Barua ya wazi kwa Mbowe & CHADEMA: Kajipangeni Upya

watakuita Sukuma Ganga au Mataga bila kujua hata wewe ulikuwa unapambana na team mwendazake...ngoja waamke huko..

wamejigeuza kundi ambalo agenda zao ndio ziwe agenda za watanzania wote, wanataka Taifa liwadekeze maana wao ndio specials katika Taifa hili...yaani leo hii Taifa na chama kilicho madarakani kiache kutekeleza ilani ya chama baadala yake kiwasikilize chadema na ilani yao..
 
Hapa umebwabwaja tu mkubwa, unapiga propaganda za ujinga wa siasa majitaka za maCCM....

Sijaona hoja yako. Hujui usemalo wala uzungumzalo..
Ningekuwa nimebwabwaja usingesoma na kunijibu. Ila umeona hoja. Nikuhakikishie kuwa Tanzania haina CONTROL kwenye Bei za mafuta bali ni nguvu ya soko (supply & demand). Mwaka jana tuli enjoy price ya mafuta hadi Tsh 1560/- kwa lita ya dizeli kwa kuwa shughuli za dunia zilipungua kutokana na COVID19. Demand iliteremka

Kuanzia Februari 2021 nchi nyingi hasa za ulaya zimefanya vaccinations hadi 40% ya population na maambukizi yamedhibitiwa na hivyo shughuli za uchumi na biashara zimepamba moto. As a result demand ya mafuta imepanda. Na Bei inapanda
 
CDM hiyo katika mpya muiweke kwenye ilani yenu ya 2025 mkaiombee kura waacheni CCM watekeleze ilani yao waliyoiombea kura...nyie subirini 2025 kwenye ilani yenu muiweke katiba mpya halafu mje kuinadi tuwape ridhaa..
 
We pimbi, rais anawajibika kufuata vipa umbele vya umma/wananchi, siyo vyake yeye binafsi na kikundi kidogo Cha watu wa chama chake🙄

Kwani ile nafasi amejiweka pale mwenyewe?!!!

vipaumbele vya umma ni vipi? na nani aliviandaa?
 
CDM wanazingua mama kaanza vizuri hafu hata hyo katiba wanayolilia ndo itabadilisha umaskini,Bora basi wangekuja na kipaumbele Cha kuondoa umaskini na ajira kwa vijana ambao ni wengi kwenye hili taifa. Waje na agenda ya kugusa watu wengi ila blah blah za katiba tu bila kuondoa umaskini it doesn't make sense.
Kuna kiasi kikubwa huelewi(na wenzako) nini maana ya katiba na inatakwa kwa nini.Nendeni mbali zaidi bila kudhani ni vitabu tu vyenye maandishi vitachapishwa Kaa ujiulize:Kama ni kitu "chepesi" kwa nini CCM wakatae kuwa na mpya?Think and think and think bigger!🤔🤔🤔🤔🤔🤔
 
With all due respect, hii barua yako inatakiwa iishie kwa secretary, haistahili kufika kwa Mbowe.

Mambo mengi uliyoandika unauelewa finyu juu yake, hili andiko lako simply linathibitisha vile wajinga wakiwa wengi kwenye jamii wanaweza kutuchagulia Rais mjinga pia...
Nakubaliana na mchango wako, lakini mawazo yangu lazima yafike kwa Mbowe. Kuna kitu nakiona kama wamekuwa excited sana baada ya yule DIKTETA kufa na kuja Rais muungwana. Ninachotaka tu wasitumie uungwana wa Rais vibaya wasije wakatugharimu
 
Kwahiyo vyama vya siasa KAZI Yao ni kudai mambo Kwa serikali.

Tafsiri mpya hii.

Mimi ninavyoelewa vyama visivyokuwa na Dola kazi yake ni kuonesha mbadala wa Yale yanayofanywa na chama kinachoongoza serikali...
Mkuu tuchukulie uko sahihi kuwa cdm wanaharibu siasa za nchi hii, hebu nitajie vyama vinavyoboresha siasa za nchi hii na vipi.
 
Wewe ni wa kumwandikia Mbowe barua ya wazi? MATAGA leo ni wa kuishauri Chadema?
Unless umeingia JF recently Mimi ni kati ya JF members walikuwa wanawasha moto dhidi ya MATAGA na Lumumba Buk7.

