Barua ya wazi kwa Mbowe & CHADEMA: Kajipangeni Upya

Hakuna watu waoga kuingia mtaani kama Watanzania. Alijaribu Mange Kimambi mwaka 2017/18 kuhamasisha maandamano kupitia Instagram hakuna hata mtu mmoja aliingia mtaani.

Baada ya uchaguzi wa 2020 ambao MAGUFULI aliuiba wote kupitia NEC na Polisi, Tundu Lissu aliitisha maandamano hakuna mtu alikwenda.

Urais ni Taasisi na siyo hivyo unavyochukulia wewe. Huyu unayemuona ni mwepesi kuliko MAGUFULI maamuzi yake yanaweza yakawa mabaya kuliko MAGUFULI.
Katiba mpya ya Tanzania IPO karibu sana kupatikana kipindi hiki kuriko awamu yeyote, tukaze buti tusiwasikilize wenye tabia ya kuridhika na nguo ya zamani!!! Hongera Mpambanaji wetu Kamanda Mbowe!!!
 
ndiyo maana miminaonaga hawa ni wahuni tu wakasome siasa hawaijui
Wewe na unaowatetea mlikosa hoja za msingi tangu siku za mwendazake, ndo maana wamnakimbilia na kushangilia mabavu badala ya zinazojenga na kulinda haki na utawala bora.
 
Sema na ninyi mnazidi,mtu Raisi Samia kaamua kuwa muungwana,lakini ni kama mnataka kumpanda kichwani sasa,watu walikuwa washakimbia mpaka nchi,hatuwasikii tena,lakini sasa imekuwa ni vurugu na vitisho tu,kwani hakiwezi kutafutwa muafaka kiungwana tu kama Mama anavyoonesha kuwa muungwana?
Wewe ni wa kumwandikia Mbowe barua ya wazi? MATAGA leo ni wa kuishauri Chadema?
 
Kwako Freeman Mbowe,
Mwenyekiti wa CHADEMA

Ni wazi CDM mnapoteza focus maana Kama alivyosema E Lowassa mwaka 2015 kuwa Chama chenu ni wana harakati zaidi kuliko wanasiasa. Wanaharakati huenda na matukio wakati wanasiasa huenda na mikakati.

Kuna mabadiliko makubwa ya kisiasa, kijamii na kiuchumi ambayo yamefanywa ndani ya kipindi cha miezi 3 au siku 100 katika utawala wa Rais SSH. Watanzania wote wanajuwa na wanaona nafuu ya maisha katika nyanja zote na wana matumaini na Rais. Sina haja ya kuyataja hapa ambayo Rais SSH amefanya kwa kuwa mengine hata Mbowe binafsi ni mnufaika wa moja kwa moja.

Sijapendezewa na Uongozi wenu wa juu wa CDM namna mnavyotaka KIUMSHURUTISHA Rais afuate VIPUMBELE vyenu badala ya vipaumbele vyake na Chama chake.

Hata kama kuna mapungufu katika vipaumbele vya Rais, naamini kuna namna ya kufikisha ujumbe kwa Rais kwa maadili na nidhamu. Kumbukeni Rais ni Taaaisi

Najuwa CHADEMA mumeomba kukutana na Rais, na Rais bado hajaonyesha atakutana nanyi lini. Hili nalo linakuwa shida kwa kuwa nyinyi akina Mbowe mnaona alipaswa aonane na CHADEMA kwanza kabla ya makundi mengine ambayo Rais amekutana nayo.

Juzi mwanachama wenu mmoja (MDUDE) ameachiwa na Mahakama ya Mbeya kwa makosa ya kusafirisha cocaine. Badala mumuache kwanza apumzike ili aboreshe saikolojia na afya ya akili, nyie mumemempandisha kwenye majukwaa na ameanza kumtishia Rais SSH.

Jana mkutano wa dinner wa akina Mama wa BAWACHA uliopangwa kufanyika pale Hekima Garden ulivunjwa na Jeshi la Polisi. Naomba mjue kuwa Serikali ipo, na hai hezewi.

