Barua ya wazi kwa Rais Samia

Lituye

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
1,862
5,680
Madai ya uwepo wa KATIBA MPYA imekuwepo toka mwaka 1995 mfumo wa vyama vingi vya siasa ulipo anzishwa. Zimeundwa tume nyingi mno na marais tofauti ili kuona namna bora ya kuwa na KATIBA MPYA.

Tume ya mwisho kabisa ya hivi karibuni iliundwa na Rais Kikwete na ikakusanya maoni ya wananchi kutaka katiba mpya.

Sisi Watanganyika tunataka kujua uliyo yasema jana kuwa Watanganyika wanahitaji elimu ya katiba hii mbovu umeipata kwa maoni ya tume ipi?

Rais unayesema KATIBA iliyokuweka madarakani sio malikitu ni kajarida tu unataka kutupa Elimu wananchi kwa kijarida hicho kwa faida gani?

Ni mwanafunzi gani anakubali kufundishwa na mwalimu kihiyo kitu kisicho na faida?

Sisi Watanganyika tutakuonesha kuwa katiba yetu ni ya muhimu.

Mimi binafsi najua binadamu wana mapungufu ila ile kauli yako kuwa KATIBA ni kajitabu tu imenifikirisha sana kuwaza kuto kukusamehe kwa kuwa nawaza ulisema kwa makusudi.

Pia tambua utakapo tolewa madarakani ama kwa kura halali au kwa nguvu ujue huna wa kumlaumu kwa kuwa umesema mwenyewe katiba haipaswi kuheshimiwa.
 
Back
Top Bottom