Kama ni Mtanzania halisi Nina wajibu kukosoa CCM inapokosea na upinzani inapokosea.

Kwa mfano kwenye andiko hili nawashauri wakafanye mkutano Mkuu ili wajitathmini namna ambavyo utawala wa Mwendazake uliwaathiri kisha watengeneze dira na namna ya kuendesha Siasa zao na Rais mwenye haiba ya usikivu na uungwana.
 
Nakubaliana na mchango wako, lakini mawazo yangu lazima yafike kwa Mbowe. Kuna kitu nakiona kama wamekuwa excited sana baada ya yule DIKTETA kufa na kuja Rais muungwana. Ninachotaka tu wasitumie uungwana wa Rais vibaya wasije wakatugharimu
Wether they are excited or not, that's not an issue, Chadema wamekuwa wakitumia njia hiyo kudai haki zao toka enzi za Kikwete, then akaja Magufuli, na sasa ni zamu ya Samia, jinsia yake isitumike kama kigezo cha kuwaona wengine wabaya wakidai haki zao, kama hataki kusumbuliwa, atii na kufuata sheria zikiwemo za vyama vya siasa.

Mahaba yenu kwa "mama" msiyalete kwenye mambo ya msingi ya kitaifa yakawapofusha mpaka msione vile wengine wanavyokandamizwa haki zao kuminywa, kauli ya Mdude ni moja ya kielelezo cha wale walioonja machungu ya kudai haki yao na adhabu waliyopewa bila kosa lolote, mnaoona Mdude amekosea ni wale mliolewa utawala wa CCM.
 
Hapa umebwabwaja tu mkubwa, umepiga propaganda za ujinga wa siasa majitaka za maCCM ukidhani sote ni wajinga kama mlivyo huko....

Sijaona hoja yako. Hujui usemalo wala uzungumzalo...
Katiba nzuri mpya ni kitu kisichoepukika lazima tuipate siyo kwa hisia za Prof Shivji au Prof KABUDI, au Mbowe au Zitto, ni takwa la wakati.

Ni namna gani au wakati gani mwafaka kupata Katiba hiyo ndiyo panahitaji utulivu.

Tulitumia zaidi ya Tsh 350 Bilion mwaka 2014/5 na tukaletewa Rasimu Feki ya Chenge badala ya ile ya Warioba.

Busara na hekima vinahitajika hapa kuepuka makosa yaliyotokea mwaka 2014/5 kwani kitakachokuja kama Katiba kitakuwa ndiyo mwongozo wa nchi kwa miongo mingi ijayo.

Hizi pressure za CHADEMA na Mbowe za kumsukuma Rais SSH ndani ya siku 100 aanzishe mchakato wa Katiba siyo kwamba tu zimekosa adabu bali hazina muelekeo, hazionyeshi zinataka nini na zinapaswa kudhibitiwa na wana CHADEMA wenye busara.

Sikutegemea wangemleta MDUDE so quickly kwenye majukwaa aanze kuropoka vile dhidi ya Rais wakati akili yake inataka healing ya hali ya juu.

Strategists wa CHADEMA ni nani na wanafanya nini?
 
Kuna kiasi kikubwa huelewi(na wenzako) nini maana ya katiba na inatakwa kwa nini.Nendeni mbali zaidi bila kudhani ni vitabu tu vyenye maandishi vitachapishwa Kaa ujiulize:Kama ni kitu "chepesi" kwa nini CCM wakatae kuwa na mpya?Think and think and think bigger!
Nyie ndo mumedaganywa maendeleo yanahusisha vitu vingi pamoja na sera, tunaweza kuwa na katiba nzuri ila bila mikakati ya kujikwamua umaskini ukaendelea kuwepo tu
 
Nyie ndo mumedaganywa maendeleo yanahusisha vitu vingi pamoja na sera, tunaweza kuwa na katiba nzuri ila bila mikakati ya kujikwamua umaskini ukaendelea kuwepo tu
Unahitaji kubatizwa upya.Kamsome CCM music utamuelewa.😝😝😝😝
 
Nyie ndo mumedaganywa maendeleo yanahusisha vitu vingi pamoja na sera, tunaweza kuwa na katiba nzuri ila bila mikakati ya kujikwamua umaskini ukaendelea kuwepo tu
Unaweza kuwa na hoja lakini hata hizo sera kama hazisimamiwi na sheria hamna kinachofanyika. Kwani sasa hatuna sera? Sera tunazo ila sheria zinazosimamia hizo sera ndo zimekuwa kizungumkuti.