USHAURI WANGU:
CHADEMA wakumbuke kuwa Rais SSH siyo Kiongozi wa CCM na CHADEMA pekee bali ni Kiongozi wa Watanzania wote walio kwenye vyama na wasio na vyama. Kazi ya Samia tumeiona kwa muda mfupi na tuna matumaini kuwa yuko kwenye MSTARI SAHIHI na kuna makubwa nchi yetu itapata chini ya Uongozi wake.

Ametupa Uhuru wa kuongea na kushauri kwa mujibu wa Katiba, tuutumie vizuri kwa masilahi mapana na nchi yetu.

Katiba Nzuri kweli tunaitaka na Rais SSH kasema tumpe muda kwanza aratibu mipango yake ya uchumi, then suala la Katiba litakuja. Kwa nini tusimpe benefit of doubt Rais wetu kwa hilo? Maana mtangulizi wake (Magufuli) alisema "Kwenye Kampeni zangu sikuahidi Katiba". Ila huyu Samia anasema tumpe muda tu, nyinyi hamutaki.

Na kwa miaka 5 CHADEMA walikuwa wanaongelea Tume Huru Ya Uchaguzi, kuibiwa kura za uchaguzi na kesi za kubambikizwa. Sasa ndiyo wameanza kudai Katiba naada ya DIKTETA Magufuli kufariki.

Nawashauri CHADEMA, waitishe Mkutano wao Mkuu ili waweke mkakati wa nini wanachokitaka na siyo kila mwenye kusimama jukwaani anataka cha kwake. Wawatumie vijana wao wasomi waandike dira yao na miongozo ya vitu gani wadai kutoka Seikalini.
Well said, ni kweli chadema waachane na matamko yanayo jenga chuki na hisia hasi kwa Rais. Vinginevyo itaonekana ni kutaka kupima kina cha maji, na hivyo watakabiliwa na nguvu ya mkono wa chuma. Na zaidi itawafanya watu kuamini kuwa Magufuli alikuwa sahihi kuwanyima jukwaa wapinzani.

Waibue hoja na kero zinazo mgusa mwananchi wa kawaida kama ilivyokuwa enzi za Dr. Slaa, katiba iwe ni hoja ya nyongeza

Sent from my TECNO F3 using JamiiForums mobile app
 
Sisi Watumishi wa Umma tumeshapandishwa Madaraja na Nyongeza zetu kwa hiyo tunashauri kila mmoja aangalie Maslahi yake
 
CDM hiyo katika mpya muiweke kwenye ilani yenu ya 2025 mkaiombee kura waacheni CCM watekeleze ilani yao waliyoiombea kura...nyie subirini 2025 kwenye ilani yenu muiweke katiba mpya halafu mje kuinadi tuwape ridhaa..
Uchakuzi gani watashiriki bila tume huru?
 
CDM wanazingua mama kaanza vizuri hafu hata hyo katiba wanayolilia ndo itabadilisha umaskini,Bora basi wangekuja na kipaumbele Cha kuondoa umaskini na ajira kwa vijana ambao ni wengi kwenye hili taifa. Waje na agenda ya kugusa watu wengi ila blah blah za katiba tu bila kuondoa umaskini it doesn't make sense.
Badala ya kutushawishi kwa sera nzuri wanalilia katiba, kwa hiyo wao tukiwapa nchi kipaumbele chao ni katiba mpya, mambo ya ustawi wa nchi tutapambana wenyewe.
 
CDM wanazingua mama kaanza vizuri hafu hata hyo katiba wanayolilia ndo itabadilisha umaskini,Bora basi wangekuja na kipaumbele Cha kuondoa umaskini na ajira kwa vijana ambao ni wengi kwenye hili taifa. Waje na agenda ya kugusa watu wengi ila blah blah za katiba tu bila kuondoa umaskini it doesn't make sense.
Hawa inatakiwa wakong'otwe tu hawana akili
 
Tatizo lilipo kwa sisi wantanzania mtu anapokuwa na mawazo kinzani na mawazo yako huonekana ni adui na msaliti . Lakini kumbe inawezekana kuchukua yale mawazo kinzani na kuyafanyia kazi ama kuoutweigh kwa hoja iliyo bora zaidi.

