Bashe, Tofauti ya Sukari Kutoka Brazil vs itokayo Zambia na Uganda ni ipi?

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,163
22,672
Salaam, Shalom!!

Tunaambiwa tusubiri mwezi tena Ili tupate sukari ya kututosha,

Ningependa kujua nini maana ya dharura?

Yaani tusubiri bunge likae ndipo libadili taratibu za kuwaondolea viwanda kuwa waagizaji pekee? Kwanini lisitoke tamko la dharura kuruhusu wafanyabiashara kuagiza sukari Toka Zambia na Uganda?

Nchi Iko kwenye uhaba wa Sukari, kwanini wafanyabiashara wasiruhusiwe kuvuka mipaka na kununua sukari hapo Jirani Zambia au Uganda?

Sukari Toka Zambia au Uganda ni wiki tu imefika.

Brazil kunani?
Hata ubora tu wa Sukari ya Kilombero imethibitika kuwa Bora kuliko ya Brazil, sukari Toka Brazil haikozi kwenye chai hata uweke vijiko 5 pia kuna tetesi kuwa sukari hiyo Toka Brazil ni GMO ,Bei Chee ila HASARA Kwa AFYA za watumiaji, cancer nk nk.

Ni muda mwafaka wa kununua sukari Kwa Jirani zetu kukidhi uhaba uliopo tukisubiri viwanda vyetu vya ndani vizalishe sukari ya kutosha.

Ombi: Tuchukue ndege yetu mpya ya mizigo ilopaki, ipakie shehena ya kutosha hapo Zambia na Uganda, ndani ya wiki shida ya sukari iwe historia.

Nawasilisha🙏
 
Brazil siyo sukari ni uhundwaji wa chemicals ndiyo maana hata ukiunga inawekwa nyingi sana.

Hakuna nchi (kama Tanzania) wataruhusu mlete sukari kutoka Zambia au Uganda ambapo wanajua hawatapata 10 percentage, hii dunia imebaki na binadamu wachache sana, wengi ni watu waliopo duniani.
 
Ndege zetu mpya kabisa zimepaki,

Tuchukue ndege Moja mpya itue pale Lusaka Zambia ipakie shehena ya kutosha sukari iwe mtaani ndani ya siku 7 tu.
 
Brazil siyo sukari ni uhundwaji wa chemicals ndiyo maana hata ukiunga inawekwa nyingi sana.

Hakuna nchi (kama Tanzania) wataruhusu mlete sukari kutoka Zambia au Uganda ambapo wanajua hawatapata 10 percentage, hii dunia imebaki na binadamu wachache sana, wengi ni watu waliopo duniani.
Unaachaje sukari Toka Kwa Museveni au Zambia Kwa Jirani zetu halafu uagize sukari Toka Brazil?

Tukichukua ndege yetu mpya ya mizigo ikapakie sukali Zambia au UG, ni siku mbili tu Nchi tatizo limeisha.

Mbona Mrema aliweza?

Tuache ubinafsi🙏
 
Salaam, Shalom!!

Tunaambiwa tusubiri mwezi tena Ili tupate sukari ya kututosha,

Ningependa kujua nini maana ya dharura?

Yaani tusubiri bunge likae ndipo libadili taratibu za kuwaondolea viwanda kuwa waagizaji pekee? Kwanini lisitoke tamko la dharura kuruhusu wafanyabiashara kuagiza sukari Toka Zambia na Uganda?

Nchi Iko kwenye uhaba wa Sukari, kwanini wafanyabiashara wasiruhusiwe kuvuka mipaka na kununua sukari hapo Jirani Zambia au Uganda?

Sukari Toka Zambia au Uganda ni wiki tu imefika.

Brazil kunani? Hata ubora tu wa Sukari ya kilombero imethibitika kuwa Bora kuliko ya Brazil, ni muda mwafaka wa kununua sukari Kwa Jirani zetu kukidhi uhaba uliopo tukisubiri viwanda vyetu vya ndani vizalishe sukari ya kutosha.

Nawasilisha🙏
unawasilisha nini akati shehena ya sukari inapakuliwa bandarini wakati huu 🐒

hayo masuala ya sheria sio ya wakati huu ni wakati ujao, hiyo ni dira na uelekeo tu umepewa ili kusudi baadae isijekutokea hali kama ya sasa 🐒

hivi sasa mambo yalishapangwa na yanatekelezwa kama yalivyokusudiwa 🐒
upotoshaji si muhimu na hauna maana yeyote....
 
Hiyo sukari inayopakuliwa bandarini wanatumia chepe kufaulisha Mzigo?
 
Salaam, Shalom!!

Tunaambiwa tusubiri mwezi tena Ili tupate sukari ya kututosha,

Ningependa kujua nini maana ya dharura?

Nchi Iko kwenye uhaba wa Sukari, kwanini wafanyabiashara wasiruhusiwe kuvuka mipaka na kununua sukari hapo Jirani Zambia au Uganda?

Sukari Toka Zambia au Uganda ni wiki tu imefika.

Brazil kunani? Hata ubora tu wa Sukari ya kilombero imethibitika kuwa Bora kuliko ya Brazil, ni muda mwafaka wa kununua sukari Kwa Jirani zetu kukidhi uhaba uliopo tukisubiri viwanda vyetu vya ndani vizalishe sukari ya kutosha.

Nawasilisha🙏
Hiyo sukari ya Brazil inayoitwa brown sugar ni sukari chafu na takataka za sukari ambazo ni very cheap, kama London wazungu hawali utumbo hivyo Wanigeria na Waafrika ni kujikusanyia tuu bure, the cost ni transport only!.

Sukari yote ya Zambia inapita Dar port!. Tuondoe tuu zuio la ku imports sukari, ya Uganda ipitie Mutukula, ya Zambia ipitie Tunduma, ya Malawi ipitie Kasumulu, ya Kenya ipitie Namanga na Holili, ya Rwanda ipitie Rusumo, Burundi kupitia Mayovu, Msumbiji kupitia Nakonde, it take just a day na sukari itakuwa imejaa Tanzania!.
P
 
Back
Top Bottom