Chadema yawasilisha barua Ofisi ya Bunge kufuatia sakata la kina Mdee

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,703
218,248
Kama walivyoahidi jana kwenye Mkutano wao na Waandishi wa habari , leo wamekamilisha .
---
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimewasilisha barua Ofisi ya Bunge la Tanzania, kikimkumbusha Spika wa Bunge hilo, Tulia Ackson kuwaondoa wabunge Halima Mdee na wenzake 18 bungeni, kikieleza kuwa si wanachama halali.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Jumatatu, Desemba 18, 2023 Katibu wa Chadema Kanda ya kati aliyepeleka barua hiyo, Emmanuel Masonga amesema pia wamepeleka nakala Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) pamoja na Ofisi ya Rais Ikulu.
 
Back
Top Bottom