Cha msingi zaidi hatujikiti katika kuwaza katika changamoto zetu za msingi ili tuweze kujinasua hapa tulipo.
 
Sababu zilizotolewa na raisi zina mashiko, ndio kwanza ameingia madarakani ana vipa umbele vyengine. Na wakati huo huo yuko katikati ya covid crisis (janga la kiafya).

Ukitazama maneno ya raisi hajasema kama hatoshughulikia suala la katiba. Amesema watu wavute subra, nadhani anastahili kupewa muda kidogo. Binafsi mambo aliyoyafanya kwenye kusimamia haki na watu wasio na hatia kutolewa magerezani naunga mkono hoja apewe muda kidogo (kama mwaka ivi).

Janga la covid inshallah liko njiani kuisha.Kwenye nchi ambazo zinachanja na watu wake sio wabishi nadhani mwisho wa mwaka huu asilimia kubwa itakuwa ishachanjwa na watu washarudi kwenye hali za kawaida. Hivi naandika mataifa mengi yashaondoa utaratibu kama wa kuvaa barako, imebakia 1.5m ambayo huenda mwishoni ikaondoka pia na kurudi kwenye full turbo charge.
Asante kwa mawazo chanya. Busara inahitajika sana kuliko HARAKATI. Wananchi wanamuelewa Rais Samia sana kuliko hicho ambacho CDM wanataka kusema ni cha muhimu kuliko kupanga uchumi
 
Wachukue hatua kwa post yako ambayo haioni udhalimu, dhuluma, wizi na ufisadi wa maccm kwa miaka 60 ya kuwepo madarakani katika nchi yenye utajiri mkubwa wa rasilimali lakini haina chochote kile cha kujivunia!? Hebu tia akili kichwani acha KUKURUPUKA na kuandika upumbavu!
Miaka 60 kweli seriously CCM haina cha kujivunia? Hapo ndipo mnakosa objectivity. Kwa hiyo Tanzania iko kama alivyoiacha mkoloni? Kweli kama na wewe BAK uko kwenye safu za CDM, no wonder what we see and hear

Halafu eti wewe unanikuta mimi MPUMBAVU kwa vile uwezo wako wa kuelewa hoja zangu ni mdogo. Isitoshe hakuna tusi jipya yote yako kuanzia binadamu ameumbwa.
 
Badala ya kutushawishi kwa sera nzuri wanalilia katiba, kwa hiyo wao tukiwapa nchi kipaumbele chao ni katiba mpya, mambo ya ustawi wa nchi tutapambana wenyewe.
Katiba ndio kila kitu ndio maana wanaapa kuitetea na kuilinda kwa maana wanaongoza inchi kwa kisheria katiba muhimu
 
Ok Sasa kipi cha ajabu kwa CDM kudai katiba mpya?? Mpaka ukaamua kuwananga
Sijaona mtoa hoja alipowananga chadema zaidi ya kutaka waheshimu bilaumbele vya Rais na kutumia lugha ya staha.

Mdude kwenye mkutano wa bavicha baracuda alisema " nitamnyoa Rais kwa weembe ule ule niliomnyoa magufuli"
 
Kipi cha kujivunia? Elimu, Afya, uchumi, ajira, mshikamano vyote hovyo kabisa.

Mimi sijui kuremba kama unaandika upuuzi sijui kukwepesha.

Eti nawe una hoja?? 🤣🤣🤣🤣🤣
Kajisemea CAG Assad Acquired Stupidity disease!!!! Hoja zako za kipuuzi huko huko lumumba siyo humu. Unadhani ni kwanini maccm damu damu Butiku na Warioba wanapigia sana debe Katiba mpya!?

Unadhani kwanini Mkapa alitaka sana uchaguzi wa mwaka jana usimamiwe na Tume huru ya uchaguzi?

Hebu acha kuonyesha ujuha wako hadharani eti nawe una hoja!!! Hoja za kuwakumbatia majizi, mafisadi na wauaji wa maccm si hoja ni takataka tu.

Miaka 60 kweli seriously CCM haina cha kujivunia? Hapo ndipo mnakosa objectivity. Kwa hiyo Tanzania iko kama alivyoiacha mkoloni? Kweli kama na wewe BAK uko kwenye safu za CDM, no wonder what we see and hear

Halafu eti wewe unanikuta mimi MPUMBAVU kwa vile uwezo wako wa kuelewa hoja zangu ni mdogo. Isitoshe hakuna tusi jipya yote yako kuanzia binadamu ameumbwa.
 
Mbowe jana,amesema hawapiga magoti kukutana na SSH..wala hawabembelezi..
Bottom line,inaonekana mbowe anaona amechelewa kuitwa kuongea na SSH,
Anasahau kuwa maneno yake ya shombo dhidi ya SSH,Kama hili la eti hawabembelezi na hawana mpango ndo yanafanya SSH achelewe kuwaita,,
Hata JPM alikua anawapenda wapinzani,wakamtibua,,mar aambiwe eti PHD yake ni fake,hana elimu na kwamba ametia hasara nchi kununua ndege,etc
 
Sijaona mtoa hoja alipowananga chadema zaidi ya kutaka waheshimu bilaumbele vya Rais na kutumia lugha ya staha.

Mdude kwenye mkutano wa bavicha baracuda alisema " nitamnyoa Rais kwa weembe ule ule niliomnyoa magufuli"
Mdude sasa kawa milionea,,tulimchangia milioni 20 juzi tu
 
Mbona hata katiba iliyopo Ina mazuri mengi ukiondoa ku I favor ccm madarakani ila changamoto ya hii nchi yetu Bado umaskini na sip katiba. Katiba inaweza kuwa nzuri bila mipango ya kukuza uchumi na umaskini hatutavuka sehemu. Kenya Wana katiba nzuri ila umaskini uko palepale
Mkuu cariha ongeza sauti
 
Ningekuwa nimebwabwaja usingesoma na kunijibu. Ila umeona hoja. Nikuhakikishie kuwa Tanzania haina CONTROL kwenye Bei za mafuta bali ni nguvu ya soko (supply & demand). Mwaka jana tuli enjoy price ya mafuta hadi Tsh 1560/- kwa lita ya dizeli kwa kuwa shughuli za dunia zilipungua kutokana na COVID19. Demand iliteremka

Kuanzia Februari 2021 nchi nyingi hasa za ulaya zimefanya vaccinations hadi 40% ya population na maambukizi yamedhibitiwa na hivyo shughuli za uchumi na biashara zimepamba moto. As a result demand ya mafuta imepanda. Na Bei inapanda
Ndoo maana Russia na Saudi arabia,wamekaa na kuamua kuongeza supply ya mafuta,kwani matumizi yanapanda kwa sasa na kufanya bei ipae..
 
Mbowe jana,amesema hawapiga magoti kukutana na SSH..wala hawabembelezi..
Bottom line,inaonekana mbowe anaona amechelewa kuitwa kuongea na SSH,
Anasahau kuwa maneno yake ya shombo dhidi ya SSH,Kama hili la eti hawabembelezi na hawana mpango ndo yanafanya SSH achelewe kuwaita,,
Hata JPM alikua anawapenda wapinzani,wakamtibua,,mar aambiwe eti PHD yake ni fake,hana elimu na kwamba ametia hasara nchi kununua ndege,etc
Freeman Mbowe tunamjua kuliko Wana Chadema wanavyomjua.

Hivi kweli mtu aliyeng'ang'ania UENYEKITI wa Chama kutoka mwaka 2000 na haruhusu wengine wagombee (kumbuka Chacha Wangwe na Zitto Kabwe), kweli ana moral authority ya kudai KATIBA?

Hivi kweli tumkague anavyoteua wale akina mama kuwa wabunge wa Viti maalum miaka yote kweli anafuata Katiba ya Chadema?
 
35 Reactions
Reply
Back
Top Bottom