Katiba ni sheria mama kiasi kwamba mwelekeo chanya huzaliwa na katiba iliyobora kulingana na nyakati tulizonazo na zinazokuja.
 
Katiba nzuri mpya ni kitu kisichoepukika lazima tuipate siyo kwa hisia za Prof Shivji au Prof KABUDI, au Mbowe au Zitto, ni takwa la wakati.

Ni namna gani au wakati gani mwafaka kupata Katiba hiyo ndiyo panahitaji utulivu.

Tulitumia zaidi ya Tsh 350 Bilion mwaka 2014/5 na tukaletewa Rasimu Feki ya Chenge badala ya ile ya Warioba.

Busara na hekima vinahitajika hapa kuepuka makosa yaliyotokea mwaka 2014/5 kwani kitakachokuja kama Katiba kitakuwa ndiyo mwongozo wa nchi kwa miongo mingi ijayo.

Hizi pressure za CDM na Mbowe za kumsukuma Rais SSH ndani ya siku 100 aanzishe mchakato wa Katiba siyo kwamba tu zimekosa adabu bali hazina muelekeo, hazionyeshi zinataka nini na zinapaswa kudhibitiwa na wana CHADEMA wenye busara.

Sikutegemea wangemleta MDUDE so quickly kwenye majukwaa aanze kuropoka vile dhidi ya Rais wakati akili yake inataka healing ya hali ya juu.

Strategists wa CDM ni nani na wanafanya nini?
Unahitaji strategy gani kudai katiba mpya ya wananchi...?

Kudai lolote toka kwa watawala wa kisiasa ni kuwapigia kelele za kukera na kuudhi ktk masikio yao mpaka washindwe kulala wala kula...

Ndivyo hufanyika kokote pale. Ndivyo ilivyofanyika wakati wa Mwendazake Magufuli hata kumkera na kuanza kuchukua maamuzi mabaya, ya hasira yaliyomuathiri hata yeye na mwisho akajikuta anakufa kifo cha aibu....

Ndivyo itakavyofanyika kwa huyu mama ambaye kiuhalisia na mlaini na mwepesi kuliko wote. Akifanya kosa kidogo kwa kutochukua maamuzi ya busara na hekima before it's too late, ataishia kulekule alikoishia mwenzake waliyeingia naye madarakani...

Hayo mnayoyataka na mleta mada, fanyeni nyie kwani huko CHADEMA hatua ilishapitwa na kwa sasa wako kwenye utendaji na utekekezaji wa maazimio ya vikao vyote...
 
Rais anawajibika kufuata vipa umbele vya umma/wananchi, siyo vyake yeye binafsi na kikundi kidogo Cha watu wa chama chake🙄

Kwani ile nafasi amejiweka pale mwenyewe?!!!
Nani kakudanganya wewe.
Nafasi Ile hajajiweka, umama kwa maana ya majority ndio wamemuweka... Kikundi Cha watu wake ndio walipata majority, unasemaje kikundi kidogo . na Uchaguzi ndio unaweka vipaumbele vya Umma. Chama Cha siasa wakati wa kutengeneza ilani kinafanya tathmini ya mahitaji ya wakati huo na kuamua sisi tutafanya haya mkitupa ridhaa.
ILANI NDIO VIPAUMBELE.
Umma ungetaka Katiba ungewachagua walionadi Katiba Mpya ktk ilani zao.
Lakini la pili unapozungumzia Umma jaribu kuwa Specific kidogo.
Tafsiri yako ya Umma Ni wafuasi wa upinzani na Wanaharakati au una maana gani...
Naamini CCM ikisimama na kusema hatuoni haja ya Katiba bado zadi ya 50% ya Umma (entire population) wataona sawa.
 
Kwa nini mnaizungumzia Chadema tu na sio ACT, TLP, NCCR au CUF ?
Kwa sababu Chadema wanaamini wao ndio UMMA makundi mengine sio UMMA ndio maana wanadai Rais anatakiwa atekeleze matakwa ya UMMA (i.e. CHADEMA)😂😂
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom