangilia kwa amani na utulivu wawapo uwanjani ikiwa ni pamoja na kuepuka mambo yafuatayo:-

 • Mihemuko na maneno ya kuhasimiana kati yao.
 • Kuingia na chupa za maji majukwaani
 • Kuingia na silaha ya aina yoyote
 • Kupaki magari ndani ya uwanja pasipokuwa na kibali maalum
 • Kukaa sehemu ambazo tiketi zao haziruhusu
Lazaro B. Mambosasa - SACP

Kamanda wa Polisi Kanda maalum

DAR ES SALAAM.

06/05/2021

1620295759629.png
 

Mkwe21

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
2,150
2,000
Hii imekaa vizuri!! Ila kuna polisi Lukuki njiani (barabarani) ili kupunguza foleni ila msaada wao ni mdogo sana!! Kwani hawatumii weledi!! Pia tunaomba biashara zipunguzwe katikati ya njia ili tuweze kuwahi kwenye kujiongezea kipato!! Foleni huchangiwa na ufanyaji was biashara katikati ya barabara
 

Bigawas

Senior Member
Feb 19, 2021
125
225
Mzee wa miaka 61 ni jambazi, tena ameanza wizi kuanzia 2013. Inaonyesha alistaafu,akaingia kwenye mishe hizi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom